Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kasi kwa wanasoka ni mtaji uwanjani

Muktasari:

  • Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool ya aliyeipa mafanikio lukuki, moja ya masharti aliyotaka ni kuwapiga bei, beki mkongwe Dani Carvajal na Ferland Mendy, akisema wachezaji hao hawataendana na mipango yake ya kiufundi.

WIKI hii moja ya habari kubwa katika medani ya soka, ni magwiji wa soka barani Ulaya, Real Madrid kuhusishwa kumnyakua kocha Mjerumani Jurgen Klopp wakati wa majira ya kiangazi.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool ya aliyeipa mafanikio lukuki, moja ya masharti aliyotaka ni kuwapiga bei, beki mkongwe Dani Carvajal na Ferland Mendy, akisema wachezaji hao hawataendana na mipango yake ya kiufundi.

Kama vile haitoshi, jamaa kasema anataka kuona winga mshambuliaji Mohamed Salah na beki wa kati Virgil Van Dijk ambao wote alikuwa nao Liverpool wanatua klabuni hapo.

Mipango ya Klopp inakumbusha kuwa mchezaji wa soka, kuwa na kasi ni mtaji mkubwa kwake na timu kwa ujumla. Ukitazama wachezaji hao wa Madrid aliowasema, kasi wanayo lakini kwa sasa wana vikwazo.

Mfano Mendy, ni beki wa kushoto ambaye mara kwa mara amekuwa akipata majeraha ambayo yanamfanya kuwa nje muda mrefu.

Wakati Carvajal mwenye miaka 34 ni beki wa kulia ambaye tayari ameshacheza mechi 420 akipata vikombe vyote muhimu ikiwamo mataji 6 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huyu kikwazo ni kanuni ya kutumika sana na umri.

Tukirudi hapa nyumbani Tanzania, kiungo mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Kibu Denis tayari dili la kutua Al Nasr Benghazi ya Libya limekamilka na uongozi wa Msimbazi umeshamuaga rasmi.

Uhamisho huo ni dhahiri kuwa utimamu wa Kibu mwenye umri wa miaka 27 hauna shaka ikiwamo ustahimilivu na kasi yake. Unapokuwa na kasi ina maana mwili wake ni imara na hauna hali ya uvivu.

Ndio maana pale mchezaji anapoonyesha kuwa na kasi bila kuchoka hufuatiliwa kwa karibu ili kujua kama kasi yake ni ya asili au ya kuchochea na dawa za kuongeza nguvu. Ikiwa ni ya asili hapo ni bonge la mtaji katika kufanikiwa katika soka na kununuliwa klabu kubwa.


UKWELI KASI KWA WANASOKA

Hakuna uchawi katika kasi wanayochomoka nayo wanasoka kushambulia na kuzuia, ni uwezo binafsi unaochangiwa na vitu kadhaa ikiwamo umri, mwili, nidhamu, mazoezi na juhudi binafsi.

Lakini linapokuja suala la wachezaji wanapokuwa viwanja vya nyumbani huku wakiwa na washabiki wao wenye wazimu wa soka inakuwa ni habari nyingine.

Haishangazi mchezaji kama Salah au Kylian Mbappe, kuwa na kasi katika mchezo wenye upinzani mkali hii ni inatokana na mashabiki, benchi la ufundi na wachezaji anaocheza nao wanamfanya kuwa na ari ya juu ya ushindi.

Kukosa ari ya ushindi ni sawa na kuwa na nyumba bila paa, ari ya ushindi inaweza kumfanya mchezaji kuwa na hisia nzuri hivyo kuweza kujituma bila kuchoka na kusaka ushindi.

Umri wa wanasoka wenye kasi ni miaka 17-24, misuli huwa ni michanga ambayo bado haijachoka hivyo kuwa myepesi kupokea mazoezi na kujijenga vyema na kuwa na utimamu imara wa mwili.

Miili ya wanasoka wenye maumbo ya wastani unawafanya kuwa wepesi mwenye uwezo wa kupanda kushambulia na kurudi kasi kuwakaba maadui zao.

Wanasoka wenye kasi huwa wamezoea mazoezi na kuwa sehemu ya maisha yao hivyo kushikamana na mazoezi ya timu na yale binafsi ikiwamo mazoezi ya gym na viungo.

