Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wewe ni mchezaji unayefunga swaumu, soma hapa!

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Waislam wameanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambayo ni nguzo ya nne kwa mujibu wa dini hiyo na iliyohimizwa katika Qur'an kupitia sura ya Al Baqara 2:183 ikisema; "Enyi mlioamini mmefaridhishiwa Swaumu (Ramadhani) kama waliofaridhishiwa waliokuwapo kabla yenu ili mpate kumcha Mungu." Tena aya zinazofuata zinafafanua masiku yenyewe ni machache tu (siku 29 au 30).

KWA mara nyingine, waumini wa dini ya Kiislam na Kikristo wameingia katika kipindi muhimu cha ibada ya kufunga kama wanavyohimizwa na dini zao.

Waislam wameanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambayo ni nguzo ya nne kwa mujibu wa dini hiyo na iliyohimizwa katika Qur'an kupitia sura ya Al Baqara 2:183 ikisema; "Enyi mlioamini mmefaridhishiwa Swaumu (Ramadhani) kama waliofaridhishiwa waliokuwapo kabla yenu ili mpate kumcha Mungu." Tena aya zinazofuata zinafafanua masiku yenyewe ni machache tu (siku 29 au 30).

Kadhalika Wakristo leo ilikuwa ni siku ya Jumatano ya Majivu tayari kwa mfungo wa Kwaresma unaochukua siku 40 wakirejea kile alichokifanya Bwana Yesu Kristo kama ilivyondikwa katika vitabu vyote vinne vya Injili, ikiwamo Matayo 4:2 inayosema;

"Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa." Luka 4:1-2 inaeleza juu ya funga ya Yesu. Pia Musa alifunga kwa siku 40 kama ilivyoandikwa katika Kumbukumbu ya Torati 9:9 na Kutoka 34:28-35 na vitabu vingine, lakini Yesu Kristo pia amefundisha katika Matayo 6:16-18 jinsi ya kufunga, ili kila mtu alipwe ujira na Mungu aliye sirini.

Kwa kifupi kwa sasa watu wapo katika mfungo unaowagusa hadi wachezaji wa soka na wanamichezo wengine katika utekelezaji wa ibada hiyo ya kufunga swaumu.

MFU 01

Mwanaspoti linakuletea kwa uchache dondoo muhimu ya mambo ya msingi ambayo wachezaji wa soka na wanamichezo kwa ujumla wanaoendelea na majukumu yao katika kipindi hiki cha swaumu ili kulinda afya zao na kuwa na ufanisi uwanjani sambamba na kutekeleza ibada kwa imani zao.


IBADA NA MAHITAJI

Kipindi hiki cha mfungo ni kipindi cha ibada, nidhamu na kujitathmini kwa waumini duniani kote. Kwa wachezaji wa soka wanaofunga, changamoto huwa kubwa zaidi kwa sababu wanapaswa kuunganisha ibada na mahitaji makubwa ya mwili yanayotokana na mazoezi na mechi.

Katika ligi mbalimbali duniani, tumeshuhudia wachezaji wakubwa kama Mohamed Salah, Karim Benzema na Sadio Mane wakicheza katika kiwango cha juu wakiwa wanafunga. Hata hapa Tanzania wapo wachezaji wanaotekeleza ibada za funga huku wakiendelea kucheza kwa ufanisi mfano kina Feisal Salum, Mudathir Yahya na wengineo.

Hii inaonyesha kuwa inawezekana mtu kufunga na kuendelea na jukumu lake uwanjani kama kawaida, lakini inahitaji maandalizi sahihi, uelewa wa kisayansi wa mwili, na usimamizi mzuri wa ratiba.

MFU 02

1. Lishe bora wakati wa futari na daku

Lishe ni nguzo kuu kwa mchezaji anayefunga. Mwili unapokosa chakula na maji kwa saa nyingi, hifadhi ya nishati hupungua. Hivyo, wakati wa futari na daku, mchezaji anapaswa kula vyakula vyenye virutubisho kamili.

Wanga (complex carbohydrates) kama wali wa kahawia, viazi, tambi au mkate wa ngano husaidia kutoa nishati ya kudumu.

Protini kutoka kwenye nyama isiyo na mafuta mengi, samaki, mayai au kunde husaidia kurekebisha misuli.

Matunda na mboga hurejesha vitamini na madini muhimu.

Maji ya kutosha ni lazima ili kuzuia upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Inashauriwa kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi au sukari nyingi wakati wa futari, kwani vinaweza kusababisha uchovu na uzito usiohitajika wakati wa mazoezi.


2. Zuia upungufu wa maji mwilini

Moja ya changamoto kubwa kwa mchezaji anayefunga ni kukosa maji mwilini hasa kama mechi au mazoezi yanafanyika katika hali ya joto kali kama hali iliyopo kwa sasa hususani jijini Dar es Salaam na miji ya Pwani.

