Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UBISHI WA MZEE WA KALIUWA: Diamond anavyopita njia ya Ronaldo

Muktasari:

  • Nchi haijengwi na wanasiasa tu. Kila mtu ana tofali lake anachangia kwenye kuijenga nchi. Shule zote hapa nchini zimejaa majina ya viongozi wetu wakubwa. Ukienda hospitali hadi wodi zimepewa majina ya viongozi wa kisiasa na siyo madaktari wenyewe.

TANZANIA ndiyo nchi pekee ambayo watu wanaoheshimiwa sana na kuenziwa ni wanasiasa tu. Hakuna wanamichezo. Hakuna wasanii, hakuna wataalamu wanaopewa heshima na nchi. Madaraja yote yamejaa majina ya wanasiasa. Barabara zote zimepewa majina ya wanasiasa. Viwanja vya ndege vyote ni majina yao.

Nchi haijengwi na wanasiasa tu. Kila mtu ana tofali lake anachangia kwenye kuijenga nchi. Shule zote hapa nchini zimejaa majina ya viongozi wetu wakubwa. Ukienda hospitali hadi wodi zimepewa majina ya viongozi wa kisiasa na siyo madaktari wenyewe.

Kila kitu ni siasa nchini. Pale nchini Ureno wamekuja na jambo kubwa na zuri. Ni heshima wanayompatia mchezaji wao mwenye mafanikio makubwa kwenye soka kwa taifa hilo, Cristiano Ronaldo.

Baada ya kuupa jina lake uwanja wa ndege wa Madeira, sasa wamekuja kwenye sarafu. Madeira airport ni uwanja wa nne kwa ukubwa na ufanyaji kazi nchini Ureno. Kwa kazi kubwa aliyofanya Cristiano kwenye soka uwanja umebadilishwa jina na sasa unaitwa Cristiano Ronaldo Airport.

Huwezi kukuta kitu kama hicho Tanzania. Majina yote ya shule, barabara, vituo vya mabasi na treni vyote vimejaa majina ya wanasiasa. Utadhani wanasiasa wanafanya kila kitu kwenye nchini.

Wenzetu wametoka huko. Wanaheshimu na kuthamini mchango wa kila nyanja. Wanaheshimu na kukumbuka watu wa kada mbalimbali. Taifa la Ureno siku siyo nyingi watazindua rasmi sarafu yenye picha na jina la Cristiano Ronaldo kama sehemu ya kuenzi na kutambua mchango wa gwiji huyo wa soka duniani.

Hii ndiyo tofauti kubwa kati ya sisi na wao. Mchezaji huyo maarufu na mwenye mafanikio makubwa katika historia ya taifa hilo ametengenezewa safaru yenye thamani ya Euro 7. Utakumbuka amekuwa akitumia sana chaps ya namba 7 kwenye kila kitu chake akiambatanisha na vifupisho vya jina lake “CR7”. 

DIA5
DIA5

Kwenye njia hiyohiyo sarafu ya Cristiano itatoka hivi karibuni. Pale Ureno kuna wanasiasa wengi sana maarufu, lakini kwenye hili wameamua kwenda na Cristiano Ronaldo. Nchi haiwezi kuheshimu na kuenzi wanasiasa tu. Ni vyema kuheshimu na watu wa kada mbalimbali.

Ni kweli kupitia siasa ndiyo tunapata viongozi wa kitaifa, lakini nchi haiendelei kwa nguvu za wanasiasa tu. Tunahitaji kujifunza na kuanza kuangalia pia kada nyingine.

Wako Watu wengi sana wanafanya makubwa nchini, lakini hawaenziwi. Hawatambuliki. Hakuna anayejali. Inasikitisha sana. Kwa nchini masikini kama Tanzania siyo rahisi kutengeneza sarafu, lakini kuna maeneo mengi ya kuenzi watu.

Tuna mbuga za wanyama na hifadhi. Tuna barabara, madaraja, shule, vyuo vikuu, viwanja vya ndege na kadhalika. Tanzania siyo nchi ya wanasiasa tu. Watu kama Said Salim Bakhresa siyo wanasiasa, lakini wote tunajua makubwa anayofanya.

DIA4
DIA4

Huyu ni mmoja wa wafanyabiashara na matajiri wakubwa wa nchini, kuenziwa ni jambo jema sana. Analipa kodi nchini na kutoa ajira kwa maelfu ya Watanzania. Ni vigumu sana kupitisha siku bila kutumia bidhaa yake. Ni mtu wa kukumbukwa.

