Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Opare Collins...Mayele, Morisson acha kabisa

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akishangilia bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Picha| Loveness Bernad

“MAMA ndiye alinitabiri nitakuwa star na nyota kila pande. Nikiwa na raha kwa mwenye hasira nisijigambe, usimpige mkeo piga shangwe kwa maana ‘young killer’ sio ngazi, hivyo mwambie shetani asinipande.”

Hiyo ni baadhi ya mistari ya staa wa Bongofleva nchini, Kassim Yusuph maarufu Young Killer aliyoimba kwenye wimbo wake uitwao 13 aliomshirikisha Fareed Kubanda ‘Fid Q’ miaka mitano iliyopita.

Young Killer anaamini mama’ke ndiye alimtabiria makubwa anayoyafanya hadi leo jambo ambalo ni sawa na mshambuliaji wa Biashara United, Mghana Opare Collins (21).

Mwanaspoti limefanya mahojiano na Opare aliyefunguka maisha yake ya soka na binafsi.


USTAA TOKA KWA MAMA

Opare anasema safari ya kucheza soka ilianza akiwa shule nchini kwao Ghana katika eneo la Nobewam baada ya kuaminiwa na mwalimu wake kisha kupewa baraka na mama’ke, Yaa Georgina. “Nilikuwa nacheza kawaida tu shule na mtaani, lakini siku moja mwalimu wangu akaniambia najua kucheza mpira na kabla ya hapo mama alishaniambia anatamani niwe mcheza mpira,” anasema.

“Kauli hizo mbili niliziunganisha na kugundua kuna kitu ninacho. Niliporudi nyumbani nikamwambia mama kuwa mwalimu kaniambia najua kucheza mpira, basi akafurahi na kuniambia niendelee kucheza ipo siku nitakuwa mchezaji mkubwa.”


MSHUA AZINGUA

Wakati Opare akiwa mdogo chini ya miaka 10 huku ndoto zake zikiwa ni kucheza soka, wazazi waliachana na Opare kwenda kuishi na baba’ke, Kojo Owusu lakini mambo hayakumuendea vizuri na baadaye kurudi kwa mama.

“Niliishi na baba, lakini akawa hanipi muda wa kutosha kucheza mpira. Siku moja aliniambia mpira si chochote wala hautanifikisha sehemu yeyote, hivyo nitafute kitu kingine cha kufanya kwani hata mtaani kwetu hakuna mchezaji hata mmoja aliyefanikiwa.

“Kauli iliniumiza kichwa, halafu ukimuangalia baba kamaanisha na kanuna. Kiukweli ilinibidi nichukue uamuzi wa kurudi kwa mama ambaye alinipokea vizuri,” anasema Opare.


AACHA SHULE

Kumbe staa huyu aliyekamata namba ya kudumu kikosi cha kwanz apale Biashara United aliacha shule na hapa anaeleza kwanini, “baada ya misukosuko ya familia, mwaka 2015 nikiwa na miaka 14 niliamua kuacha shule na hapo nilimuambia mama kuwa siioni shule kama itanisaidia kufikia malengo yangu ya soka na kuomba kutumia gharama zile za shule kwenye soka.

“Baada ya hapo mama alianza kunisapoti kwa kila kitu ikiwemo kunipa pesa ya kununua viatu, jezi na hata nauli huku akinipa moyo kuwa ipo siku nitafanikiwa.”

Opare anaeleza kuwa hapo ndipo safari yake ya soka ilianza rasmi na alipata timu ya Daraja la Pili iitwayo Miracle SC aliyo-ic-h-ezea kuanzia 2015 hadi 2018 alipoamua kutimkia mjini Accra kujiunga na Accra Lions na baadaye kuachana nayo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kisha kurudi Miracle kabla ya kuja Bongo.