Upungufu wa maji unaweza kusababisha:

- Kupungua kwa nguvu na kasi

- Maumivu ya kichwa

- Kukaza kwa misuli

- Hatari ya kuzirai

Hivyo basi, wachezaji wanapaswa kunywa maji taratibu na kwa wingi kati ya futari na alfajiri wakati wa daku kwa wale wanaotekeza sunna hiyo ya kula daku.

Vinywaji vyenye madini (electrolytes) vinaweza kusaidia kurejesha chumvi muhimu mwilini.

MFU 03

3. Mpangilio wa mazoezi

Makocha wanapaswa kupunguza makali ya mazoezi wakati wa Ramadhani. Badala ya mazoezi mazito mchana, ni vyema yafanyike:

Baada ya futari au karibu na muda wa kufuturu ili mchezaji aweze kula mara tu baada ya mazoezi

Mazoezi yanapaswa kulenga zaidi mbinu (tactical training) kuliko nguvu nyingi za mwili. Pia, muda wa mazoezi uwe mfupi ili kuepusha uchovu kupita kiasi.


4. Usingizi, mapumziko

Kwa kipindi hiki cha mfungo hususani wale wanofunga Ramadhani hubadilisha ratiba ya kawaida ya usingizi kwa sababu ya ibada za usiku na kuamka kwa daku.

Hivyo, wachezaji wanashauriwa:

- Kulala mapema iwezekanavyo baada ya swala za usiku

- Kupata usingizi wa mchana (power nap) ikiwa inawezekana

- Kuepuka matumizi ya simu au vifaa vya kielektroniki muda mrefu usiku

- Usingizi wa kutosha husaidia mwili kupona, kuimarisha kinga na kuongeza umakini uwanjani.


5. Ushauri kwa Bodi ya Ligi

Ili kulinda afya ya wachezaji wanaofunga, viongozi wa Ligi na waandaaji wa mashindano mbalimbali wanapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

MFU 04

(a) Ratiba mechi za mchana wa jua kali

Mechi zinazochezwa mchana wakati wa joto kali zinaongeza hatari ya upungufu wa maji mwilini na uchovu mkubwa. Ni busara kupanga mechi:

Jioni karibu na muda wa kufuturu au usiku baada ya futari

Katika mashindano makubwa Ulaya kama yale ya Ligi ya Mabingwa mara kadhaa waamuzi huruhusu mapumziko mafupi ili wachezaji wanaofunga waweze kunywa maji au tende wakati wa kufuturu. Hii ni ishara ya heshima na uelewa wa mahitaji yao ya kiimani na kiafya. Kwa hiyo hata kwa Bodi ya Ligi na waamuzi watakochezesha ndani ya muda huo walifanye hivyo kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa siku za nyuma kipindi kama hiki kuonyesha uungwana.


(b) Mapumziko ya muda (Cooling Breaks)

Katika hali ya hewa ya joto, kuwe na mapumziko ya muda katikati ya kila kipindi ili wachezaji wapate nafasi ya kupumua na kupunguza joto mwilini. Kipindi hiki cha mfungo ndio iwe maradufu kusaidia wachezaji waliofunga iwe Kwaresima au Ramadhani.


(c) Ushirikiano na madaktari wa timu

Madaktari na wataalamu wa lishe wahusishwe moja kwa moja kupanga ratiba ya mazoezi na lishe ya wachezaji wanaofunga. Vipimo vya mara kwa mara vya afya vinaweza kusaidia kugundua dalili za uchovu au upungufu wa maji mapema.


6. Msaada wa kisaikolojia na kiroho

Ramadhani na Kwaresima si tu kipindi cha kufunga bali pia ni cha kuimarisha imani. Wachezaji wanaweza kupata nguvu ya kiakili na kisaikolojia kupitia ibada na nidhamu ya mfungo. Makocha na viongozi wanapaswa kuwapa mazingira yanayoheshimu imani zao bila kuwanyima haki yao ya kushiriki kikamilifu katika timu.

MFU 05
MFU 05

MSISITIZO

Wachezaji wa soka wanaofunga Ramadhani au Kwaresima wana uwezo wa kuendelea kung'ara uwanjani ikiwa watazingatia lishe bora, maji ya kutosha, usingizi wa kutosha na upangaji mzuri wa mazoezi. Aidha, waandaaji wa ratiba na viongozi wa ligi wana jukumu kubwa la kulinda afya za wachezaji kwa kuepuka mechi za mchana wa jua kali na kuruhusu mapumziko maalum pale inapohitajika.

Kwa mshikamano kati ya wachezaji, makocha, madaktari na viongozi wa mashindano, inawezekana kulinda afya za wachezaji wanaofunga huku wakidumisha ushindani na burudani ya soka kwa mashabiki duniani. Mwanaspoti linawatakia waumini wote mfungo mwema kwa ujumla!