Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Warembo wa Cape Verde na zali la Arsene Wenger

PAZIA Pict


ARSENE Wenger anapenda kupekua kila kitu. Alipofika Highbury pale London Septemba 1996 beki mahiri wa Arsenal, Tony Adams alikaririwa akisema: “Arsenal imeleta kocha ambaye ana akili kama mwanafunzi wa shule ya msingi.” Watu wote walicheka.


Ndivyo Wenger alivyo. Baadaye akawabadilisha Arsenal kuwa timu kubwa licha ya kutumia pesa kidogo. Waingereza wakamuita profesa. Sasa hivi akili hiyo ameipeleka Fifa. Ndiye ambaye anashughulika na mambo haya yanayoendelea sasa hivi katika mpira wa wakubwa kule duniani.


Baada ya kuachana na Arsenal, Wenger sasa hivi ni akili kubwa ya Fifa. Ndiye ambaye anapanga mipango hii mipya katika mipira. Mipango ambayo inaendelea ndani na nje ya uwanja. Mojawapo ni hili hapa la kuifanya michuano ijayo ya Kombe la Dunia kuwa na timu 48.

Ile michuano ya mwisho ambayo ilifanyika pale kwa Waarabu wenye fedha Qatar na ilijumuisha timu 32 tu. Na michuano mingine mingi iliyopita ilikuwa imejumuisha idadi hiyo ya timu. Ghafla Wenger na wajuzi wenzake wakafanya haya mabadiliko.

PAZ 05

Ghafla Afrika inaweza kuingiza timu 10 katika michuano hii ijayo ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika Marekani, Canada na Mexico. Timu tisa zitakwenda moja kwa moja katika michuano hii na nyingine inaweza kucheza hatua ya mtoano na watu wengine wa mabara mengine.

Na sasa kuna timu ambazo zimekwenda katika michuano hii kwa mara ya kwanza kama vile Cape Verde. Na kuna wengine wamefuzu ingawa kwa kaiwada kwa sasa hawana mbavu kubwa katika soka la Afrika. walishawahi kufuzu hapo nyuma, lakini kwa sasa hawana mbavu kubwa.

Inanikumbusha Taifa Stars yetu ambayo kwa sasa imefuzu mara tatu mfululizo katika michuano ya Afcon baada ya mabadiliko yaliyofanyika ya kuongeza idadi kubwa ya timu kutoka 16 hadi 24. Tukafanikiwa kufuzu mara nyingi na hata sasa tunasubiri kwenda zetu Morocco katika michuano mingine ya Afcon, Desemba mwaka huu.

PAZ 01

Kuna rafiki zetu wamefuzu kule Kombe la Dunia wanakwenda kutuwakilisha. Mfano ni Cape Verde ambayo pia imebarikiwa kuwa na warembo wazuri. Ukweli ni kwamba wamepiga hatua kubwa katika siku za karibuni, lakini zamani kidogo maisha yangekuwa magumu kwao.

Cape Verde ni koloni la Wareno na katika siku za karibuni wameamua kutoacha asili. Wanakusanya vijana wao waliozaliwa Lisbon kule kwa kina Cristiano Ronaldo na kuwaleta kucheza timu yao ya taifa. matokeo yake wamekuwa wasumbufu kwa mataifa makubwa ya Afrika.

Na sasa, kwa mfumo mpya wa kina Wenger wamekwenda moja kwa moja juu ya msimamo wa kundi lao na watacheza Kombe la Dunia kule Marekani, Canada na Mexico. Zamani kulikuwa na safari ndefu kidogo. Baada ya kufuzu hatua hii wangepaswa kucheza na Morroco ya Achraf Hakimi au Senegal ya Sadio Mane.

PAZ 04

Safari hii wamekwenda moja kwa moja. Makundi yamekuwa mengi na ukiongoza kundi unakwenda Kombe la dDunia huku wa pili anayefuata akiwa na pointi nyingi akisaka nafasi ya kucheza mtoano na washindi wa nafasi ya pili kwingineko. Tukiachana na Cape Verde wenyewe kuna wengine ambao wamekwenda kwa sababu kama hii. Mfano ni majirani zetu Afrika Kusini ambao wamefuzu pia mbele ya Nigeria. Hapa nitaandika kitu. Afrika Kusini imefuzu mbele ya Nigeria wakati Cape Verde imefuzu mbele ya Cameroon.

