Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Novatus endelea kuwapambania wenzako

Muktasari:

  • Miongoni mwa ambayo Novatus ameyasema ni amekuwa akiwatafutia fursa wachezaji wenzake hapa nchini ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi lakini muitikio umekuwa ni hasi.

KIJIWE kimefuatilia vyema mahojiano kati ya Novatus Miroshi na kituo kimoja cha luninga hapa nchini.

Miongoni mwa ambayo Novatus ameyasema ni amekuwa akiwatafutia fursa wachezaji wenzake hapa nchini ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi lakini muitikio umekuwa ni hasi.

Kwamba anatengeneza mazingira ya hao wachezaji wapate timu za kujiunga nazo nje ya Tanzania lakini wenyewe wamekuwa wakizipotezea na wengi wanatamani kubaki hapa nchini na kwenda Simba na Yanga.

Hili ni jambo kubwa sana ambalo Novatus amekuwa akilifanya na kiukweli anastahili kupata pongezi nyingi kwa sababu sio wachezaji wengi wenye moyo kama wake.

Tunamwelewa Novatus kwa hicho anachokifanya kwa vile anaifikiria zaidi timu yetu ya taifa ‘Taifa Stars’ ambayo kiukweli bado haina idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Inakatisha tamaa kwa mchezaji pindi wenzake ambao anawapigania kwa kuwatafutia fursa, wanamwangusha kwa kuona maisha yao wayamalizie hapa nchini katika klabu zetu kubwa ambazo wakati mwingine hata baadhi haziwasajili.

Hapa kijiweni tunamwomba Novatus licha ya wenzake kutoonyesha utayari wa kwenda nje, asichoke kutafuta fursa kwa ajili yao bali aendelee kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wake.

Inawezekana wapo ambao wana utayari wa kufanya hivyo ila bado hajaweza kuwafikia na zikitokea fursa watazichangamkia tofauti na walichokifanya wenzao.

Asikatishwe tamaa na wale ambao hawaonyeshi utayari wa kile anachowashauri bali awafikirie zaidi ambao wanatamani fursa hiyo lakini bado haijawafikia.