Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi nyota wa Ligi Kuu walivyoipeleka Tanzania Kombe la Dunia Futsal

Muktasari:

  • Fainali za Mataifa ya Afrika za Futsal ambazo zimetumika kuzipata timu hizo mbili, zilifanyika nchini Morocco kuanzia Aprili 22 hadi 30 ambako wenyeji na Tanzania waliokutana katika mechi ya fainali, ndio watakaoiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia la Futsal la Fifa 2025.

TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Futsal imeweka historia ya aina yake baada ya kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2025, ikiwa ni moja ya mataifa mawili tu, pamoja na Morocco, yatakayoiwakilisha Afrika huko nchini Ufilipino kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 7.

Fainali za Mataifa ya Afrika za Futsal ambazo zimetumika kuzipata timu hizo mbili, zilifanyika nchini Morocco kuanzia Aprili 22 hadi 30 ambako wenyeji na Tanzania waliokutana katika mechi ya fainali, ndio watakaoiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia la Futsal la Fifa 2025.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano ya Futsal kuandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa upande wa wanawake na Tanzania inaandika rekodi ya kwanza kwenye mchezo huo.

Tanzania ilikuwa kati ya timu tisa kutoka Afrika zilizochuana kumpata bingwa na mshindi wa pili atakayewakilisha Kombe la Dunia mwaka huu.

Tanzania ilipangwa kundi C na Madagascar, Senegal huku kundi B likiwa na Angola, Misri na Guinea ilhali Kundi A likiwa na waandaaji wa mashindano hayo Morocco, Cameroon na Namibia.

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Afrika lakini kwa duniani hii ni mara ya pili baada ya kufanyika 2010 nchini Hispania ambako Brazil ilitwaa ubingwa huo.

Katika Bara la Ulaya, UEFA ilizindua mashindano ya kwanza ya Futsal kwa Wanawake (UEFA Women’s Futsal EURO) Februari 2019, yakihusisha timu kutoka mataifa manne, Hispania, Ureno, Urusi na Ukraine.

Tanzania ilistahili kufika fainali ya Afrika kutokana na ubora iliyouonyesha tangu mashindano hayo yanaanza hadi fainali.

Ingawa ni mchezo mgeni kwa Afrika, lakini rekodi za Tanzania kwenye mashindano mbalimbali yaliisaidia kwa kiasi kikubwa kufika hatua hiyo.


NJIA YAO

Tanzania ilikuwa kati ya timu tisa zilizokuwa zinawania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu kama Senegal, Cameroon ambazo zimepiga hatua kubwa kwenye soka.

Timu hiyo ilianza harakati zake ikishinda mechi mbili za makundi, sare ya 4-4 na Madagascar na kuichapa Senegal mabao 3-1 kisha kutinga nusu fainali na kuitoa Cameroon kwa jumla ya mabao 3-2.


REKODI

Tanzania imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu kwa fainali ya mashindano hayo ya kwanza.

Hii ni ishara ya maendeleo makubwa ya mchezo wa Futsal katika ukanda huu ambao mara nyingi umekuwa nyuma kwenye mashindano mbalimbali ya wanawake.

Kitendo cha Tanzania kufika hatua hiyo itafungua macho ya mashirikisho mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki kuwekeza zaidi kwa wanawake kwenye mchezo huo.


KOMBE LA DUNIA

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), timu mbili zilizocheza fainali Afrika zimekata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali za Dunia za Futsal kwa Wanawake zitazofanyika Ufilipino.

Tanzania kwa kucheza fainali, imekuwa moja kati ya timu hizo mbili na hivyo kuwa miongoni mwa mataifa ya kwanza kutoka Afrika kushiriki mashindano ya dunia.

Hii ni historia nyingine iliyowekwa na timu hiyo, ikifuata nyayo za timu ya Tanzania iliyofika fainali mara mbili na kutwaa Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani huko Rio de Janeiro Brazil 2014, pamoja na timu ya taifa ya soka ya wenye ulemavu, Tembo Warriors, ambayo ilifika robo fainali katika Fainali za Kombe la Dunia la soka kwa watu wenye ulemavu 2022 zilizofanyika huko Uturuki.


WALIOIBEBA TANZANIA

Takribani kikosi chote kilichoitwa na kucheza kwenye mashindano ya Futsal hakina utofauti na kile cha Twiga Stars kinachoitwa kwenye mashindano mbalimbali.

Nyota kama Naijat Abbas, Aisha Mnunka, Stumai Abdallah, Donisia Minja na wengineo wamekuwa na mchango mkubwa kuifikisha Tanzania kwenye hatua hiyo kubwa.

Uzoefu walioupata kuanzia kwenye Ligi Kuu ya Wanawake Bara na mashindano mbalimbali ya kimataifa yamechangia kwa kiasi kikubwa.

Kiwango kizuri cha Minja ambaye hadi sasa ndiye kinara wa Tanzania akifunga mabao matatu ikiwa tofauti ya bao moja na kinara wa mashindano ya Futsal, yamemfanya mkali huyo wa kupiga frii-kiki na penalti kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo.

Mbali na Minja lakini pia kipa Naijat alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo na mashuti langoni kwenye mechi mbili alizocheza dhidi ya Senegal na Cameroon na hilo limethibitishwa baada ya kuondoka na tuzo ya mchezaji bora.

Licha ya Morocco kubeba ubingwa lakini tuzo ya kipa bora wa fainali ilikwenda kwa mwanadada huyo Mtanzania.

MSIKIE KOCHA

Kocha wa timu hiyo, Curtis Reid alisema: “Nimefurahi wachezaji walicheza vizuri, Morocco wana kila kitu kuanzia miundombinu, tulionyesha kiwango bora naamini tutakuwa bora zaidi siku za usoni.”