Mabao ya Lionel Messi na Julian Alvarez yametosha kuivusha Argentina kwenda robo Fainali katika Kombe la Dunia 2022 Qatar baada ya kuifunga Australia mabao 2-1.
Argentina itacheza mechi ya robo fainali dhidi ya Uholanzi Disema 9 saa 4:00 usiku.
Australia imeaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo hicho dhidi ya Argentina.