Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mh, mume hata hajui mkewe anavaa nini!

Muktasari:

Hilo ni kosa kubwa mno. Haijalishi mke amekuzidi fedha au la, mwanamume unapaswa kuonyesha uanamume wako kwa kutoa huduma ndani ya ndoa.

Kuna wanaume wengi naweza kusema wanakosea sana…ameoa hajui mkewe anavaa nguo ananunuliwa na nani?

Hilo ni kosa kubwa mno. Haijalishi mke amekuzidi fedha au la, mwanamume unapaswa kuonyesha uanamume wako kwa kutoa huduma ndani ya ndoa.

Ni aibu unaitwa mume, halafu hujui mkeo anakulaje, anavaaje na huduma zingine muhimu za ndani.

Uanamume siyo kitandani tu ndugu yangu, uanamume ni kuonyesha kuitunza familia. Kama huna kitu, masuala haya yanapaswa kujadiliwa…ninachosema hapa ni kwamba mwanamume usionyeshe kama vile huhusiki katika kumlea mkeo au kuilea nyumba.

Unarudi umelewa unataka chakula kizuri, kinatoka wapi? Tafakari, je wewe ni kiongozi kweli kwenye nyumba au ni kiongozi wa hovyo? Jibu unalo.

Ambacho nataka kusema ni kwamba katika maisha penda kupata muda wa kujifunza ili upate mapya; Jambo moja ambalo ningependa kila mtu alizingatie katika siku ya leo na kuendelea ni kwamba ni jambo baya sana kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Aidha ni jambo baya zaidi kufanya mapenzi na watu wengi tofauti.

Kwa nini ni mbaya? Unapofanya mapenzi na watu wengi tofauti, siyo tu kwamba unahatarisha maisha kwa sababu labda unaweza kupata magonjwa kama Ukimwi na kadhalika, lakini pia kisaikolojia inamfanya yule ambaye anafanya hayo mapenzi, kupoteza kujiamini na kujiona kama ni mtu ambaye pengine asiwe tena na mwelekeo unaofaa katika mapenzi.

Kuna wasichana unashangaa anafanya ngono na wanaume zaidi ya 10, wapo pia wanaume wanafanya haya, ni ngumu sana mtu wa namna hii kumthamini mwenzi wake wanapoingia kwenye ndoa. Ukitaka maisha mazuri ya ndoa hakikisha unakuwa na staha katika mapenzi.

ZINGATIA HAYA

Jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aliye kwenye uhusiano ni kuwa, kama unataka kutosheka na penzi la mpenzi wako ni lazima uitosheleze kwanza akili yako.

Unapaswa kuamini kuwa, uliyenaye ni bora na kwamba kama ziko kasoro, lililo la msingi ni kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.

Anachanganya mambo ndiyo sababu hatosheki

Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.

Lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani, ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo kuliko sasa.

Nguvu za kijinsi

Kama hukuwa unafahamu; Ni kwamba idadi ya wanaume wasio na uwezo wa kufanya vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka.

Pia wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, kwamba kama siyo kuwa na uwezo mdogo, basi hukosa kabisa nguvu za kuendelea. Wengine wanaweza kuanza, lakini hawawezi kuendelea au wengine hata kuanza ni shida.

Idadi kubwa ya wanaume bado wanasumbuliwa na tatizo hili hasa kwa sababu ya kutokuwa tayari kuchukua hatua hasa za kuzingatia ushauri.

Ziko sababu nyingi za kukumbwa na hali hii, ikiwamo ulevi, kutofanya mazoezi, kujichua au utumiaji holela wa vyakula, hasa vyenye mafuta.

Hata hivyo kwa kuzingatia tiba sahihi ya vyakula kama nilivyoeleza, mtu anaweza kupona. Kwa mfano kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa kwa ustadi kama pilipili, parachichi na kadhalika vinaweza kumfanya mtu kuondokana na tatizo hilo.

Niliwahi kulizungumzia kwa kina jambo hilo na hata kutaja tiba zake, wengi waliozingatia wameondokana na tatizo hilo. Shida ni kwamba wengi hawachukui hatua, bali ni maarufu zaidi wa kulalamika.Uwe chanzo cha raha unazozitaka zitokee katika uhusiano au ndoa yako.

Dismas Lyassa ni mtaalamu wa uhusiano aliyesajiliwa na Serikali kupitia taasisi ya Global Source Watch, 0712183282 au 0755444555