Tanzania tuna watu wengi wamefanya makubwa kwenye nyanja mbalimbali. Kwenye Bongofleva kuna mtu kama Diamond Platinumz. Ni mmoja kati ya vijana waliotoka kwenye maisha ya chini na kwa sasa ni tajiri. Ni aina ya watu ambao wanapaswa kuenziwa.

DIA2 (1)
DIA2 (1)

Kwa ukubwa na umaarufu wake angeweza hata kuchongewa sanamu, lakini sisi ni wanasiasa tu. Kuna mtu kama Hasheem Thabit ni Mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza Ligi Kuu ya Kikapu  Marekani maarufu kama NBA. Siyo jambo dogo. Ni mtu anayepaswa kuenziwa. Ni mtu anayepaswa kukumbukwa na nchi. Nchi haijengwi na wanasiasa tu.

Ni zaidi ya miaka 12 tangu afariki dunia, lakini kiwanda cha BongoMovie hakijawahi kumsahau Steven Kanumba. Huyu mtu hakuwa wa kawaida. Alikuwa nembo ya nchi. Tunaweza hata kuupa jina la uwanja hata mmoja wa ndege hapa nchini. Wenzetu wanajaribu kuheshimu watu wao na makubwa waliyofanya bila kuangalia ni kada ipi.

Sisi hapa nchini wa kuenziwa ni wanasiasa tu. Hakuna nchi duniani inayojengwa na siasa pekee. Kuna sanaa, michezo, burudani na maeneo mengine. Hakuna ubaya wowote kwenye kutambua mchango wa kada nyingine kujiletea maendeleo kama Taifa.

Diamond Platinumz ni Cristiano Ronaldo wetu. Wakati mwingine siyo mpaka mtu afe ndiyo akumbukwe. Kama kuna nafasi ya kuheshimu mchango wa mtu akiwa hai tufanye hivyo.

DIA2
DIA2

Ureno na mataifa mengine yanaheshimisha sana watu wao. Sarafu yenye jina na picha ya Cristiano Ronaldo kuanza kutumika hivi karibuni. Ni heshima kubwa sana kwa Cristiano Ronaldo. Ni Heshima kubwa kwa mchezo wa soka.

Tumekuwa na watu kama Suleiman Nyambui, Filbert Bayi, Juma Ikangaa ni majina maarufu kwenye historia ya mchezo wa riadha nchini. Yanastahili kuenziwa. Hawa watu walikuwa wa kwanza kabisa kuitangaza nchi kupitia riadha. Nchi hii siyo mali ya wanasiasa tu, ni vyema kuenzi na kutambua mchango wao.

Kwa upande wa urembo na ulimwende kuna mtu anaitwa Flaviana Matata. Huyu binti wa Kitanzania amekuwa balozi mzuri kwenye majukwaa ya kimataifa na anastahili pongezi. Ni muda wa kutambua mchango wao kwa Taifa. Kila nyaja tukikaa chini tutapata wawakilishi wanaostahili.

Kwa miaka 20 ya hivi karibuni pengine Tanzania hutawahi kuzalisha mrembo mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii kama Wema Sepetu. Ni kweli maisha yake binafsi yamekwenda kwa jamii, lakini haiondoi ukweli kuwa amekuwa Miss Tanzania mwenye kupendwa sana na watu na mwenye ushawishi zaidi nchini.

DIA1
DIA1

Hawa watu siyo wa kuwachukulia poa. Kuna namna kama nchi tunapaswa kuwaenzi. Kuna makubwa wamelifanyia Taifa letu. Kwa vijana wanaopenda muziki wa rap bila shaka yoyote Profesa Jay ni nembo ya mtaa. Siyo lazima kila kitu kiitwe kwa jina la mwanasiasa. Profesa Jay anapaswa kuheshimiwa. Kuna thamani kubwa sana aliiongeza kwenye muziki wetu wa rap.

Ureno kumpa heshima Cristiano iwe na la kujifunza kwa Taifa letu. Siyo lazima na sisi kutoa sarafu yenye picha na jina la mtu mwenye mchango mkubwa kwa Taifa, lakini tuna barabara, shule, hospaitali siyo lazima kila siku zipewe majina ya wanasiasa tu.

Watu kama Ruge Mutahaba wana mchango mkubwa kwenye kiwanda cha burudani nchini. Kuna namna wanasiasa 'wamejipakulia sana minyama'. Nadhani ni muda wa kubadili uelekeo, Cristiano na Diamond wote ni sawa kila mtu kwa nchi yake.