Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpira wa kikapu ulivyotoboa 2025

KIKAPU Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa mafunzo ya nje ya nchi, alisema makocha watatu; Denisi Lipiki, yeye Manyerere na Maureen Sizya, walishiriki mafunzo ya juu ya ukocha ya FIBA Level 2 nchini Uganda, huku nchini Hungary, Phineas Kahabi akishiriki mafunzo hayo.

KAMISHNA wa Makocha wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Robert Manyerere, amesema mwaka 2025 ulikuwa ni wa maendeleo ya mpira wa kikapu.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti kuhusiana na maendeleo ya mchezo huo kwa mwaka 2025, akianzia eneo la ukocha, alisema yalifanyika mafunzo ukocha ya madaraja tofauti yakiwamo ya awali na daraja la kwanza kitaifa, yaliyofanyika katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Arusha, Mbeya, Lindi, Tanga na Dar es Salaam.

Kwa upande wa mafunzo ya nje ya nchi, alisema makocha watatu; Denisi Lipiki, yeye Manyerere na Maureen Sizya, walishiriki mafunzo ya juu ya ukocha ya FIBA Level 2 nchini Uganda, huku nchini Hungary, Phineas Kahabi akishiriki mafunzo hayo.

KIKA 02

MASHINDANO

Kuhusiana na mchezo wa kikapu, amesema mafanikio ya mchezo huo yalionekana baada ya timu zetu kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Amesema kwa upande wa timu za taifa, timu ya taifa ya vijana wavulana na wasichana zilishiriki mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika kwa mafanikio makubwa.

Kwa upande wa wanawake, amesema timu ya Fox Divas na DB Lioness zilishiriki mashindano ya Africa Women Basketball League (AWBL) mjini Nairobi, Kenya.

Timu ya wanaume ya Dar City ilishiriki mashindano ya Road to BAL Elite 16 kwa mafanikio makubwa, hali iliyofanya ipate wild card ya kushiriki mashindano ya Africa Basketball League Machi 2026.

Timu nyingine ni Stein Warriors, ambayo alisema ilishiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (EABC) kwa mafanikio makubwa, hali iliyomfanya mchezaji wa timu hiyo, Sisco Ngaiza, kuchaguliwa kuwa mlinzi bora.

KIKA 01

UBORA WA LIGI

Amesema ligi za kikapu zilifanyika kwa ubora mkubwa baada ya kupata wadhamini, hali iliyozifanya ligi hizo ziwe za kuvutia.

Baadhi ya ligi zilizopata wadhamini ni pamoja na Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (NBL) na Ramadhani Cup.

Kwa mujibu wa Manyerere, Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), iliyodhaminiwa na BetPawa na kampuni ya simu ya Vodacom, ndiyo iliyokuwa bora zaidi.

Amesema wachezaji wa timu 32, kati ya hizo 16 za wanaume na 16 za wanawake, walinufaika na udhamini huo, hali iliyofanya ushindani kuongezeka.


TIMU 4 ZILIZOTISHA 2025

Timu za mpira wa kikapu za Dar City, Stein Warriors, JKT na Pazi, zilizoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam 2025, ndizo zilizoongoza kwa ubora.

Ubora wa timu hizo umetokana na mipango waliyoweka ya muda mrefu ya kuinua timu zao katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

KIKA 04

DAR CITY

Ubora wa timu hii umetokana zaidi na uwekezaji mkubwa, uliowawezesha kusajili wachezaji inaowahitaji pamoja na kocha kutoka nje ya nchi, hali iliyofanya iwe gumzo Afrika nzima.

Pamoja na kusajili wachezaji wa kimataifa, kiwango cha wachezaji wazawa kiliweza kuongezeka.

Mmoja wa wachezaji hao, Amin Mkosa, alisema uwepo wa wachezaji wa kimataifa katika timu yake umemfanya abadilike kwa kiasi kikubwa.

“Nimekuwa nikijifunza kwa wachezaji wa kigeni ninaocheza nao, hali iliyonifanya nifuate uchezaji wao,” alisema Mkosa.

KIKA 03

STEIN WARRIORS

Timu hiyo iliyopanda daraja mwaka jana na kushika nafasi ya tatu katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), iliweza kusajili nyota mbalimbali na kuwapa ajira.

Stein Warriors ilionyesha imejipanga vizuri, wachezaji wake wakifanya mazoezi kila asubuhi. Katika mazoezi hayo, wamekuwa wakirekodi na kuyatathmini.


JKT

Ubora wa timu hiyo umetokana na uwekezaji mkubwa kwenye nidhamu ya mazoezi. Pia imekuwa ikiwatumia wachezaji wake wazawa, hali iliyofanya ifanye vizuri katika mashindano yake.


PAZI

Ukongwe wa timu hiyo pamoja na mchango wa wachezaji wa zamani waliokuwa wakiisapoti timu hiyo, ulichangia timu hiyo kuwa bora mwaka 2025.

KIKA 05

VEINS BC, LEADERS BC ZAONGOZA LIGI

Timu za mpira wa kikapu za Veins BC na KR One zinaongoza katika msimamo wa Ligi ya Kikapu Daraja la Kwanza Mkoa wa Dar es Salaam.

Veins BC ambayo iko Kundi A inaongoza kwa pointi 13, ikifuatiwa na Leo Kings yenye pointi 13 pia.

Takwimu iliyotolewa na Kamati ya Ufundi na Mashindano imeonyesha uongozi wa Veins BC umetokana na tofauti ya pointi 86.

Pointi hizo zilipatikana baada ya Veins BC kufunga pointi 425 na kufungwa pointi 339, hivyo kupata tofauti ya pointi 86.

Timu nyingine katika kundi hilo ni Mlimani BC (10), Jogoo (9), Cavaliers BC (9), Kigamboni Heroes (9), Kigamboni Kings (9), Dar Kings (7), Service BC (6) na Game Time Squad (6).

Kwa upande wa Kundi B, timu inayoongoza ni Leaders BC kwa pointi 13, ikifuatiwa na Ukonga Kings (13), KR One (12), Magone (11), DB VTC (11), Mbezi Beach Spurs (9).