Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakinyo, Kalolo walivyosepa na milioni 10 za Rais Samia

Mwakinyo Pict
Mwakinyo Pict

Muktasari:

  • Moto ulianza kuwaka kutoka Fayheroes Sports  Promotion kutokana na pambano lao ambalo lilifanyika Azura Beach, Kawe jijini Dar.

WIKIENDI iliopita kutoka Novemba 15 hadi 16, mwaka huu ilikuwa ya moto katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kutoka na kufanyika mapambano matatu makubwa huku mawili yakifanyika ndani ya siku moja.

Moto ulianza kuwaka kutoka Fayheroes Sports  Promotion kutokana na pambano lao ambalo lilifanyika Azura Beach, Kawe jijini Dar.

Katika pambano hilo jumla ya mapambano tisa yalichezwa kati ya hayo, mawili yalikuwa yakuania mikanda ya ubingwa  Pugulistic Syndicate of Tanzania PST ambapo bondia Jesca Mfinanga ambaye ni mtoto wa mwamuzi wa mchezo huo, Pendo Njau alikuwa na kibarua cha kuwania mkanda wa ubingwa huo dhidi ya Dorothea Mhoza.

MWAK01
MWAK01

Jesca yeye wala hakutaka shughuli yake kuwa ngumi kwani ndani ya raundi ya pili akafanikiwa kumtwangwa kwa Technical Knockout mpinzani wake Dorothea Mhoza na kufanikiwa kutwaa mkanda wa ubingwa wa PST kwa wanawake kwenye uzani wa Light.

Lakini pia Lupakisyo Shoti alikuwa na kibarua kizito mbele ya bondia mzoefu, Paul Kamata katika pambano la kuwania mkanda wa ubingwa wa PST kwenye uzani wa Middle.

Katika pambano hilo, Shoti alifanikiwa kushinda kwa pointi za majaji wote watatu kwa kumtandika Kamata na kuweza kushinda mkanda wake wa kwanza wa ubingwa kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Wakati mapambano ya Novemba 15, miongoni mwa mabondia walipanda ulingoni alikuwepo bondia na mchekeshaji, Miraji Supakila maarufu kama ‘Mkali Wenu’ ambaye alipanda ulingoni kwenye pambano la utangulizi la raundi sita dhidi ya Bakari Dunda.

MWAK02
MWAK02

Katika pambano hilo ambalo ni la pili kwenye ngumi za kulipwa kwa Mkali Wenu alifanikiwa kushinda kwa Knockout  ya raundi pili pamoja na mapambano mengine yaliopigwa usiku huo.

Novemba 16 katika jiji la Tanga kulifanyika pambano kubwa la aina yake ambalo liliwakusanya mabondia wengi wenye majina ambalo lilikuwa limeandaliwa na Mafia Boxing Promotion ikiwa na lengo kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Katika pambano hilo ambalo lilifahamika kama Ngumi ya Tanga, kura yangu ndiyo maendeleo ya Tanga ambapo pambano kuu lilimuhusisha Mtanzania, Kalolo Amiri dhidi ya Sandeep Kumar wa India.

MWAK03
MWAK03

Kalolo alipanda ulingoni kuwania mkanda wa PST katika uzani wa Bantam dhidi ya bondia huyo wa India na kufanikiwa kumtandika kwa Knockout ya raundi ya pili.

Ushindi huo umepelekea Mtanzania huyo kupewa zawadi ya shilingili milioni za KO ya Mama ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya motisha kwa mabondia wanaofanya vizuri katika mapambano ya kimataifa ambayo yatahusisha mikanda ya ubingwa.

Lakini mbali ya bondia huyo kulamba bingo ya mkwanja huo, Karim Mandonga alifanikiwa kumchapa mpinzani wake Alibaba wakati Abbada Cadabra akishinda kwa Knockout dhidi ya Snowden Munyanja Malawi wakati Yohana Mchanja akimpoteza pia Mghana,  Sihle Jelwana wa Ghana.

