Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakubwa Bara na maajabu yao CAF

PUMZI Pict


TIMU zote nne za Tanzania zimetolewa katika mashindano ya kimataifa msimu huu baada ya kushindwa kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.


Umekuwa msimu wa kihistoria kwa namna zote mbili, chanya na hasi.


Chanya ni kwamba kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa kuingiza timu nne hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika...kitu kikubwa sana!

Hasi ni kwamba kwa mara ya kwanza, hakuna timu ya Tanzania iliyotinga hatua ya robo, tangu iwe tabia kwa nchi yetu kufuzu hatua ya makundi tangu msimu wa 2018-2019.

Yote kwa yote umekuwa wakati mzuri sana kwa Tanzania, kikubwa ni kuifanya hii kuwa tabia kwa timu nne kufuzu hatua ya makundi.

Hata hivyo, msimamo wa jumla wa timu za Tanzania umekuwa wa kushangaza sana.

Simba ambao ndio wababe wa michuano ya kimataifa kwa timu za Tanzania, imekuwa na msimu mbaya, huku Azam FC iliyofuzu kwa mara ya kwanza hatua hii, imefanya vizuri zaidi.

PUMZ 02

AZAM FC

Imekuwa ikijaribu kwa misimu 12 kufika hatua hii, tangu iliposhiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2013.

Wakati ule ilitolewa na AS Far Rabat ya Morocco katika raundi ya pili, huku John Bocco akipoteza penalti ya dakika ya mwisho ya mchezo.

Endapo Azam FC ingepata penati ile, ingevuka na kufuzu raundi ya mchujo (play off) kukutana na timu zilizotolewa kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya hapo imekuwa na misimu ya kuumiza hadi safari hii ilipofanikiwa.

Imemaliza na pointi tisa na kuwa vinara kwa timu za Tanzania, japo katika kundi alilokuwapo la Kombe la Shirikisho imemaliza ya tatu.

Pointi hizo tisa zingeweza kuifanya ivuke kama kundi lao lisingekuwa na ushindani kama kiasi hiki.

Kwa mfano Kundi C la Singida Black Stars, Otoho d 'Oyo ya Congo Brazzaville imefuzu ikiwa na alama 9 tu.

Hata Simba SC katika ule msimu wa 2018/19, ilifuzu robo fainali kwa pointi tisa kama hizi.

Lakini kwa Azam FC imekuwa tofauti...ndio mpira.

Katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) iliyopita, Tanzania ilifuzu 16 Bora kwa pointi mbili tu, ilhali kuna timu katika makundi mengine zilikuwa na alama nyingi zaidi ya hizo na hazikufuzu...mpira ni mchezo wa sheria, kanuni na taratibu.

PUM 04

YANGA

Kwa msimu wa pili mfululizo Yanga inaishia hatua ya makundi.

Baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho 2023 na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa 2024, ilitarajiwa ingepiga hatua kubwa zaidi na kuandika historia.

Lakini msimu uliofuata ikakwamia makundi na sasa imekuwa tabia kwao.

Hadi inakwenda katika mechi ya mwisho ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, timu hiyo ilikuwa imefunga mabao mawili tu.

Hili ni anguko kubwa sana kwa Wananchi na wanatakiwa kujiuliza wanakwama wapi...ili warejee kwa kishindo msimu ujao.

PUM 01

SIMBA

Wababe wa mechi za kimataifa walio katika anguko kubwa.

Kutoka fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita hadi kuishia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa.

Simba ambayo ndio ilifungua njia kwa timu za Tanzania kimataifa, imekuwa na msimu mbaya zaidi katika historia yake.

Ilipofuzu kwa mara ya kwanza hatua hii mwaka 2003 ilimaliza na pointi saba.

Na ilipambania nafasi hadi siku ya mwisho pale Abidjan dhidi ya Assec Mimosas.

Lakini safari hii imeishiwa pawa baada ya mechi tatu tu za kwanza za Kundi D.

Hili ni anguko kubwa kwao na hawapaswi kuona ni sawa.

Inatakiwa kukaa na kujiuliza imekwama wapi ili warekebishe.

PUM 03

SINGIDA BLACK STARS

Timu mpya iliyokusanya kikosi chenye uzoefu na kufanya maajabu.

Katika msimu wake wa kwanza kimataifa imefika hatua ya makundi...maajabu!

Lakini, hata hivyo ni kama ilijipiga risasi yenyewe.

Ikiwa katika mashindano makubwa kama hayo, ilimtoa kocha wake, Miguel Gamondi.

Kama hiyo haitoshi, ikawatoa nyota wao muhimu kana kwamba ilishapata mafanikio iliyoyataka.

Hii sio sawa sawa kwa timu inayotaka kushindana sawasawa.

Hata hivyo, kila timu ina malengo yake na yawezekana kwao ilishafikia malengo yao baada ya kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mwisho wa siku kuna bomu Tanzania inaandaa na litakuja kuifyatukia Afrika misimu michache ijayo.