MZEE WA UPUPU: ASFC inakua, lakini maandalizi yanadumaa
Msimu wa nane wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports upo kwenye hatua ya nusu fainali na tayari nusu fainali moja imefanyika wikendi hii.
Ilikuwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ambapo Azam FC waliwakaribisha Simba na kushinda 2-1.
Achana na ufundi wa James Akaminko. Achana na uwezo wa Isah Ndala. Na pia achana na namna Daniel Amoah alivyomuweka mfukoni Jean Baleke.
Nataka uangalie mchezo wenyewe kwa ujumla ulivyokuwa. Kiwango kibovu, mipira ya butua butua na pasi nyingi zilizopigwa kupitia katikati ya uwanja.
Pasi zilizotawala mchezo huu ni ndefu na za pembeni. Hii ni kwa sababu ya ubovu wa uwanja. Uwanja wa nangwanda Sijaona haukuwa tayari kwa mchezo wa Mei.
TFF wenye mashindano yao angalau mchezo huu waneuahirisha kama ule wa Singida kusubiri uwanja uwe vizuri.
Mashindano haya ambayo yalianza 2015/16 yamejipatia umaarufu mkubwa na yanazidi kuongez mvuto. Lakini maandalizi yake yamekuwa ya zima moto kila msimu.
Hivi kwanini TFF inashindwa kutangaza viwanja vya fainali mwaka mmoja kabla? Kwa mfano kwenye fainali ya mwaka huu pia watangaze kabisa uwanja utakaotumika kwa nusu fainali na fainali ya msimu wa 2023/24, 2024/25 na 2025/26.
Mikoa itakayoandaa mechi hizo ikijijua mapema, itafanya maandalizi mazuri ya uwanja na kufikia siku ya mechi uwanja unakuwa na hadhi ya nusu fainali kweli.
Mchezo wa Azam FC na Simba uliharibiwa sana na ubovu wa uwanja kiasi cha kusababisha makocha kutowaruhusu wachezaji wao kuwa huru sana na mpira.
Ukipata mpira piga mbele watu wagombanie, ukisema ukae nao unaweza kusababisha matatizo kwa sababu uwanja hauruhusu.
Unaweza kusema unataka kukokota, mpira ukadunda kwenye moja ya vinundu vya uwanjani, ukatoka kwenye himaya yako na kuhamia kwa wapinzani. Sasa hilo likitokea karibu na lango lako si ni hatari hiyo?
TFF inapokaa na kuandaa mashindano haya, inayaandaa kwa kiwango cha chini sana, sijui ubunifu umfika mwisho au hawataki kuekeza!?
Ingekuwa sahihi sana TFF ikaamua mechi zote za nusu fainali na fainali zikafanyika uwanja wa Mkapa ili mbongi la hali ya juu lipigwe na kuitendea haki mechi.
Ilianza kama utani mwaka 2017 pale TFF ya Malinzi ilipoipeleka fainali Dodoma. Ilielekeweka kwa wakati ule kwa sababu upepo wa nchi ulivumia Dodoma kutokana na "Mzee" kuhamishia serikali yake mjini humo.
Lakini mwaka uliofuata, 2018, nao ukawa wa zimamoto. Fainali ikatangazwa kupelekwa Arusha kwa tangazo la ghafla.
Alipoingia madarakani bwana Karia ndiyo akaongeza na mechi za nusu fainali kufanyika kwwnye uwanja utakaoteuliwa na mamlaka.
Siyo wazo baya hata kidgo lakini TFF inataliwa kuwekeza kwenye hili. Mikoa inayopata nafasi ya kuandaa mechi hizi iimeshindwa kufanya maandalizi yanayostahili ukubwa wa mchezo huu.
Kwenye mechi ya Azam FC na Simba, hadi siku moja kabla ya mchezo uwanja ulikuwa katika matengenezo. Kwa kawaida timu hufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi, lakini kwa Ndangwanda hicho litu mimi kama mwandishi Sijaona. Timu ziliruhusiwa kuungalia tu naa kuondoka kwenda kifanya mazoezi kwenye viwanja watakavyojitafutia wenyewe.
Na hilo ni tatizo jingine kwenye kupeleka mechi hizi mikoani. Ukiacha uwanja wa mechi, mikoa yetu haina viwanja ambavyo timu zitafanya mazoezi kabla ya mchezo.
Viwanja ambavyo Azam FC na Simba zilifanya mazoezi kabl ya mechi hii ni kituko. TFF inatakiwa iliweke hili kwenye kanuni za mashindano kwamba mkoa utakaopata nafasi ya kuandaa mechi hizi, uhakikishe pia unaanmdaa viwanja viwili vizuri vya mazoezi kwa ajili ya wageni.
Kuicheza nusu fainali kwenye uwanja wa kubahatisha "kunapunguza utamu" wa mchezo kwa sababu wachezaji hawawezi kufunguka barabara. Lengo la awali lilikuwa kupeleka mechi hizi kwenye viwanja ambavyo havijawahi kuona burudani ya soka la kiwango kama hicho kwa miaka mingi au hawajawahi kuona kabisa.
Lakini ghafla hilo limepuuzwa na fainali imepelekwa Tanga. Siyo mbaya pia lakini basi maandalizi yaboreshwe. Angalau fainali ya msimu uliopota kule Arusha kwa sababu uwanja ule ulitengezwa kwa ajili ya nusu fainali. Japo nao haukuwa tayari kwa ajili ya nusu fainali, lakini haukuchakaa baada ya nusu na ukaonekana kufaa kwa fainali.
Lakini kwa sasa ni tofauti kabisa. Viwanja havijirudii na hakuna anayejali. Mechi kubwa kama hizi zikifanyika kwenye uwanja bora inakuwa safi sana kwa fainali ya pande zote mbili uwanjani.
Tanzania tuna bahati kwamba tunaye mtu aliyewekeza mabilioni ya penasa kwenye mpira wetu. Ili kumlibda yeye na kuwavutia wengine, kanunia yaamdalizi lazima ihusishe moja kwa moja kwenye mamambo ya miundombino. Nia njema ya TFF inaharibiwa na maandalizi ya muda mfuoi na kusababisha kuwa na mechi ya nusu fainali kuchezwa bila shida yoyote.