Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi ya kipekee Lamine Yamal Vs Ufaransa

REKODI Pict

Muktasari:

  • Ikiwa kuna timu moja ya taifa inayoufahamu vizuri uwezo wa Lamine Yamal, basi ni Ufaransa. Licha ya kuwa kinda huyo bado ana safari fupi katika kikosi cha taifa cha Hispania, lakini tayari amekuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Ufaransa, akifunga mabao matatu katika mechi mbili rasmi.

TEXAS, MAREKANI: UNAWEZA kusema Lamine Yamal ni kama tayari anajua jinsi ya kung’ara dhidi ya Ufaransa.

Hiyo inatokana na kwamba, winga huyo chipukizi wa Hispania amefunga mabao matatu katika mechi mbili pekee dhidi ya Les Bleus, leo Jumanne saa 4:00 usiku atakuwa na matumaini ya kuendeleza rekodi hiyo ya kuvutia wakati mataifa hayo mawili yatakapokutana katika nusu fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, wakipigania nafasi ya kufuzu fainali.

Ikiwa kuna timu moja ya taifa inayoufahamu vizuri uwezo wa Lamine Yamal, basi ni Ufaransa. Licha ya kuwa kinda huyo bado ana safari fupi katika kikosi cha taifa cha Hispania, lakini tayari amekuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Ufaransa, akifunga mabao matatu katika mechi mbili rasmi.

REKO 01

Mchezaji huyo ambaye jana Julai 13, 2026 alitimiza miaka 19, anaingia kwenye mchezo huo akiwa na morali kubwa baada ya kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika ushindi wa Hispania dhidi ya Ubelgiji kwenye robo fainali.

Ingawa bado hajaonyesha kiwango chake bora kwa mwendelezo katika mashindano haya akifunga bao moja pekee katika mechi sita, rekodi yake dhidi ya Ufaransa inawapa La Roja sababu nyingi za kuamini kuwa anaweza kung’ara tena katika moja ya majukwaa makubwa zaidi ya soka duniani.

Takwimu zinajieleza zenyewe. Kati ya mabao saba ambayo Lamine Yamal ameifungia timu ya taifa ya Hispania, matatu ameyafunga dhidi ya Ufaransa. Hivyo, Les Bleus ndiyo timu ambayo ameifunga mabao mengi zaidi kuliko mpinzani mwingine yeyote.

REKO 02

Onyesho lake la kwanza la kukumbukwa lilikuwa katika nusu fainali ya UEFA Euro 2024, alipofunga bao la kuvutia kwa shuti la mbali na kuisadia Hispania kupata ushindi wa mabao 2-1. Chini ya mwaka mmoja baadaye, aliitesa tena Ufaransa katika UEFA Nations League 2025 kwa kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa kusisimua wa mabao 5-4.

Maonyesho hayo yameongeza kujiamini kwake, huku Lamine Yamal akisisitiza kuwa Hispania haina sababu ya kuiogopa Ufaransa, hasa baada ya kuwaondoa kwenye mashindano makubwa mawili katika miaka ya hivi karibuni.

Mbali na rekodi yake bora dhidi ya Ufaransa, Lamine Yamal ameanza vyema maisha yake katika timu ya taifa ya Hispania. Katika mechi 31 alizoichezea Hispania, ameshuhudia ushindi mara 23, sare saba na kupoteza mchezo mmoja pekee, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi chini ya kocha Luis de la Fuente.

REKO 03

Katika mechi hii ya nusu fainali, Lamine Yamal anakutana na nyota kama Kylian Mbappé na Mike Maignan, ambao tayari wameonja uwezo wake wa kubadili matokeo.

Kwa kuwa nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia ipo mezani, Hispania itategemea tena kipaji cha kijana huyo. Ikiwa Lamine Yamal ataonyesha kiwango kilekile alichokizoea dhidi ya Ufaransa, anaweza tena kuwa mchezaji wa kuamua matokeo na kuipeleka La Roja hatua moja karibu zaidi na kutwaa taji lingine la Kombe la Dunia baada ya timu hiyo kushinda mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.