Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Una ushuzi? Ajira hii hapa changamka!

USHUZI Pict

Muktasari:

  • Wazazi wengi wamekuwa wakifundisha watoto kutofanya jambo hilo mbele za wakubwa au watu waliowazidi umri au hata sehemu za watu wengi.

NEVADA, MAREKANI: KATIKA jamii nyingi hapa nchini na Afrika kwa ujumla suala la kushuta (kujamba) hadharani tena mbele ya waliokuzidi umri, huonekana kama ni kitendo cha kukosa heshima.

Wazazi wengi wamekuwa wakifundisha watoto kutofanya jambo hilo mbele za wakubwa au watu waliowazidi umri au hata sehemu za watu wengi.

Hata hivyo, hiyo ni tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani ambako kitendo hicho cha kutoa ‘upepo’ huwa ni sehemu ya ucheshi, ukakamavu na ajira kiasi cha kuundwa kwa shindano maalum la watu kuchuana na washindi kuzoa zawadi mbalimbali ikiwemo Dola 25,000 (takriban Sh61 milioni).

Leo tunakusogezea mchezo huu mezani kuanzia asilia na kila kitu unachouhusu.

USHU 08

ASILI YAKE

Kwa mara ya kwanza mchezo huu ulichezwa huko Ulaya karne ya 8-11 moja katika nchi za Skandinavia.

Watu wa nchi hizo walikuwa na tamaduni nyingi za kujifurahisha na miongoni mwao ilikuwa ni kushindana kuachia ushuzi.

Katika  nyakati tofauti wanajeshi walikuwa wakishinda kujamba kama sehemu ya kuonyesha ukomavu wao.

Pia katika karne ya tano, huko Ugiriki mchezo huu ulikuwa ukitumika kama sehemu ya maonyesho  ya vichekesho.

Kule Japan kuanzia miaka ya 1603 hadi 1868 kujamba ulikuwa ni mchezo rasmi na kuna hadi michoro iliyochorwa kuonyesha mchezo huo.

Katika nchi zote hizi mchezo huu kwanza ulitumika kama sanaa ya maigizo ya kuchekesha na wakati mwingine ulitumia kama sehemu ya kuonyesha ukakamavu.

Baada ya kuanzishwa kwa miaka, mchezo huu uliachwa miaka ya katikati  kabla ya kuanza tena kuchezwa kuanzia 1990 hadi sasa na nchi zinazocheza sana kwa sasa na zina mashi-ndano kila mwaka ni Marekani, Canada, Japan, Ujerumani na India.

USHU 07

MASHINDANO YA DUNIA

Mashi-ndano hayo yanayoitwa World Farting Championship kwa mara ya kwanza yalianzishwa huko Reno, Nevada, Marekani 2008.

Katika mashindano hata kuna aina tatu za vipengele. Cha kwanza ni wale washiriki wanachuana kuachia kijambo kwa muda mrefu. Pia kuna washindani wanajamba kwa ubunifu, mfano ni kujamba kwa mdundo au mtindo maalum wa kuvutia.

Mwisho ni wale wajambaji ambao wanajamba kwa pozi, yaani kidogo kidogo lakini mara nyingi.

USHU 06

KANUNI ZA MASHINDANO

Mashindano hutumia vifaa maalumu kama, Decibel meter ambacho hupima sauti, Gas sensor, ili kupima uzito wa hewa/gesi pamoja na saa ili kujua muda ambao mjambaji ameutumia.

Mshiriki haruhusiwi kutumia gesi ya bandia kama helium au nitrous oxide ili kumsaidia kujamba, anatakiwa awe na afya njema na asiwe na tumbo kubwa sana na kabla ya shindano kuanza hufanyiwa vipimo ili kutazama utimamu wao.

Mshiriki pia atatakiwa ajambe kiasili kusiwe na kitu chochote cha kumsaidia.