Kuna mataifa ya Afrika Magharibi ambayo yameshuka kisoka. Mfano hata Ghana ambao wamefuzu kwenda katika michuano hii. Kumbuka kwamba hawa walishindwa kufuzu katika michuano iliyopita ya Afcon. Hawana tena wachezaji kama kina Michael Essien, lakini mfumo huu ambao uliwafanya wajikute kundi moja na Madagascar, Mali, Comoro, Jamhuri ya Kati na Chad uliwafanya waende Kombe la Dunia.

Ina maana kuwa hata kama Ghana ingefeli kidogo tu, basi Madagascar wangeenda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. Naamini hii ni Ghana mbovu, lakini imefanikiwa kufuzu kwenda Kombe la Dunia kwa sababu ya mfumo huu mpya. Kama kundi lao lingekuwa na vigogo naamini wasingeweza kufuzu. Na kama wangelazimika kucheza hatua ya mtoano na vigogo wengine sidhani kama wangefuzu. Hata hivyo mabadiliko ya kina Wenger yamewafanya wafuzu.

PAZ 02

Ni kweli kwamba Afrika Kusini na Cape Verde zimefanikiwa kuzufu moja kwa moja mbele ya vigogo wasio bora kwa sasa katika soka la Afrika kama Cameroon na Nigeria hii, lakini licha ya kuongoza makundi wangelazimika kucheza hatua inayofuata na vigogo wengine wagumu zaidi kama mtindo ungekuwa uleule wa kutafuta timu tano kutoka katika Bara la Afrika.

Matokeo yake nadhani kuna timu ambazo sio bora sana, lakini zimefuzu kwenda Kombe la Dunia kule Marekani, Canada na Mexico. Na sio sisi tu kuna timu nyingi ambazo sio bora kutoka mataifa mengine, lakini zimefuzu Kombe Dunia lijalo. Wengine wamekwenda kwa mara ya kwanza.

Taifa kama Qatar limekwenda kwa mara ya kwanza kwa njia ya kufuzu baada ya kuandaa kama mwenyeji katika fainali zilizopita. Walikuwa dhaifu na nadhani wataendelea kuwa dhaifu kwa sababu hakuna mabadiliko ya msingi ambayo wameyafanya katika soka lao. Ni wachezaji wangapi wa Qatar wameenda nje kucheza soka la ushindani tangu michuano ile? Hakuna. Ni vile tu na Asia wameongezewa nafasi za kushiriki michuano hii.

PAZ 03

Mataifa kama Uzbekistan, Jordan na New Zealand pia nayo yamekwenda Kombe la Dunia. Kisa? Kina Wenger wametanua goli na maisha yamekuwa rahisi kufuzu katika michuano ijayo ya Kombe la Dunia. Mfano kule kwa New Zealand ilikuwa inakuwa ngumu kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa sababu mbabe wao alikuwa Australia. Baadaye Australia akaona anajichosha kushiriki mechi za kufuzu kule bara lao kwa sababu alikuwa hapati changamoto nzuri ya kufuzu akahamia Asia.

New Zealand ambaye alikuwa mchovu siku zote kule ghafla akageuka kuwa mbabe katika nchi ndogo ambazo ukubwa wa eneo zinalingana na Wilaya ya Kibaha. Kwa mabadiliko haya hatimaye naye amefuzu Kombe la Dunia.

Nini tutegemee? Nadhani tutegemee matokeo ya kuchekesha katika michuano ijayo ya Kombe la dDunia. Nadhani tunaweza kupata matokeo ya mabao 10-0 kwa timu ambazo zimepitishwa kwa mabadiliko haya ambayo hata Taifa Stars ingeweza kufuzu.

Kama Jordan inapangwa kundi moja na Ufaransa yenye Kylian Mbappe na Ousmane Dembele pale mbele, basi tunaweza kushuhudia matokeo yenye aibu katika michuano ya Kombe la Dunia. Timu nyingi hazikutani pale kwa sababu ya ubora wao, bali kwa sababu ya idadi iliyotakiwa na kina Wenger.

Hii ndio sababu sisherehekei sana kina Cape Verde kufuzu au kina Afrika Kusini kurudi tena katika michuano hii. Wanaweka historia, lakini kwa mfumo uliopo sasa sioni maajabu makubwa sana kwao kufuzu. Na timu ambazo zinaweza kutuwakilisha vyema kutoka bara hili zitabaki kuwa zilezile tu.