Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE WA KALIUA: Simba, MO ziheshimiane

Muktasari:

  • Mohammed Dewji hakuishia hapo tu. Alikwenda Sokoni na kuketa Makocha wa Daraja la juu Msimbazi. Patrick Aussems, Sven Ludwig Vandenbroeck, Abdelhak Benchikha na wengine wengi wameupata Heshima kuwa sana Klabu ya Simba na mpira wetu kwa ujumla.

Kama kuna mtu ameleta Mapinduzi makubwa kwenye Soka letu zama hizi, basi ni Mohammed Dewji. Usajili wa watu kama Jose Luís Miquissone, Clatous Chota Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Aishi Manula, Rally Bwalya na wengine waliifanya Simba kuwa timu tishio ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Mohammed Dewji hakuishia hapo tu. Alikwenda Sokoni na kuketa Makocha wa Daraja la juu Msimbazi. Patrick Aussems, Sven Ludwig Vandenbroeck, Abdelhak Benchikha na wengine wengi wameupata Heshima kuwa sana Klabu ya Simba na mpira wetu kwa ujumla.

Maisha ya ujanja kwenye mpira wetu yanaelekea Ukingoni. Maisha ya mpira wetu kuchezewa na Masela yameanza kufika Tamati. Mpira wetu unakuwa kila kukicha. Nafasi za wapigaji taratibu zinaondoka. Kumekuwa na Matangazo Mengi sana ya Biashara kati ya Mohammed Dewji na Klabu ya Simba.

Kuna namna Mohamed ananufaika sana na Klabu ya Simba kwa kutangaza Biashara zake. Kuna namna anajufaika sana yeye kuwa Sehemu ya Simba Kibiashara. Kwa Pesa ambazo Mohamed amechangia Simba, Klabu pia imenufaika sana.

Kuendesha timu sio jambo dogo. Simba inapswa kumuheshimu sana Mohammed. Mohammed anapswa kuiheshimu sana Simba. Wote wamesaidiana. Wote wametoana mbali.

Kila mmoja amenufaika kwa upande wake. Kwa Sababu zama zinabadilika, mambo ya Ufadhili yamepitwa na wakati. Simba imekuwa kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa Klabu kwa karibu miaka Saba sasa.

Hakuna kinachokamilika. Kila siku utasikia mchakato unaendelea! Kumekuwa hakuna uwazi wowote kwenye Ndoa ya Klabu ya Simba na Mohamed Dewji. Kumekuwa na ukakasi mwingi sana. Viongozi wa Klabu wameshindwa kuwa wakweli na wawazi mbele ya Wanachama na Mashabiki wa Simba. Muwekezaji naye anakuja na matamko mara kwa mara yenye kuwavuruga Mashabiki.

Ukiona unaingia kwenye Mgogoro na Mchumba wako, hiyo Ndoa achana nayo. Kuna historia nzuri sana baina ya Klabu ya Simba na Mohamed Dewji.

Kuna Mafanikio makubwa sana ambayo kila upande umenufaika lakini, hii vuta ni kuvute haina Afya kwa upande wowote. Hizi ni zama za Biashara sio fadhila. Serikali baada ya Simba kuja na mawazo ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa Klabu za Mpira, ulikuja na kuleta utaratibu wa Wawekezaji walau kuwa Watatu ekes timu za Wanachama kama Simba.

Nadhani Simba inapaswa kwenda huko. Nadhani Simba inapaswa kufanya kidogo marekebisho ya Katiba yao kuelekea huko. Migogorp ya Mohammed Dewji na Klabu ya Simba imetajwa sana katika Kipindi cha misimu mitatu ya hivi karibuni ambapo Simba haijafanya vizuri.

Imeshindwa Kufika Nusu Fainali Klabu Bingwa Afrika. Imeshindwa kufika Kutwaa Taji lolote kubwa hapa Nyumbani. Ukiona unaanza Migogoro na Mchumba wako kal ya ya Ndoa, ni Bora Usiingie kabisa kwenye Ndoa yenyewe.

Habari za kuwa na Tajiri anayetoa Pesa za Hisani zimepitwa na Wakati. Simba kwa sasa wanahitaji Muwwkwzajo sio Mfadhaili. Kama Simba wataenda na Staili hii kuna siku watamkosea Heshima Mohamed Dewji. Kama Mohamed Dewji ataendelea kubaki Simba kwa namna hii kuna siku ataikosea Heshima Simba.