MWAK04
MWAK04

Wengine walioshinda katika pambano hilo, Oscar Richard akimtwanga Paul Magesta, Halima Vunja Bei akimchapa kwa Knockout Halima Bandora,  Luqman Kimoko naye akimdunda Bosko Bakari na Hassan Waziri naye akimpiga Yusuph Kileo kwa pointi.

Wakati  wakazi wa Tanga wakiendelea na sekeseke la kuangalia pambano la ngumi ya Tanga siku hiyo katika ulingo mwengine jijini Dar es Salaam kulikuwa na vita kali kiendelea ndani ya Ukumbi wa Warehouse, Masaki kwa Mtanzania, Hassan Mwakinyo aliyekuwa na kazi ya kutetea mkanda wake wa ubingwa wa World Boxing Organisation upande wa Afrika ‘WBO Afrika’.

Katika pambano hilo, Mwakinyo alitetea mkanda wake wa ubingwa wa WBO Afrika dhidi ya Daniel Lartey kutoka Ghana.

Mwakinyo ambaye alifanikiwa kutetea mkanda wake huo kwa mara pili kwa ushindi wa Knockout ya raundi ya tisa katika pambano ambalo lilipangwa kupigwa kwa raundi kumi kwenye uzani wa middle.

Ushindi huo umepelekea, Mwakinyo kufanikiwa kupewa zawadi ya Shilingi milioni  KO ya Mama ambayo imetoka kwa Rais wa Dk Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha mchezo wa ngumi za kulipwa hasa katika mapambano ya mikanda ya ubingwa wa kimataifa mabondia wanafanya vizuri.

Lakini baada ya ushindi huo, Mwakinyo ambaye kwa sasa ni bondia namba moja Afrika kwenye uzani wa middle na bondia wa 15 duniani katika mabondia wanaotambulika na WBO alitoa kauli yenye utata ambayo baadhi ya wadau wamekuwa na maswali mengi licha ya ushindi wake.

MWAK05
MWAK05

Mwakinyo alisema kuwa: “Pamoja na chuki mnazonionesha za wazi, watu ambao mnapaswa kunisaidia lakini mimi nitahakikisha siku moja mnasimama na kuamini kama mimi ndiyo bondia pekee wa Tanzania ninaeweza kuleta ubingwa wa dunia Tanzania, nitapigana vita vyote ambavyo mtapigana na mimi†.

Bondia huyo ameonyesha kuwa kuwa kuna kundi la watu linamuandama au limepanga kumpoteza lakini bado kauli yake imekuwa ikitengeneza maswali mengine ya kimsingi juu yeye kuchukiwa anavyodai.

Lakini ya ujumbe huo, uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti umeonyesha kuwa bondia huyo katika mapambano yake yaliopita alicheza na mabondia waliokuwa na rekodi yenye nzuri fofauti ya mpinzani huyo.

Januari 27, mwaka huu, Mwakinyo aliwania mkanda wa ubingwa huo kwa mara ya kwanza dhidi ya Elvis Ahorgah wa Ghana ambaye alimchapa kwa Technicak Knockout katika pambano lilofanyika Zanzibar

Mwakinyo alishinda pambano hilo mpizani wake akiwa na nyota moja na nusu kabla ya kupanda tena ulingoni Juni mosi, mwaka huu kupanda ulingoni kutetea mkanda wa ubingwa wake dhidi ya Patrick Allotey akiwa hadhi ya nyota moja na nusu kabla ya kutetea tena juzi kwa mara ya pili mkanda wake huo.

Ukiondoa pambano la Mwakinyo katika pambano hilo ambapo Tony Rashid alifanikiwa kumchapa kwa pointi  Twalib Tuwa katika pambano la raundi nane.

Lakini Joseph Maigwisa yeye amefanikiwa kumchapa kwa kwa Knockout ya raundi ya pili Ivan Magumba kutoka Uganda katika pambano la raundi kumi.