Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwangosi atuma ujumbe Simba, amtaja Sadio Mane

MWANGOSI Pict


KAULI mbinu ya mshambuliaji wa Simba, Baraka Mwangosi ni usipojiamini hakuna anayeweza kukuamini na kukubali, anaitumia kama silaha yake ya kuzipambania ndoto za kuwa mchezaji mkubwa ndani na nje ya nchi.


Katika mahojiano na Mwanaspoti, Mwangosi anaeleza kila hatua katika maisha yake inabeba mafunzo ya kujituma, uvumilivu na bila kukata tamaa, akingoja muda sahihi utakaomtambulisha kwa matendo.


Ikumbukwe kuwa, Simba ilimsajili Mwangosi kutoka Mbeya City kipindi cha usajili wa dirisha dogo la Januari 2026. Pia aliwahi kuichezea Mbeya Kwanza ya Ligi ya Championship.

Ndani ya Simba, tangu ametua Januari 2026, amecheza mechi nne za Ligi Kuu, huku zingine tano akiwa Mbeya City na kufanya jumla kucheza mechi tisa, ana asisti moja.

Bao pekee alilonalo ni lile la Kombe la Shirikisho la CRDB alilofunga wakati Simba ikishinda 3-0 dhidi ya Greenland ikiwa hatua ya 64 bora.

MWANGO 01

Katika nafasi yake ya ushambuliaji ndani ya kikosi cha Simba, ukimuondoa Jonathan Sowah aliyeondolewa kwenye majukumu akiwa amefunga mabao matatu, mwingine aliyekuwa anashindana naye ni Selemani Mwalimu aliyemaliza na mabao tisa.

Mwangosi aliyezaliwa Januari 28, 2002 (umri wa miaka 24) anasema anatambua kila kitu kina hatua zake, hivyo anajifunza ujasiri na kutokukata tamaa kupambana.

“Neno la Mungu katika kitabu cha Yoshua 1:9 kinanifunza ujasiri, hicho ndicho ninachokizingatia katika kazi zangu,† anaanza kusema.

MWANGO 02

Anaongeza: “Nazingatia nidhamu kwa ujumla ndani na nje ya uwanja, kwani wachezaji wengi wanaofanya vitu vikubwa wanajitunza na wanajua kufanya vitu kwa wakati.” 


MAISHA NDANI YA SIMBA

Anasema anaona mwanga mkubwa kucheza kikosi hicho na kila mchezaji kwake ana jambo la kujifunza, ili kuendelea kuwa bora na siku moja kutegemewa kucheza kikosi cha kwanza.

“Siyo kujifunza tu kwa wale ambao nacheza nao nafasi moja, najifunza vitu ambavyo vinafanya mchezaji kucheza kwa kiwango cha juu na kutegemewa na timu, hilo ndilo kubwa na la msingi.

“Pia napenda kuangalia mechi nyingi zilizopita kwa wachezaji mbalimbali ndani na nje ya nchi, naangalia uchezaji wao, nidhamu, kujituma kwao, najifunza na kuvifanyia kazi ndiyo maana nasisitiza uvumilivu ni kitu cha muhimu sana.”

MWANGO 03


AMTAJA SADIO MANE

Anasema tangu anakua alikuwa anamfuatilia mshambuliaji wa klabu ya Al-Nassr na timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane.

“Mimi nimezaliwa katika familia ya dini, baba yangu ni mchungaji, ndiyo maana namkubali sana Sadio Mane kutokana na nidhamu na unyenyekevu wake,” anasema. 

Anasema anajifunza utayari wa kila jambo, akizingatia akiwa ndani ya mpira anapaswa kufanya nini na kujiandaa baada ya kukaa nje na kazi hiyo.

“Kitu kinachowapa mawazo watu wengi siyo tu kwenye mpira, anapokuwa katika kazi fulani anasahau kwamba kuna kesho, lazima kujiandaa kupata na kukosa, mfano kama Mane ambaye haonyeshi kitu chochote zaidi ya kujihusisha na misaada katika jamii, hata akiwa nje ya soka hatasumbuka.” anasema.

Ukiachana na hilo, anasema msimu uliopita wa 2025-2026 umempa funzo wa kujipanga kisawasawa, ili kuhakikisha ligi ya msimu ujao inayotarajia kuanza Agosti 14, 2026 anafanya vitu vikubwa.

MWANGO 04

Alipoulizwa baada ya kujiunga na klabu ya Simba vitu gani vimebadilika kwake, anasema: “Naishi maisha ya kawaida kama nilivyokwambia nimelelewa familia ya dini, kwa hiyo siwezi kujua jamii inanichukuliaje.”

Jambo lingine ambalo Mwangosi anabainisha kwamba: “Mpira siyo umri, badala yake ni uwezo ambao mchezaji anaouonyesha uwanjani, nidhamu na huduma yake kuifaa timu.”

MWANGO 05

WADAU WANAMUONA MBALI

Staa wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel anasema anatambua kipaji kikubwa alichonacho Mwangosi, lakini anahitaji kupata uzoefu zaidi ili kutegemewa kikosi cha kwanza.

“Aina ya kikosi kama cha Simba kinachohitaji mchezaji wa kuamua matokeo, Mwangosi anahitaji muda wa kupata uzoefu naamini atafanya makubwa, kwani mikimbio yake na upigaji wake wa mipira yupo vizuri.”

Mwi ngine aliyemchambua Mwangosi ni nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Yusuf Mhilu aliyeichezea Geita Gold iliyopanda Ligi Kuu kwa msimu ujao, anasema: “Kwa umri wake ajitume, ajifunze zaidi kwa wen gine, asiwe na haraka ili asije akatoka katika mstari, naamini atakuja kufanya makubwa zaidi.”