Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni fainali za Antonela na Georgina

FAINALI Pict

Muktasari:

  • Tayari mastaa hao wameshafanya mambo makubwa katika nchi zao na sasa Ronaldo anayeiwakilisha Ureno na Messi wa Argentina wanakimbizana na umri, lakini kila mmoja akiwa na majukumu mawili muhimu kwenye mashinda hayo; kuhakikisha nchi yake inafika mbali pia anavunja rekodi binafsi tangu alipoanza kushiriki michuano hiyo.

WASHINGTON, MAREKANI: KULE Marekani ndiko waliko Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakiziwakilisha nchi zoa katika fainali za Kombe la Dunia 2026, huku wakiwa na ndoto kubwa za kuvunja rekodi fulani katika historia ya soka la kimataifa.

Tayari mastaa hao wameshafanya mambo makubwa katika nchi zao na sasa Ronaldo anayeiwakilisha Ureno na Messi wa Argentina wanakimbizana na umri, lakini kila mmoja akiwa na majukumu mawili muhimu kwenye mashinda hayo; kuhakikisha nchi yake inafika mbali pia anavunja rekodi binafsi tangu alipoanza kushiriki michuano hiyo.

Hata hivyo, nyuma yao kuna mashabiki wa aina tatu wanaosindikiza ndoto zao zitimie ambao ni wale wa nchi wanazozichea yaani wananchi wenzao, wa klaba zao na pia wake na wapenzi wao.

FAIN 04

Ronaldo ni mpenzi wa mrembo Georgina Rodriguez huku Messi akiwa mume wa ndoa wa Antonela Roccuzzo na wote hao wapo nao nchini Marekani.

Lakini, jambo unalopaswa kujua ni kwamba warembo hao wamekuwa wakifunika zaidi mitandaoni pale wandani wao wanapocheza mechi za mashindano hayo kwani huko mitandaoni wamekuwa wakivuruga kwa kuposti vitu vingi kuanzia picha wanazopiga wakiwa viwanjani, vaibu la mashabiki na ujumbe wa kuwatia mioyo wanaume wao na ni hapo ndipo fainali hizi zimepachikwa kuwa zao. 

FAIN 01

Mathalan, majuzi wakati Messi akiichezea Argentina na kufanikiwa kupiga hat trick dhidi ya Algeria katika mechi ya hatua ya makundi, Antonela alichapisha picha kadhaa katika ukurasa wake wa Instagram akiwa na familia yake na kupongeza mumewe zikisindikizwa na mabusu motomoto.

Mwanadada huyo alirudia tena pale mumewe huyo alipofunga mabao mawili dhidi ya Austria na vilevile kwenye ushindi wa mabao 3-1 alipotupia dhidi ya Jordan. 

FAIN 05

Kwa upande wa Georgina sapoti lake la Ronaldo si mchezo akiwa na watoto wao, lakini mara nyingi katika posti zake akiwa uwanjani amekuwa akitumia fursa hiyo kutangaza biashara yake mpya ya mavazi.

Georgina alihudhuria mchezo wa Ureno dhidi ya Colombia mjini Miami akiwa na watoto wao ambao ulimalizika kwa suluhu na ni ule ulioibua kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya mashabiki waliodai Ronaldo hakuwa na msaada kwa timu.

FAIN 03

Ni katika mchezo huo mwadada huyo alitoa sapoti kubwa kwa mwandani wake akimtumia maneno ya faraja. Kwa upande mwingine, watoto wao Cristiano Ronaldo Jr na Mateo wamekuwa sambamba na mama yao kama walivyo wale wa Messi ambao muda wote wako jukwaani na mzazi wao wa kike kum sapoti baba yao.