Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takwimu za pasi zinavyofichua mabadiliko EPL miaka 10

PASI Pict

Muktasari:

  • Arsenal inaongoza msimamo wa ligi, pia wamekuwa miongoni mwa timu zinazokosolewa zaidi kuhusu namna zinavyocheza.

LONDON, ENGLAND: KUMEKUWA na mjadala mkubwa kuhusu namna mchezo wa Ligi Kuu England ulivyo msimu huu, lakini kulinganisha takwimu za pasi kunaonyesha wazi jinsi soka la England limebadilika katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Arsenal inaongoza msimamo wa ligi, pia wamekuwa miongoni mwa timu zinazokosolewa zaidi kuhusu namna zinavyocheza.

Hata hivyo, Arsenal haiko peke yao. Ukiangalia takwimu moja muhimu ya pasi, inaonyesha kuwa ligi nzima imebadilika sana katika muongo uliopita. Takwimu za pasi za msimu huu wa Ligi Kuu England na kuzilinganisha na zile za miaka 10 iliyopita, kinachovutia zaidi si tu ni wachezaji gani wanaopiga pasi nyingi zaidi, bali pia ni nafasi wanazocheza uwanjani.

Katika msimu wa 2015–16, wachezaji wanne kati ya sita waliopiga pasi nyingi zaidi walikuwa viungo wa kati, huku Cesc Fàbregas akiongoza kwa kupiga pasi 2,829. Nyuma yake walifuata viungo wengine watatu wa kati; Andrew Surman (2,287), Mesut Ozil (2,276) na Aaron Ramsey (2,154). Ilibidi kusubiri hadi nafasi ya tano ndipo mchezaji ambaye si kiungo wa kati aonekane kwenye orodha.

PAS 01

Lakini, ukiangalia msimu huu, hali imebadilika kabisa. Nafasi nne za juu zote zinashikiliwa na mabeki wa kati, huku Elliot Anderson akiwa kiungo anayeongoza kwa pasi akiwa nafasi ya tano kwa takribani pasi 1,900.

Miongoni mwa mabeki hao, ni beki wa Liverpool, Virgil van Dijk, anayeshika nafasi ya kwanza kwa kupiga pasi 2,205. Inaweza kuonekana kama bahati tu, lakini takwimu hizi zinaashiria mabadiliko makubwa kuhusu wapi mpira unachezwa zaidi uwanjani na jinsi timu zinavyocheza.

Kwa ufupi, eneo halisi la mchezo limekuwa likibana zaidi kiasi kwamba mabeki wa kati sasa wanacheza katika maeneo ambayo zamani yalikuwa yanatawaliwa na viungo wa kati. Hii inawezekana ni matokeo ya timu nyingi kucheza kwa kujilinda zaidi na kuruhusu presha ya wapinzani.

Takwimu hizi pia zinaonyesha kuwa aina ya kiungo anayesimamia mpira na tempo ya mchezo, aliyekuwa maarufu miaka ya 2010, imepungua sana katika Ligi Kuu England.

Kwa mfano, Fabregas alikuwa akipiga wastani wa pasi 0.98 kwa dakika katika msimu wa 2015–16. Lakini Declan Rice, ambaye ndiye mpiga pasi bora katika timu inayoongoza ligi kwa sasa, anapiga wastani wa pasi 0.69 kwa dakika.

PAS 02

Mtu anaweza kusema Fabregas alikuwa wa kipekee, lakini hata Mesut Ozil (0.74) na Aaron Ramsey (0.82) walikuwa na wastani mkubwa wa pasi kwa dakika kuliko Rice msimu huu.

Kwa upande mwingine, Van Dijk, mpiga pasi anayeongoza ligi ana wastani wa pasi 0.84 kwa dakika. Si pasi pekee zinazoonyesha mabadiliko haya. Mchezaji mwenye miguso mingi zaidi ya mpira katika ligi msimu huu ni Elliot Anderson. Ingawa yeye ni mfano tofauti kwa kuwa ni mchezaji mwenye kipaji katika timu inayopambana na kushuka daraja, wachezaji wanne wanaomfuata wote ni mabeki wa kati.

Ukilinganisha na msimu wa 2015–16, wachezaji wanne wa juu kwa miguso ya mpira wote walikuwa viungo wa kati.

Katika msimu huo, Fabregas aligusa mpira mara 3,395, wastani wa miguso 1.17 kwa dakika. Van Dijk kwa sasa ana wastani wa 0.99 miguso kwa dakika, wakati Rice ana 0.9. Dominik Szoboszlai ana wastani mkubwa kidogo wa 0.94, lakini takwimu zake zimeathiriwa na kucheza mara kwa mara katika nafasi za karibu na safu ya ulinzi.