Moja kati ya Makosa makubwa ya Viongozi wa Klabu ya Simba, ni kushindwa kuweka wazi Makubaliano ya Mohammed Dewji na Klabu yao. Hakuna mtu aliyenyooka Katika hili.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana katika mchakato wa uwekezaji. Kumekuwa na utata mwingi sana wa Taarifa. Kama hili jambo halitowekwa sana, kuna siku MO ataikosea Heshima Simba. Kama hii migogoro itakomaa, kuna siku Simba itamkosea Heshima MO.

Simba na MO ni lazima wakae chini wamalizane vizuri. Klabu inahitaji kuwa na Wawekezaji walau watatu ili kupunguza Ngonjera. Klabu inahitaji kuwa na Wawekezaji sio Wafadhili. Ni kweli Klabu zetu nyingi zimedumu kwa Sababu ya Fadhila za watu mbali mbali lakini muda umebadilika. Zama zimebadilika. Dunia ya Hisani haipo tena.

Ni muda wa kuanza kufanya Biashara . Kama Mohamed Dewji bado anaitaka Simba, wakae chini wazungumze makubaliano upya. Simba ya miaka sita nyuma, sio Simba pia ya leo. Ni muda wa Klabu ya Simba kuingia makubaliano ya Kibiashara sio Ushabiki na Hisani tena. Viongozi wa Simba ni lazima wawe wakweli kwenye hatua zote za mchakato kwa Wananchama na Mashabiki. Klabu haiwezi kupelekwa Kihuni kihuni tu.

Mohammed anapaswa kuniheshimu Simba na Simba, inapaswa kumuheshimu Mohammed. Kila mtu amemtoa mwenzie mbali. Mchakato wa uendeshaji wa Klabu ya Simba imekuwa na longolongo sana.

Kuna muda hujui hata mkweli Nani! Simba ni kama imechezewa kwa miaka karibu saba sasa! Klabu ya Simba imeendelea kuishi kizamani. Zama zimebadilika. Simba wanapswa Kuandaa mazingira upya ya Uwekezaji bila kutazama uwepo wa Mohammed Dewji. Wanapswa kuzungumza naye vizuri ili kuondoa sintofahamu. Anaweza kuwa na matatizo yake kama Mwanadamu yotote lakini haiondoi ukweli kuwa ametoa mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya Klabu.

Ni wakati wa kuanza upya. Simba inahitaji kufanya marekebisho Kidogo ya Katiba yao. Simba inahitaji kipengele kinachoruhusu Wawekezaji zaidi ya Mmoja. Simba inahitaji kufanya tathimini upya ya kujua thamani halisi ya Klabu. Simba inahitaji kutoa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi upande wa Wanachama .

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kwa upande wa muwekezaji wanapswa pia kuthibitishwa na Wanachama . Simba inabidi iende mbele. Simba inabidi iwe ya Kisasa zaidi. Mambo ya kutegemea Hisani za watu yamepitwa na wakati. Vilabu vyetu hasa Simba na Yanga vinaumasikini wa Kimfumo tu.

Siku mifumo ya Klabu hizi zikikaa sawa, ni fahari nyingine kwa Nchi ya Tanzania. Shida kubwa ya Simba ni kujidanganya kuwa wameshafanya Mabadiliko. Hapa ndipo panapoifelisha Simba. Viongozi wengi sio wakweli. Wamesema mara nyingi tu kuwa Mohammed Dewji ametoa Pesa! Huu Uongo haukupaswa kuachana bila kukanusha.

Ni kweli Dewji ameibeba Simba lakini ni kweli pia kuwa Simba imembeba. Ni muda wa pande zote kukaa chini na kufanya makubaliano upya. Ni vema Simba kuona faida ya kuwa na Wawekezaji zaidi ya Mmoja. Itasaidia sana Tajiri kuacha kususa. Itasaidia sana kuondoa Utegemezi wa mtu maana kuna Kesho. MO na Klabu ya Simba ni lazima wakae chini ili kupata namna Bora ya kuendesha Klabu.

Mabadiliko ya Klabu ya Simba yamejaa Janja Janja sana. Kila mtu amegeuka Chawa kwenye kuipiga Simba. Huu ni wakati wa Klabu ya Simba kumuheshimu MO na Mohammed kuiheshimu Klabu ya Simba. Lakini ukiona Migogoro wakati wa Uchumba, huo ni mtego. Kwenye Ndoa itakusumbua sana.