Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stand United na kina United wengine

STAND Pict

Muktasari:

  • Umekuwa ni utamaduni sasa kwa timu za Tanzania kuwa na tukio la namna hii linalowaunganisha mashabiki na wadau wengine katika kuifurahia klabu yao, likiasisiwa na Simba SC miaka 17 iliyopita kabla klabu nyingine zikiwamo Yanga na Azam kuiga.

MFULULIZO wa matamasha ya burudani kwa timu za mpira wa miguu nchini umeendelea juma lililopita kwa klabu ya Stand United ya Shinyanga nayo kufanya shughuli yake.

Umekuwa ni utamaduni sasa kwa timu za Tanzania kuwa na tukio la namna hii linalowaunganisha mashabiki na wadau wengine katika kuifurahia klabu yao, likiasisiwa na Simba SC miaka 17 iliyopita kabla klabu nyingine zikiwamo Yanga na Azam kuiga.

Siku ya Stand United imeitwa Wana Day, yaani Siku ya Wana kwa sababu klabu hiyo jina lake la utani ni Chama la Wana.

Hivyo Wana walikuwa na shughuli yao ambayo ilifana sana kwenye Uwanja wa Kambarage, mjini Shinyanga na Wana kuleta matumaini kwamba siku zijazo huenda mambo yakawa bora zaidi ya hapa.

Wakati shughuli ikifana, kupitia ukurasa huu, tunajaribu kuliweka juu kidogo jina la Stand United katika mahali linapostahili kuwepo jina la miamba hawa wa Shinyanga, ‘Igembe Nsabo’.

STAN 01

NI UNITED

Hii ni timu inayotokea Shinyanga mjini katika kituo kikuu cha zamani cha mabasi ya mikoani.

Wapiga debe na wafanyabiashara wengine wa sokoni pale wakaungana na kuanzisha timu waliyoiita Stand United yaani Muungano wa Stendi.

Muungano katika mpira sio jambo geni hapa nchini, lakini hapo kabla hakukuwa na utamaduni wa kutumia jina la United kuuenzi Muungano huo hadi miaka ya 1990 pale Watanzania walipoanza kufuatilia mpira wa nje.

STAN 05

Zikazuka timu kama Moro United, Singida United na hatimaye ndio hawa Stand United.

Muungano unaozungumziwa hapo unaweza ukawa wa timu zaidi ya moja au watu wa aina tofauti wanapokuja pamoja.

Kupitia Stand United, pumzi ya moto inakufungua kifikra kwa kukupa asili ya klabu nyingine duniani zinazotumia jina la UNITED.

STAN 02

KINA UNITED WENGINE

Kila nchi huwa na utamaduni wa majina ya mazoea yatakayoambatana na majina rasmi kwa klabu zake na kila watu wana historia yao inayobeba maana halisi ya maneno yanayotumika.

Kwa mfano, asilimia kubwa ya klabu za Hispania hutumia neno la REAL; kama Real Madrid, Real Betis, Real Sociedad nk.

Uturuki hutumia neno Spor; kama Alanyaspor, Antalyaspor, Trabzonspor, Kayserispor, Bursaspor nk.

Kwa hawa kina United, asili yao ni England ambako utakutana na Manchester United, Newcastle United, Leeds United, West Ham United na hadi Ligi za chini kabisa katika timu kama Thame United, Wrexham United nk.

STAN 03

Timu ya kwanza kutumia jina la United ni Newcastle pale timu mbili kutoka mji wa Newcastle, Newcastle East End (ambayo mwanzo kabisa iliitwa Stanley FC) ilipoungana, kwanza na Rosewood FC, halafu ikachukua baadhi ya watu kutoka timu iliyokufa ya Newcastle West End na kuzaliwa Newcastle United mwaka 1892.

Baada ya hapo, zikazaliwa United nyingine nyingi.

Juu kabisa, nilizungumzia kuhusu UNITED kutokana pia na Muungano wa watu wa aina tofauti, zaidi ya kuungana timu.

England kama moja ya mataifa makubwa na yenye uchumi bora duniani, huvutia watu kutoka kila pande ya dunia.

Watu hawa ndio wakati mwingine huweka kando tofauti zao na kuungana kuunda timu moja.

Hapa ndipo utaipata klabu kama West Ham United ambapo wafanyakazi wa kiwanda cha chuma cha Thames Iron Works waliokuwa na asili ya nchi mbalimbali duniani, walipoamua kuunda timu yao mwaka 1900, timu hiyo ikiwa na miaka 5, wakaamua kuiita West Ham United.

STAN 04

Hawa wanaoitwa Mashetani Wekundu, Manchester United, hapo kabla walikuwa wakiitwa Newton Heath na mwaka 1902 ndipo wakajibadilisha na kujiita Manchester United.

Na hii ni baada ya matajiri wanne, akiwamo mchezaji wao Harry Stafford na mtengeneza bia, John Henry Davies, kuunganisha mitaji yao na kuinunua klabu hiyo iliyokumbwa na ukata kiasi cha kukaribia kufilisika.

Katika wote hao, mkasa wa Leeds United ni wa kipekee. Hawa walianza kama Leeds City mwaka 1904 lakini mwaka 1919 wakakumbwa na kashfa kubwa ya malipo yasiyo halali kwa wachezaji wao.

Hii ilikuwa kashfa kubwa iliyochafua jina lao na katika kujisafisha, wakaamua kuondoa City na kuweka United...hawakuwa na sababu yoyote ya kimuungano.

Hongereni Stand United kwa tamasha lenu...lakini safari ijayo alikeni timu moja ya Uingereza yenye jina la United, Wana wenzenu!