Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Penalti ya Kyle Walker yazua mjadala

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Manchester City alionekana kwenye kamera za runinga akimdhibiti mchezaji wa Tunisia, Fakhereedine Ben Youssef eneo la hatari jambo ambalo lilisababisha mwamuzi kutoa penalti.

Mkongwe wa soka England, Rio Ferdinand ameelezea faulo iliyosababishwa na Kyle Walker na kuwapatia bao la kusawazisha Tunisia jana Jumatatu usiku, lilikuwa ni kosa la kimchezo.
Nyota huyo wa Manchester City alionekana kwenye kamera za runinga akimdhibiti mchezaji wa Tunisia, Fakhereedine Ben Youssef eneo la hatari jambo ambalo lilisababisha mwamuzi kutoa penalti.
Ferdinand amesema kwamba tukio hilo lilitokea kwa bahati mbaya jambo ambalo likazalisha lipenalti na kuwapa ushindi Tunisia.
Hata hivyo kosa ambalo Ferdinand analiona ni beki huyo kucheza faulo eneo ambalo halikuwa upande wake jambo ambalo lilitokea kwa bahati mbaya.
Alisema kosa jingine ilikuwa ni wakati akiokoa hatari hiyo hakuwa anamuangalia adui, hivyo macho yake alikuwa ameelekeza mbele kwa kipa na akajikuta mkono wake unampiga adui na kusababisha kutolewa adhabu ya penalti.
Baada ya mchezo huo kumalizika, Walker alisema wakati anauacha mpira udunde hakujua kuwa kulikuwa na adui nyuma yake hivyo alimzuia bila kukusudia. Pia akasema ingekuwa ni kwenye Ligi Kuu jambo hilo haamini kama ingekuwa ni adhabu.