Mmiliki wa timu wa klabu ya Azam FC, Yusuf Bakhresa jana Jumamosi mchana alikutana na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kuwapongeza kutokana na ushindi wa mchezo uliopita wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Simba na kuwatakia kila la kheri katika mechi zijazo.