Ubora wa siku 100 za Didier Gomes Simba

Sunday May 02 2021
New Content Item (2)
By Mwandishi Wetu

NIANZE kwa kusema msimu wa 2020/2021 katika soka la Tanzania una matukio mengi na ratiba mbalimbali. Katika ratiba na matukio hayo tumeshuhudia katika ngazi za kimataifa ambapo klabu za Tanzania tumeshuhudia kusambaa kwa majukumu. Ziko timu zinacheza ligi na mashindano ya ndani, lakini ziko ambazo kwa utaratibu wa kimpira zinacheza mashindano ya kimataifa.

Timu zinazoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ziko mbili. Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Namungo ipo katika Kombe la Shirikisho Afrika na zote zimetinga hatua ya makundi. Bahati nzuri uwepo wa hizo timu umetupa faida kubwa ya kuingiza timu nne. Bahati mbaya Namungo kaishia hapo alipoishia, lakini Simba ikiwa imesogea juu sana pengine kinyume na tulivyotarajia kufika robo fainali.

Tumeshuhudia klabu ya Simba inakwenda kucheza kwenye robo fainali baada ya kutoka hatua ya makundi ikiwa inaongoza. Mafanikio haya hayakuja kwa bahati mbaya yapo mengi nyuma ndani na nje ya kiwanja. Ndani ya uwanja, Simba wamekuwa na walimu kadhaa. Hivi karibuni walikuwa na kocha Patrick Aussems, kisha akaja mwalimu Sven Vandenbroeck na ghafla aliondoka hivyo ilikuwa lazima maisha yaendelee na kwenye management (usimamizi) kuna kinaitwa human resource (rasilimali watu). Wakafanya replacement (mbadala) wakampata mwalimu Didier Gomes Da Rosa kutoka Al Merrikh ya Sudan.

Nimekuwa nasema kuwa kufundisha mpira ni fani. Ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine. Mwalimu Da Rosa kama wengine wote ana weledi unamuongoza kwa kuzingatia principles of coaching, philosophy (kanuni za kufundisha, falsafa) na professionalism (weledi).

Ziko tabia ambazo kocha wa mpira anatakiwa awe nazo ambazo Kocha Gomes ameonekana anazo. Kwanza ni karama ya kufundisha mpira. Karama kwenye coaching ni mwalimu kuonyesha ile passion (shauku) na wachezaji wakatambua kwamba mwalimu anaupenda huo mchezo wenyewe kuwafanya wafuate kile anachokitaka. Pili lazima aonyeshe anaufurahia mchezo wenyewe. Aonyeshe kwamba anawajibika kwa mchezo wenyewe. Wachezaji watawajibbika kwa sababu wanaona na wewe kocha unawajibika

Jambo la tatu ni humor. Ni mwalimu kuonyesha kwamba anaupenda ule mchezo kuanzia kwenye maandalizi hadi kwenye mechi. Asichoke kwa sababu ya kukumbana na changamoto. Huenda kuna changamoto ndani ya Simba lakini Gomes hazifanyi kuwa tatizo japo ni mgeni

Advertisement

Mwalimu huyu nadhani amekwenda mbali zaidi lakini akajiridhisha kwenye baadhi ya mambo kama kujenga umoja wa timu. Kujenga team work sio jambo rahisi. Amekuta mambo yanakwenda sawa na akaweza kumaintain. Nguzo kuu za team work ziko tatu ambazo mojawapo ni mawasiliano.

Ndani ya Simba kuna mawasiliano thabiti kati ya wachezaji, makocha, management na benchi la ufundi. Gomes amehakikisha hilo linatengemaa. Kocha huyo pia amejenga ari na moyo wa ushindi. Wachezaji wajione wako pale kwa ajili ya kufanya kazi. Mwalimu anafundisha mbinu, akili na maarifa, lakini lazima atengeneze winning attitude kwa wachezaji.Kingine ni kutengeneza motivation na pia kujenga team ego. Kuiona timu kwanza, mimi baadaye. Kama timu huitangulizi ndio wakati mwingine unajikuta ari, moyo, nguvu na nidhamu ya kupigania timu inakuwa iko chini.

Kubwa lingine ambalo analisimamia ni nidhamu. Kabla mwalimu hajafika kuna mchezaji alifungiwa kwa sababu ya nidhamu. Lakini kwa sasa tatizo la utovu wa nidhamu linaonekana kupungua. Kama hauna nidhamu, malengo hayawezi kufikiwa. Mchezaji anatakiwa anachokifanya kionekane ni kioo. kiwe reflection ya timu.

Mbali na yote, anaonekana kustudy vizuri malengo ya Simba, akaingiza vitu vingi ambavyo vinaonekana kuwasaidia. Kuna kitu kwenye coaching kinaitwa GROW. Heruf G inawakilisha goals au malengo, R inawakilisha realiaty, O inamaanisha Options na W ni will ya kusaidia klabu itimize kile ilichokipanga.

Juu ya yote haya, mwalimu amekuta kuna utulivu ndani ya timu. Kuanzia kwenye uongozi, Simba inajiendesha kisasa. amekuta wachezaji wako pamoja bahati nzuri usajili ulifanyika vizuri. Anachokifanya kimetokana na yale mengi mazuri aliyowakuta pale kutokana na watu kukaa pamoja.

Pia rotation (mzunguko) anayoifanya imekuwa na matokeo chanya na ni kocha ambaye anaonekana ana mbinumbinu nyingi lakini pia ni mwalimu mwenye mamlaka na haridhiki na uzembe usiokuwa na sababu. Mwalimu Da Rosa hapo alipofikia kwa namna timu inavyocheza anaonekana anaweza kufika hata fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia itategemea namna walivyojipanga.

Advertisement