Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco wamekipata walichokitafuta, wamejivua nguo

PAZIA Pict


KUTOKA Rio de Janeiro hadi Paris kisha Tunisia, video zimesambaa zikionyesha mashabiki wa mpira wakishangilia video iliyokoswa na Brahim Diaz katika pambano la fainali ya Afcon 2025 dhidi ya Senegal. Mwishowe bingwa alikuwa Senegal dhidi ya Morocco na watu wakashangilia.


Kwa nini chuki hii dhidi ya Morocco? Nadhani walipanda mbegu. Timu nzuri kama ilivyo, watu wanaipenda Morocco. Waafrika wengi waliishangilia Morocco wakati ilipotinga nusu fainali ya Kombe la Dunia pale Qatar 2022 na kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufanya hivyo. Hata kama Wamorocco wenyewe hawajioni kama ni Waafrika.


Katika michuano hii iliyoisha wikiendi iliyopita Morocco wamejivua nguo wenyewe kutokana na mienendo yao ya kulazimisha kombe libakie nyumbani. Waamuzi walikuwa wanawalinda katika matukio ya 'hamsini kwa hamsini' dhidi ya wapinzani wao. Hakimi akimvuta adui jezi mwamuzi anapeta na hatoi kadi. Akivutwa yeye kadi ya njano lazima itoke.

PAZ 02

Mashabiki sio wajinga walikuwa wanaandika katika notisi kila ambacho kilikuwa kinaendelea. Matukio ya penalti yaliwachanganya na mwishowe yakawaumbua. Mechi tatu mfululizo dhidi ya Tanzania, Nigeria na Cameroon wapinzani walinyimwa penalti. Kitu cha kushangaza matukio hayo hayakwenda katika VAR. Ni afadhali waamuzi wangeenda kukataa penalti katika VAR.

Dhidi ya Tanzania, Idd Nado akiwa mbele kidogo ya mlinzi wa Morocco alisukumwa na kuanguka katika boksi. Sheria inasema kama ingekuwa bega kwa bega, basi ingekuwa sawa sio penalti, lakini Nado alikuwa kwa mbele. Mwamuzi aliyepania kuhakikisha Morocco haitolewi katika michuano alipeta haraka dhidi ya timu isiyo na nguvu Tanzania.

Dhidi ya Cameroon, Bryan Mbeumo alikwatuliwa katika boksi na mwamuzi hakutaka hata kwenda katika VAR. Dhidi ya Nigeria mchezaji mmoja wa Nigeria alivutwa katika boksi na mwamuzi hakutaka kwenda katika VAR. VAR huwa ina mawasiliano ya waamuzi waliopo chumbani na yule aliyepo uwanjani. Wote hawa walikuwa katika mifuko ya Wamorocco.

PAZ 01

Walifahamu kwamba kwa matukio yale kama mwamuzi angeitwa akatazame VAR, basi asilimia kubwa ya uamuzi wa namna hii huwa ni penalti. Katika utata wa penalti ya Idd Nado kocha wa Morocco alisikika akidai kwamba Nado alikuwa na kilo chache ndio maana alianguka kwa urahisi. Vipi kuvutwa kidogo kwa Brahim Diaz na beki wa Senegal kisha akaanguka kirahisi vile kulitokana na Diaz kuwa na kilo chache?

Inadaiwa kwamba yote haya yanatokana na umafia wa mtu anayeitwa Faouz Lekjaa. Mmorocco bilionea ambaye ni waziri wa Michezo wa Morocco na pia ni makamu wa rais wa CAF. Ndiye msaidizi namba moja wa Patrice Motsepe. Huwezi kujua waamuzi wa mechi za Morocco wanapata shinikizo gani kutoka juu. Huwezi kujua wanapewa hela kiasi gani au wanatishiwa kiasi gani kama Morocco haisogei mbele.

Mwanzoni katika mechi dhidi ya Tanzania, hata kama haitakiwi kwa mujibu wa sheria unahisi kwamba CAF wanataka mwenyeji aendelee kuwepo katika michuano ili michuano iwe na mvuto na viwanja viendelee kujaa.

PAZ 03

Hata wadhamini wa michuano wanataka timu kubwa kubwa ziendelee kuwepo katika michuano ili watu wafuatilie kwa karibu michuano yenyewe. Kwamba nani atafuatilia zaidi Tanzania kama ikiitoa Morocco? Hatuna mastaa wakubwa.

Lakini, wenzetu wenye maadili huwa wana mipaka yao. Ndio maana hawakutaka kulazimisha Qatar wasogee mbele katika fainali za Kombe la Dunia lililopita kwa sababu uwezo wao dhaifu ulijipambanua.

Hata katika michuano ya Euro na Copa America sio lazima mwenyeji asonge mbele kwa maslahi ya michuano. Ndio maana ni nadra sana kwa mwenyeji wa Kombe la Dunia kulitwaa. Ni nchi chache ambazo ziliwahi kuandaa Kombe la Dunia na kutwaa.

