Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons wasiingie kwa mazoea dhidi ya Polisi

PRISONS Pict

Muktasari:

  • Mechi hizo mbili ni za hatua ya mchujo dhidi ya Polisi Tanzania ambapo kama itapoteza itashuka daraja na ikifanya vizuri itabaki Ligi Kuu.

MAAFANDE wa Tanzania Prisons wamebakisha mechi mbili za kuwabakisha Ligi Kuu vinginevyo watakwenda na maji na kushuka hadi ligi ya Championship.

Mechi hizo mbili ni za hatua ya mchujo dhidi ya Polisi Tanzania ambapo kama itapoteza itashuka daraja na ikifanya vizuri itabaki Ligi Kuu.

Tanzania Prisons ina fursa ya mwisho ya kujitetea baada ya kushindwa kufanya hivyo dhidi ya Mbeya City katika hatua ya kwanza ya mchujo kwa kufungwa jumla ya mabao 2-0.

Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania Prisons kucheza mechi za mchujo ili kupigania kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hata hivyo safari hii inapaswa kujipanga vilivyo kwa vile aina ya timu wanayokutana nayo sio nyepesi hata kidogo.

Polisi Tanzania ina kikosi chenye wachezaji wazuri ambao wanaweza kukabiliana na timu ya aina yoyote ndani ya nchi hii.

Lakini pia wana kocha mzoefu, Mbwana Makata ambaye ana historia nzuri ya kupandisha timu daraja kwa nyakati tofauti.

Sisi hapa kijiweni tunatamani na tunasubiria kwa hamu mechi hiyo ya ndugu wawili kwani tunajua itakuwa ya kukata na shoka.