BIASHARA MAJARIBU

Msha-mbuliaji huyo mwenye mabao matatu hadi sasa Ligi Kuu Bara na moja la Kombe la Shirikisho la Azam anaeleza safari yake kuja Tanzania kuwal iikuwa kwa ajili ya majaribio. “Baada ya kurudi Miracle alitokea kaka mmoja aitwaye Abraham akanambia nina kipaji kikubwa sipaswi kucheza katika madaraja ya chini, hivyo ananitafutia timu nje ya Ghana ambapo nitacheza zaidi,” anasema Opare.

“Hapo ndipo akanileta kufanya majaribio Biashara. Nakumbuka tulikuwa sita wakati ule, lakini walinikubali mimi zaidi ikabidi nibaki hapa. Nilikaa nusu msimu bila kucheza kutokana na kutokuwa na vibali na baada ya dirisha dogo la usajili ndio nimeanza kucheza.”

“Nafurahia maisha haya licha ya kwamba kuna changamoto zake, ila naamini inanijenga na kunifanya niwe bora zaidi nikizidi kupambania ndoto zangu kwani bado nafasi ninayo ya kufanya makubwa zaidi,” anaesema Opare aliye tayari kuichezea timu yoyote watakayofikia makubaliano.


MAYELE NOMA

Licha ya wote kuwa washambuliaji lakini, Opare anakiri kuwa staa wa Yanga, Fiston Mayele kwa sasa ni bora zaidi kutokana na namna anavyocheza na kufunga.

“Ujue mimi sina chuki na mtu. Kwa sasa kwenye ligi namkubali sana Mayele. Jamaa anajua kutafuta na kufunga mabao. Akiamua kufanya jambo hashindwi na hata akishindwa utaona jitihada. Hakika kuna vitu najifunza kwake,” anasema Opare anayemfuatilia zaidi Ulaya mshambuliaji wa Manchester United, Christiano Ronaldo.


MORRISON MTU NA NUSU

Kama ulidhani nyota wa Simba, Benard Morrison ni mtukutu kwenye maisha ya kawaida kama ilivyo uwanjani, sahau hilo kwani Opare amenaelezea kuwa ni mtu na nusu. “Morisson ni zaidi ya binadamu. Ujue tulikuwa hatufahamiani kabla, lakini nilivyokuja Tanzania akajua nilimfahamu na alivyojua ni Mghana mwenzake upendo wake kwangu na Zigah (Christian - mchezaji mwenzake Biashara) uliongezeka maradufu,” anasema Opare ambaye licha ya yeye, Morisson na Zigah kuwa raia wa Ghana lakini hawatoki eneo moja nchini humo.

“Ni mtu ambaye unaweza kumpigia simu kumsalimia akakuuliza matatizo yako mengine na ukimuambia ikoje basi anakusaidia. Amekuwa akitutumia hela na kutusaidia kwa vingi ikiwemo kutushauri. Hata tulipokuja kucheza Dar - Simba ikashinda 3-0, alikuja kambini kwetu akatupa zawadi, chakula na pesa pia alitamaini tukae naye muda mrefu lakini ratiba ilikuwa imebana. kiufupi ni mtu poa sana.”


MALENGO MAKUBWA

Opare aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu Biashara United anaeleza kuwa na ndoto yake kubwa ataifikia na kuwaziba midomo waliowahi kumbeza. “Kila kitu ni ndoto, mfano juzi kati niliongea na baba baada ya muda mrefu alifurahi kuona ndoto yangu ya kucheza mpira kimataifa imetimia licha ya kwamba mwanzo hakutaka nifanye hivyo.

Sasa napigania ndoto kubwa zaidi. Natamani kuichezea timu ya taifa pia kucheza kwa mafanikio katika kila klabu ninayopita na naamini Mungu ataniwezesha nitazichezea klabu kubwa Afrika na duniani muda ukifika,” anasema Opara mwenye malengo ya kufunga mabao 15 msimu huu na sasa amefikisha matatu.