Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Tegemea haya Ufaransa Vs Argentina, Uruguay Vs Ureno

Muktasari:

Mechi ya kwanza itapigwa katika uwanja wa Kazan, ulioko katika mji wa Kazan, kutazama mechi kati ya France na Argentina kuanzia saa 11 jioni, halafu baadae safari itaelekea Sochi, kilomita 2,0596 kutoka Kazan, kutazama mechi ya kukata na shoka kati ya Ureno na Uruguay, kwenye dimba la Fisht.

Moscow, Russia. Kombe la Dunia ndio kwanza inaanza. Baada ya kutenganisha pumba na mchele, hatimaye ulimwengu unajiandaa kushuhudia mtifuano wa kukata na shoka, raundi ya 16 bora inapoanza rasmi leo.

Mechi ya kwanza itapigwa katika uwanja wa Kazan, ulioko katika mji wa Kazan, kutazama mechi kati ya France na Argentina kuanzia saa 11 jioni, halafu baadae safari itaelekea Sochi, kilomita 2,0596 kutoka Kazan, kutazama mechi ya kukata na shoka kati ya Ureno na Uruguay, kwenye dimba la Fisht.

Mechi ya Ufaransa na Argentina inatajwa kama mchezo wa fainali iliyokuja mapema sana. Wakati Argentina walipata tabu sana kuvuka hatua ya makundi, Ufaransa mambo kwa yalikuwa laini tu. Walipata ugumu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Denmark tu.

Argentina iliyosubiri maajabu ya miguu ya Lionel Messi na Marcos Rojo kujikatia tiketi, wanaingia katika mchezo huu wakiwa na ari, kasi na nguvu kubwa na kwa sababu hiyo, itabidi dunia isimame katika dakika 90, kuwapisha mabwana hawa kufanya yao.

Hata hivyo, habari za kuchekesha ni kwamba, Jorge Sampaoli, mpaka sasa hajafahamu ampange nani kuwakabili Les Blues, huku kibarua kikubwa kikiwa ni kutafuta kombinesheni matata ya ulinzi kuwazuia Paul Pogba na wenzake. Utabiri wangu, Ufaransa watashinda. Ufaransa 1-0 Argentina.

Baada ya hapo tunaelekea Sochi. Ureno na Uruguay lazima wamalizane tu hakuna namna. Walianza kwa kusuasua, wakifunga bao moja katika dhidi ya Egypt na Saudi Arabia, kabla ya kuishindilia Russia 3-0, Uruguay walimaliza hatua ya makundi bila kufungwa.

Kwa upande Ureno, walianza kwa kutoa sare ya 3-3 na Spain katika mchezo uliomshuhudia Cristiano Ronaldo akizama kambani mara tatu ‘hat-trick’, kabla ya kuinyorosha Morocco 1-0 halafu wakalazimishwa sare ya 1-1 na Iran.

Kwa matokeo hayo, tegemea kushuhudia mchezo mkali kwani mafahali hawa wana historia ya kuwa na uhasama, ikizingatiwa kuwa Ureno ndio waliowatawala Spain. Kikosi cha Oscar Tabarez, wanaonekana kuwa fiti na tayari kumaliza mchezo ndani ya dakika 90.

Ureno wanajivunia uwepo wa Cristiano Ronaldo na Ricardo Quaresma kikosini huku upande wa pili wakikenua kutokana na uwepo wa Luis Suarez na Edison Cavani katika kambi yao. Moto utawaka sio kidogo mwanangu. Tegemea Uruguay kuwapiga Ureno. Uruguay 1-0 Ureno.