Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uruguay vs Ureno: Vita ya Ronaldo dhidi ya Suarez, Cavani

Sochi, Russia. Ukiacha mandhari mazuri, wanawake wazuri na vyakula vizuri. Mambo yanazidi kunoga nchini Russia unaambiwa. Baada ya Ufaransa na Argentina kuoneshana ubabe kule Kazan, macho na masikio yanaelekezwa katika mji wa Sochi.

Majira ya saa tatu usiku, mashabiki wapatao 40,000, watafurika katika uwanja wa Fisht, ulioko katikati mwa mji wa Sochi, yapata kilomita 2,059.6, yaani umbali wa saa 27, kutoka Kazan, kutizama mtanange wa kukata na shoka kati ya Ureno na Uruguay. Patachimbika mwanangu!

Ugumu wa mchezo huu unatokana na rekodi nzuri iliyoandikishwa na Uruguay katika hatua ya makundi. Ni hivi, hadi wanaingia 16 bora, Uruguay pamoja na Croatia, wanajivunia kucheza mechi zote bila kuruhusu nyavu zao kuguswa.

La Celeste, wanaelekea Sochi wakiwa na kiburi balaa. Hawaogopi kitu na wala hawan sababu ya kuogopwa ka sababu pale mbele wapo mapacha wawili hatari, Luis Suarez na Edinson Cavani. Nyuma amesimama beki kisiki wa Atletico Madrid, Diego Godin na Jose Gimenez. Wanaanzaje kuogopa kwa mfano?

Luis Suarez, ametupia kambani kwenye Kombe la Dunia mara saba, katika historia ya taifa lake na anashika nafasi ya pili, nyuma ya Oscar Miguez mwenye mabao nane. Katika hatua ya 16, Suarez anakumbukwa kwa mabao mawili aliyofunga dhidi South Korea (2010).

Turudi kwa Ureno. Mshindi wa Ballon D'or mara tano, Cristiano Ronaldo ameonesha uwezo wake katika michuano hii, akitupia wavuni mara nne na kuivusha Ureno. Mechi ya kwanza akitupia hat-trick. Mreno huyu ataisumbua Uruguay sio kidogo.

Hata hivyo, licha ya kuibeba Ureno kwenye hatua ya makundi, Cristiano Ronaldo ana rekodi mbaya na hatua ya 16 bora kwani takwimu zinaonesha kuwa baada ya kuingia dimbani kwa zaidi ya dakika 424 kwenye Kombe la Dunia zilizopita, fowadi huyu wa Real Madrid, mwenye umri wa miaka 33, hajafunga bao hata moja.

Ukiachana na mikwaju ya penalti, Ureno imepoteza mara moja tu katika mechi 17 walizocheza katika mashindano makubwa. Wameshinda mara nane, wakatoka sare mara nane, wakifungwa mara moja. Walipigwa 4-0 na Ujerumani, huko Brazil (2014).

Kwa upande wao, Uruguay wanaonekana kuwa hatari kwenye mipira iliyokufa. Katika michuano ya mwaka huu, mabao yao tano yamefungwa kwa njia ya Mpira wa adhabu 'freekick' na kona. Ureno wao wamefunga mabao matatu kwa shuti wakiwa nje ya boksi.