Timu zenye ukakasi kubakia VPL

Muktasari:

LIGI Kuu Bara ipo katika mzunguko wa pili. Kuna timu zimefanya hesabu vizuri, huku nyingine zikisubiri kubahatisha hiyo ikiwa na maana ya kujiandaa kuvuna ulichokipanda.

LIGI Kuu Bara ipo katika mzunguko wa pili. Kuna timu zimefanya hesabu vizuri, huku nyingine zikisubiri kubahatisha hiyo ikiwa na maana ya kujiandaa kuvuna ulichokipanda.

Mzunguko wa pili unakuwa wa kukamilisha hesabu. Zipo zile zinazowania ubingwa, kumaliza nafasi za juu na kujikwamua kushuka daraja ili kuzipisha zile zinazoshindana Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kupanda Ligi Kuu.

Mwanaspoti linakuorodheshea timu zenye walakini wa kubaki Ligi Kuu msimu ujao kutokana na mwenendo wa matokeo ya mechi tangu ligi hiyo ianze 2020/2021.

MWADUI FC

Katika mechi 18 ilizocheza Mwadui FC msimu wa 2020/2021 imekula vichapo michezo 10, imeshinda minne na imetoka sare tatu. Kwa matokeo hayo imejikokotea pointi 15 zilizoifanya ikae nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi.

Ukiachana na vichapo hivyo, bado imeendelea kuwa na hali mbaya hata katika safu zao kwani eneo la ulinzi limeruhusu mabao 34, huku washambuliaji wao wakifunga 13 pekee.

Mzunguko wa pili utakuwa mgumu zaidi kwa Mwadui FC kwa sababu itacheza mechi na timu ambazo zinawania ubingwa kama Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44 katika michezo 18 iliyocheza, imeshinda 13 na sare tano ilhali Simba imecheza mechi 15, imeshinda 11, sare mbili na kupoteza mbili, hivyo ina pointi 35 katika ligi hiyo.

Ukiachana na Simba na Yanga, ipo Namungo FC na Azam FC ambazo pia zipo kwenye ushindani wa hali ya juu kwenye ligi, hivyo ikipona na kubaki ifanye kazi ya ziada.

IHEFU SC

Tangu Ihefu SC ipande Ligi Kuu, mechi ya mwisho ikiishusha Mbao FC kwenye Ligi Daraja la Kwanza. Haikuwa na matokeo mazuri ikiwa chini ya kocha Maka Mwalwisi na mpaka alipopokea mikoba Zuberi Katwila.

Timu zenye ukakasi kubakia VPL

Imecheza mechi 18, imeshinda tatu, imetoka sare nne na kufungwa 11. Hesabu zake zikipigwa zinapatikana pointi 13 walizovuna kupitia michezo waliyocheza.

MBEYA CITY

Msimu uliopita wa Ligi Kuu Mbeya City iliponea chupuchupu kushuka daraja na kulazimika kusubiri kucheza mchujo na Geita Gold ili kujihakikishia kuendelea kucheza ligi hiyo ya msimu huu, ambapo matokeo yao yamekuwa tiamaji tiamaji. Inatia wasiwasi mzunguko wa pili kama inaweza kutoboa kwani mpaka sasa imecheza mechi 18, imeshinda mbili, sare nane, imefungwa nane na kuvuna pointi 14.

Wakati huohuo raundi ya pili itakuwa na changamoto ya ushindani mkubwa hasa kwa timu ambazo zinasaka ubingwa na e zinazohitaji kumaliza juu.

JKT TANZANIA

Ni umakini wa kuchanga karata zao katika mechi zilizosalia utakaowafanya wabaki msimu ujao. Mwenendo wa matokeo yao hauridhishi kujiweka katika mazingira mazuri. Katika mechi 18 ilizocheza imeshinda tano, sare tano na imefungwa nane, hivyo imejikusanyia pointi 20