Majaji huwa wanachagua mshindi kwa vigezo tofauti tofauti kwa kutegemea na mashindano husika na aina ya vipengele.

Katika mashindano karibia yote, vipengele vinavyoshindaniwa ni pamoja mjambaji aliyejamba kwa sauti kubwa zaidi.

Mjambaji aliyetumia muda mwingi kujamba kwa mjambo mmoja. Kujamba Mfululizo na kujamba kwa ubunifu.

USHU 05

VIWANGO VYA MASHINDANO

Mashindano mengi yanaongozwa na viwango vya aina tatu, kuna Amateur (Mashindano ya Kawaida) ambayo hayahitaji maandalizi makubwa. Semi-Pro Level (Washiriki wazoefu), hapa huwa ni mashindano rasmi ambayo yanakuwa na zawadi na pengine mashabiki wengi na washiriki pia hupata lishe maalum kabla ya mashindano.

Mwisho niu Professional ambayo huwa ni mashindano ya ngazi ya dunia yanayohusisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani.

USHU 04

NCHI ZINAZOFANYIKA ZAIDI

Mashindano haya hupata umaarufu zaidi katika nchi zifuatazo:

Marekani -Reno, Las Vegas, Texas

Canada - Ontario na Toronto

Japan - Tokyo (Katika sherehe za He-Gassen Festival)

Ujerumani - Cologne, Munich

England - London Comedy Festivals

USHU 03

MABINGWA WA MUDA WOTE

Kama ilivyo soka na michezo mingine, hata huku pia kuna mabingwa wa muda wote ambao wanashikilia rekodi mbalimbali ambazo hadi leo hazijavunjwa.

Paul Oldfield au ‘Mr. Methane’, raia wa England ni miongoni mwa washiriki wa mwanzo kabia kuanzia miaka 90 na ameshinda mara kadhaa katika mashindano ya Marekani na Ulaya.

Roland “Thunderpants” raia huyo wa Marekani anashikilia rekodi ya kujamba mara 93 aliyoiweka katika mashindano 2011 ya  Reno Championships yaliyofanyika hukohuko Marekani.

Kenji ‘He-Gassen King’ ni mwamba mwingine katika mchezo huo anayetokea Japan na ndiye mshiriki pekee aliyeshinda tamasha la He-Gassen mara tatu kati ya 2014 hadi 2016.

Naye Bruno Kraft kutoka Ujerumani anashika rekodi ya kujamba mara moja kwa sekunde 57 aliyoiweka 2019.

USHU 02

ZAWADI ZINAZOTOLEWA

Mara nyingi huwa kuna zawadi za fedha kuanzia dola 500 hadi 10,000 lakini kwa mashindano makubwa ya dunia huweza kufikia Dola 25,000. Mashindano yale ya Marekani na Ulaya huwa kuna mataji na medali maalumu.

Baadhi ya washindi pia hujikuta wakipata madili yakwenda kujinga na vikundi vya uchekeshaji na baadhi huingia katika rekodi za vitabu vya Guiness.


SHERIA ZA USIMAMIZI NA NANI ANAYASIMAMIA

Sehemu nyingi ambazo zinadaa mashi-ndano ya mchez huu hazina uachanachama wa aina yoyote ingawa kuna chombo maalum kinachosimamia mchezo huu kiitwacho World Farting Championship Committee (WFCC) kilichoanzishwa huko Marekani mwaka 2012 ambacho ndio huwa kinaanda mashindano maalum ya kimataifa yanayofanyika huko  Reno na Las Vegas, Marekani.

Kwa yale mashi-ndano ya Ulaya yanasimamia na European Flatulence Arts Association (EFAA) na upande wa Japan kuna He-Gassen Cultural Federation (Japan)

USHU 01

VIGEZO VYA KUWA MSHIRIKI

Kwanza mshiriki anatakiwa kuwa na afya njema, asiwe na matatizo ya tumbo, awe na umri wa miaka 18 na kuendelea lakini baadhi ya mashindano huruhusu washiriki wenye umri wa miaka 16 na kuendelea.

