Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Russia yachafua CV ya Fifa mapema

Muktasari:

  • Uamuzi umekuja mara baada ya Russia kugundulika kuhusika na ubaguzi wa rangi kupitia nyimbo zilizoelekezwa kwa kiungo ghali duniani, Paul Pogba na wachezaji wenzake wenye asili kama yake katika mchezo wa kirafiki mwezi Machi.

UWEZO wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuwalinda wachezaji wenye asili ya Afrika, viongozi mbalimbali wa soka, na mashabiki dhidi ya ubaguzi wa rangi katika Fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Russia, unatiliwa shaka baada ya kushuhudia wenyeji Russia wakipigwa faini ya Pauni 22,000 kwa kosa la kuwabagua wachezaji wa Ufaransa.

Uamuzi umekuja mara baada ya Russia kugundulika kuhusika na ubaguzi wa rangi kupitia nyimbo zilizoelekezwa kwa kiungo ghali duniani, Paul Pogba na wachezaji wenzake wenye asili kama yake katika mchezo wa kirafiki mwezi Machi.

Kitengo maalumu kinachohusika na upingaji wa ubaguzi wa rangi cha Fifa kimekiita kitendo hiki ni cha kusikitisha na kuonya kuwa inaweza kusababisha kuwepo kwa vitendo vingine vya ubaguzi katika fainali hizo msimu wa kiangazi.

Kuhabarika zaidi, pakua HAPA jarida letu la #KombelaDunia2018 linaloletwa kwako na magazeti uyapendayo ya Mwananchi  na Mwanaspoti.