Ukimtazama mchezaji mwenye sifa ya kasi huwa si wavivu, huwa na juhudi binafsi, wanajituma bila kuchoka, wanapopoteza mpira hata kama kachoka atakaza kurudi kukaba.

Mwili wa mwanadamu una takribani zaidi ya misuli 650 ambayo kama ikijengwa vyema huweza kufanya mengi ikiwamo kuupeleka mwili kwa kasi kama vile beki wa zamani wa Yanga Shadrak Nsajigwa.

Nidhamu ya hali ya juu na tabia njema ni moja ya nyenzo kwa mwanasoka kufanikiwa kufanya mazoezi na kufuata maelekezo mbalimbali hivyo kucheza kwa kiwango cha hali ya juu akiwa na kasi.


FAIDA YA MCHEZAJI MWENYE KASI

Kutawala mashambulizi

Moja ya mambo makubwa ambayo kila timu inayotaka kushinda huhitaji ni kuwa na wachezaji wenye kushambulia kwa kasi, kuvunja ngome ya mpinzani, kuwazidi mbio mabeki na kufunga.

Wanasoka wote wanahitaji kuwa na kasi uwanjani.  Kadiri mchezaji anavyokuwa na kasi ndivyo pia anavyocheza vizuri. Ingawa kasi ya mpira wa miguu ni tofauti na michezo mingine.

Mara kwa mara mchezaji soka anahitaji kukimbia na mpira na anaweza kuhitajika kukimbia kawaida au kufunguka kwa kasi yenye nguvu kama anavyofanya Salah na Mbappe.

Kuwahi kuzuia mashambulizi

Mara nyingi kasi katika soka huhitajika mahali pasipotarajiwa, mfano mchezaji anaweza kuwa anakimbia kidogo kidogo lakini anaponyakua mpira anaweza kufunguka kwa kasi ili aweze kushambulia lakini pia lazima awe na kasi kurudi kuzuia mashambulizi anaposhambuliwa.

Vile vile mchezaji mkabaji atahitajika kufunguka ghafla kwa kasi ili kuweza kumzuia mshambuliaji ambaye si rahisi kukumkuta kama hana kasi ya ziada.

Hivyo ni kawaida kumwona mchezaji wa soka mara kwa mara kukumbana na mbio fupi fupi za kasi ambazo zinahitaji atumie nguvu kubwa kuweza kufanya hivyo.


Faida ya kimwili na kiakili

Wepesi wa kimwili kwa mchezaji kukimbia kasi kushambulia na kurudi kwa wakati kukaba huweza kuwavuruga kiakili wapinzani kiasi cha kuwapa hofu, kuwanyima nafasi ya kufikiri haraka hatimaye kuwa na uamuzi mbovu.

Kasi ya mwanasoka inajengwa kwa mazoezi tangu akiwa kinda na anahitajika kutumia akili na kutunza uwezo wake wa kuwa na kasi kwa kuzingatia programu nzima ya mazoezi anayopewa na wakufunzi.


Kuiweka mechi nzima mfukoni

Ili kuweza kudhibiti mechi nzima yaani mtaani wanasema kuiweka mfukoni timu inahitajika muunganiko wa wachezaji wenye kasi wenye ukakamavu, nguvu na stamina. Angalau nusu ya timu ikiwa na wachezaji hao inaweza kuleta matokeo makubwa.

Kwa wachezaji kama Kibu au Mbappe wameiva na wamekomaa kiukakamavu kitu ambacho kinawasaidia kukabiliana na ushindani na mazingira ya mechi ngumu zenye wachezaji wakali kama wao.

Unapokuwa na kasi na mwili mkakamavu ina maana kuwa mwili huo unaweza kudumu na kuvumilia mambo mengi ikiwamo kutopata majeraha ya mara kwa mara.


Kuwa hatua moja mbele zaidi

Mchezaji mwenye kasi ya ziada huwa ni mshindi wakati wa kushambulia au kuzuia, katika hali ya kubaki mchezaji mmoja kwa mmoja au wanapobaki wawili wakipambana.

Wachezaji kama Haaland, Salah na Mbappe akibaki na beki mmoja nafasi ya kufunga kwao huwa ni kubwa, kwa sababu kasi waliyonayo iko mbele zaidi ya mabeki.