PAZ 04

Sisi tumejivua nguo kwa sababu imeonekana mpira wetu unaendeshwa kihuni tu. Senegal ndio wamekomesha ujinga huu kwa kuondoka uwanjani katika pambano la fainali la michuano hii mbele ya rais wa Fifa, Gianni Infantino na 'genge la wahuni' wa CAF.

Sio kwamba penalti ya Diaz haikuwa halali, lakini dakika chache kabla ya hapo mwamuzi, Jean-Jacques Ngambo Ndala alikuwa amewalinda Morocco kwa kupiga filimbi ya mapema katika maandalizi ya bao la Senegal.

Wachezaji wawili walikuwa wamevutana, mchezaji wa Morocco akateleza na kuacha fursa kwa mchezaji wa Senegal ambaye alipiga kichwa kilichokwenda kuzaa kashkash ya bao halali tu.

PAZ 05

Kwanini Ndala hakusubiri kila kitu kipite kisha aende katika VAR? Lilikuwa bao halali. Na hiki ndicho kiliwatia nyongo zaidi mastaa wa Senegal pamoja na kocha wao, Pape Thiaw.

Lakini kabla ya kuelekea katika mechi hii Senegal walikuwa wamejiandaa na jambo lenyewe wakiamini kwamba Afrika na watu ambao wanafuatilia michuano hii walikuwa nyuma yao. Ni kitu ambacho kiliiacha sura ya Ndala ikiwa imesawijika huku mfalme wa Morocco na watu wake wakiwa hawaamini.

Mpaka sasa hatujui kama kulikuwa na maelekezo kwa Diaz akose penalti hiyo kwa ajili ya kuiokoa fainali lakini ni wazi kwamba tukio zima lilihitimisha safari ya Morocco kujivua nguo katika michuano hii.

PAZ 06

Nani atawaamini tena Morocco kwamba hawana mipango nje ya uwanja? Sidhani kama ni suala la ubaguzi dhidi ya Waarabu kwa sababu Misri waliwahi kutwaa ubingwa huu mara tatu mfululizo na wote tulikubaliana kwamba akina Mohamed Aboutrika walikuwa hawashikiki.

Mataji yao yote yalikuwa ya halali na hakukuwa na makandokando kutoka kwa waamuzi licha ya kwamba wakati ule CAF ilikuwa inafanya shughuli zake nyingi nchini Misri.

Kinachoipa CAF na Morocco wakati mgumu ni uungwaji mkono wa kitendo cha Senegal kutoka nje ya uwanja na halaiki ya mashabiki waliokuwa wanafuatilia pambano hilo duniani kote.

PAZ 07

Kama tukio hilo lingelaaniwa na mashabiki au vyombo mbalimbali vya habari maisha ya Senegal yangekuwa magumu katika vikao vya CAF. Wamemsimamisha Pape Thiaw lakini nani anajali?

Afadhali kubwa kwa CAF na Morocco ni kwamba Senegal walitwaa ubingwa wenyewe. Vipi kama baada ya lile sekeseke Morocco wangetwaa ubingwa? Bado ingeonekana ni ubingwa bandia. Hata paredi lao lingelaaniwa na watu wa mpira.

Wangebaki peke hao tu katika sherehe hizo. Ni tofauti na pale walipomliza Cristiano Ronaldo Qatar na kutinga nusu fainali A kombe la dunia. Kila mmoja alikuwa nao.

Naamini Senegal wameukomboa mpira wa Afrika na unapaswa kurudi katika mstari. Wenzetu wameondoka huko miaka mingi ba mwenyeji anaishi katika michuano kama timu nyingine tu. Hata wachezaji wa Morocco wenyewe hawakustahili kuonekana wanabebwa angali kila mtu anafahamu kwamba wana uwezo mkubwa tu. Nani hajui uwezo wa kina Hakimi?

Walikuwa na mechi moja tu mbaya dhidi ya Tanzania, lakini nyingine wameupiga mwingi. Kutengenezewa mazingira kwamba wanabebwa kumechafua taswira zao ndani na nje ya Bara la Afrika. Sio ajabu wachezaji wa PSG walikuwa wanatamani Senegal ichukue ubingwa kwa kile kilichokuwa kinaendelea Morocco.

Waamuzi wetu wametuthibitishia kilekile ambacho kinaendelea katika Ligi Kuu Bara. Sio kwamba waamuzi wa Afrika hawaelewi sheria wala kanuni za mchezo wenyewe.

Hapana, wanachezesha mechi kwa ajili ya kuridhisha kundi la watu fulani. Inawezekana kwa kuhongwa au kuhofia hatima ya kazi yao. Waamuzi wote waliokuwa wanaibeba Morocco ni weusi. Kama ingekuwa hiyari yao unadhani wangeweza kuwapendekelea Waarabu?

Nini kilitokea baada ya Senegal kuondoka uwanjani? Waliporudi mwamuzi akaanza kuchezesha kwa haki. Nadhani aliambiwa kwamba misheni imeharibika na sasa arudi katika misingi ya kucheza mpira kwa haki. Huwa inatokea hata huku kwetu. Waamuzi wa hizi timu kubwa wanaanza kuzitendea haki timu ndogo pindi mkubwa akiwa amepata matokeo aliyoyahitaji.