Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE WA FACT: Ilikuwa wikiendi ‘nambari wani’

Rejea wimbo wa “You’re my number one” wa Enrique Iglesias, mwanamuziki wa Marekani mwenye asılı ya Hispania.

Katika maisha yake alidhani ameshaona kila kitu duniani hadi alipokutana na mpenzi wake mpya ndipo akanyoosha mikono juu na kusema “wewe ni namba wani” kutokana na mahaba motomoto aliyokuwa akimmwagia.

I’ve sailed in a perfect dream

I’ve seen the sun make love to the sea

I’ve kissed the moon a million times

Danced with angels in the sky

Nimeshaelea kwenye ndoto kamili

Nimeshaliona jua likifanya mapenzi na bahari

Nimeshauchumu mwezi mara milioni moja

Nimedansi na malaika ambani

I’ve even seen miracles

I’ve felt the pain disappear

But still haven’t seen anything

That amazes me quite like you do

Nimeshaona hadi miujiza

Nimeyahisi maumivu yakipotea

Lakini sijawahi kuona kitu chochote

Kilichonishangaza kama unavyofanya wewe

Yaani jamaa alidhani ameshafanya kila kitu maishani. Alidhani ameshaona kila kitu, lakini kumbe alikuwa hajaona malavidavi ya binti wa watu.

Hiki ndicho kilichoikuta Tanzania wikiendi hii. Kwa miaka yote ya kabla na baada ya uhuru, Tanzania iliamini kwamba imeshaona kila kitu kwenye mpira.


Robo fainali ya klabu bingwa 1969.

Hii ni robo fainali ya Afrika iliyoshuhudia Yanga wakitolewa kwa kurusha shilingi baada ya sare ya 1-1 nyumbani na ugenini.

Na inasemekana kwenye urushaji shilingi, Yanga ilistahili kushinda kwani shilingi hiyo iliangukia upande ambao Yanga iliuchagua, lakini nahodha wa Asante Kotoko, İbrahim Sunday, akapiga kelele za kushangilia na kumchanganya mwamuzi.

Nahodha wa Yanga, Abdulrahmani Juma akazubaa na kumfanya mwamuzi aamini kwamba Kotoko wameshinda na safari ya Yanga ikaisha hivyo.


Robo fainali klabu bingwa 1970

Hii ilikuwa robo fainali ya kısası kwa Yanga kukutana tena na Asante Kotoko. Kama ilivyokuwa mwaka 1969, safari hii tena mechi zote mbili ziliisha kwa sare ya 1-1.

Lakini tofauti na wakati ule, safari hii sheria zilibadilika. Badala ya kurusha shilingi kulikuwa na mchezo wa tatu katika uwanja huru.

Kwa hiyo mechi ya tatu ikapangwa kufanyika Ethiopia na Yanga wakafungwa 2-0 na kutolewa.


Nusu fainali klabu bingwa 1974

Safari ilikuwa safari ya Simba kuwaonyesha Watanzania kitu ambacho hawakuwahi kukiona. Ikishiriki mara ya kwanza mashindano ya Afrika, Simba ambayo miaka michache iliyopita ilitoka kubadili jina kutoka Sunderland ilifika nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Ilikutana na Ghazl El Mahalla, timu ya kutoka Misri. Mchezo wa kwanza ugenini Simba walipoteza kwa bao 1-0 na kuja kushinda nyumbani baoa 1-0.

Mechi ikaingia hatua ya mikwaju ya penati na Simba wakakosa zote.


Fainali ya Kombe la CAF 1993

Baada ya miaka mingi Tanzania ikarudi kwenye ngazi za juu Afrika kwa klabu ya Simba kutinga fainali ya mashindano hayo mapya yaliyoanza mwaka mmoja nyuma yake.

Simba ilianzia ugenini nchini Ivory Coast dhidi ya Stella Abidjan na kupata suluhu huku matumaini yakiwa mengi kwamba wataimaliza kazı nyumbani.

Lakini haikuwa bahati, ikapoteza nyumbani kwa mabao 2-0 na kulikosa kombe.


Fainali ya Kombe la Shirikisho 2023

Miaka 30 baada ya Simba kufika fainali ya mashindano ya Afrika, watani wao wa jadi, Yanga SC nao wakajibu mapigo kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, licha ya ushindi wa ugenini wa 1-0, Yanga ililikosa kombe baada ya kuwa ilikubali kufungwa mabao 2-1 nyumbani.


2024 ni nambari wani

Mwaka huu, 2024, Tanzania inashuhudia klabu zake mbili zikicheza hatua ya robo fainali ya Afrika katika wikendi moja juu ya ardhi ya nyumbani.

Tena siyo tu robo fainali, bali dhidi ya miamba hasa wa soka la Afrika.

Simba wakiwaalika mabingwa wa kihistoria Al Ahly na Yanga ikiwaalika vinara wa ubora kwa soka la klabu, Mamelodi Sundowns.

Hii ni miujiza mikubwa kama ile ya Enrique Iglesias kwenye wimbo wake. Kuna mechi nne za robo fainali, lakini hizi mbili ndizo zilizungumzwa zaidi baranı Afrika.

Tanzania ni nchi pekee ambayo timu zake mbili zimefuzu hatua hii ya mashindano msimu huu. Hii inaongeza mshawasha na bashasha kwa Afrika nzima kufuatilia zaidi kınachoendelea Tanzania.

Ama kwa hakika hii ilikuwa wikiendi nambari wani.