Washiriki hutumia vyakula kama  Maharagwe, Kabichi na  Mayai kama sehemu ya maandalizi. Mshiriki pia anatakiwa kuwa na uwezo wa kujidhibiti, kuweza kujamba na kujizuia kwa wakati.


INDIA NAKO HAWAPOI

India ni miongoni mwa nchi ambazo zimeanzisha  mashindano haya katika miaka ya hivi karibuni na yalipata umaarufu mkubwa sana katika mitandao ya kijamii.

Mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 2019 yaliitwa Surat Fart Championship.

Mashindano haya yalihudhuriwa na mamia ya watazamaji na baada ya hapo ikaelezwa kwamba ilipangwa kuanzishwa kwa ligi ya taifa ya ujambaji, lakini mpango huo haukufanikiwa kutokana na ukosefu wa wadhamini. Kampuni nyingi zilionekana kutovutiwa na mchezo huo.

Katika mashindano hayo ya mwaka 2019, Nitin Sharma aliibuka mshindi wa kujamba kwa muda mrefu akitumia sekunde 25.

Raju Pardeshi akashinda kipengele cha kujamba kwa ubunifu na Ashok Thakur ambaye alipata umaarufu sana, yeye alishinda kwa kujamba kwa sauti sana.


FAIDA ZA KUJAMBA

Kuna faida lukuki za kujamba na hapa tumekuletea faida hizo kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kwanza kabisa kupitia jarida la Gut Journal lililochapishwa mwaka 2013, kitendo hicho husaidia kupunguza maumivu ya tumbo. Kawaida gesi inapoongezeka tumboni inajenga shinikizo (pressure) ambalo husababisha maumivu makali.

Utafiti uliofanywa na  Gut Microbes Research mwaka 2013, unaeleza kwamba kitendo cha mtu kujamba ni ishara ya kwamba ana Afya ya Utumbo. Katika utafiti huo imeelezwa kwamba kuwa na gesi ni ishara kwamba bakteria wazuri (probiotics) wanafanya kazi kwenye utumbo. Bakteria hao huchakata nyuzinyuzi na vyakula vigumu kuvunjwa, na kusababisha kutengenzwa kwa gesi, hivyo kama mtu hajisikii hali ya kujamba kabisa ni ishara kwamba ana upungufu wa bakteria hao, umeng’enyaji wake wa chakula ni dhaifu au ana ulaji mdogo wa vyakula vyenye nyuzinyuzi.

Mbali ya yote, kujamba ni sehemu ya kuondoa sumu ndogondogo. Kwa mujibu wa hospitali ya Mayo Clinic katika chapisho lao la mwaka  2018, wakati chakula kinavunjwa na bakteria kwenye utumbo, hutengeneza gesi kama hydrogen, methane na sulphur compounds, ikiwa gesi hizo zitaendelea kusalia kwenye utumbo inaweza kusababisha maumivu, uchovu na  msongamano wa chakula, hivyo ukijamba huwa

Mtu anayejamba huwa anasaidia mwili wake kuchochea mzunguko wa umeng’enyaji. Peristalsis ni mchakato wa misuli ya utumbo kusukuma chakula na taka kuelekea sehemu ya mwisho.

Gesi husaidia kusukuma hewa na mabaki ya chakula, na inapotoka nje ni ishara kuwa mchakato wa  peristalsis upo vizuri,Katika mahojiano yake ya mwaka 2020, Dr Satish Rao kutoka American Gastroenterological Association anasema kitaalamu kujamba hupunguza msongo wa mawazo.

Tumbo linapokuwa na gesi nyingi, ubongo hupokea ishara za kitu fulani hakipo sawa katika tumbo la mtu husika, hivyo mtu huyo anapojamba hupunguza shinikizo hilo, na ubongo hupokea ishara za utulivu.