Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MCHARO: Kutoka kuokota mipira ya gofu hadi elimu chuo kikuu

Muktasari:

  • Katika mahojiano yake na Mwanaspoti, Mcharo anasema safari yake ilianza akiwa na umri wa miaka 10, si kwa kucheza gofu, bali kwa kuokota mipira iliyopigwa na wachezaji na kupotelea kwenye vichaka au maji.

NYUMA ya mafanikio ya kila mtu kuna simulizi ya kusisimua na yenye funzo kwa wengine wanaojitafuta, ili wasikate tamaa na waamini siku yao ya kufanikiwa ipo njiani. Hivyo ndivyo anavyosimulia mchezaji wa gofu wa ridhaa, Ally Mcharo wa Klabu ya Gofu ya TPC, Moshi.

Katika mahojiano yake na Mwanaspoti, Mcharo anasema safari yake ilianza akiwa na umri wa miaka 10, si kwa kucheza gofu, bali kwa kuokota mipira iliyopigwa na wachezaji na kupotelea kwenye vichaka au maji.

“Nyumbani kwetu nilikozaliwa kulikuwa karibu na viwanja vya gofu vya TPC Moshi. Hivyo, mipira iliyokuwa inapotea baada ya kupigwa na wachezaji tulienda kuiokota kwenye nyasi ndefu au majini na kisha kuwauzia,” anasema Mcharo na kuongeza:

“Kuna wakati nilikuwa naokota mipira 20. Kipindi hicho mpira mmoja nilikuwa nauuza Sh1,000, hivyo nilikuwa napata kati ya Sh10,000 na 20,000. Hapo ndipo nilipoanza kushawishika kuupenda mchezo huo na kuamini unaweza kunipa maisha.”€

Anasema amezaliwa katika familia ya watoto watano. Ndugu zake, Sanura, Seif, Juma na Nashe, wote wanacheza gofu. Sababu kubwa iliyowavuta kwenye mchezo huo ni ukaribu wa viwanja vya gofu na nyumbani kwa wazazi wao.

“Pamoja na hilo, wazazi wetu hawajawahi kucheza gofu kabisa,” anasema.


ELIMU CHUO KIKUU

Mcharo si muumini mkubwa wa kuweka hadharani mafanikio aliyoyapata kupitia gofu, lakini ameshindwa kujizuia kuzungumzia elimu yake. Amesoma hadi ngazi ya shahada katika Chuo Kikuu cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT), ambako alihitimu taaluma ya ualimu, hatua ambayo anasema ilitokana na mchezo huo.

“Baada ya kumaliza darasa la saba nilianza kufanya kazi ya ukedi. Nilikuwa nambebea mabegi mzungu mmoja aliyeitwa John Sargent, ambaye alikuwa meneja wa TPC kwa miaka 10. Aliniambia napaswa kucheza gofu. Nilimwambia changamoto yangu ni vifaa, ndipo akaninunulia vifaa vya gharama. Alitaka niwe nacheza naye huku nikiendelea kumbebea vifaa vyake,” anasema na kuongeza:

“Jambo la msingi alilonisisitiza ni elimu. Aliniambia lazima niwe na fani nyingine ya kuniingizia kipato kwa sababu aliamini gofu pekee haliwezi kubadilisha maisha yangu. Alijitolea mfano yeye mwenyewe, licha ya kuwa mchezaji wa gofu pia alikuwa meneja. Baadaye akaondoka.

Wengine waliochangia kwa kiasi kikubwa mimi kufika chuo kwa msaada wa kifedha na ushauri ni Robert Baisaac na Jaffary Ally. Walinisisitiza umuhimu wa elimu ambayo ingenipa taaluma ya kunisaidia katika maisha yangu.â€


MKALI MWENYE HANDICAP 2+

Mcharo, mwenye handicap ya 2+, anasema kiwango hicho kinatokana na uwezo wa kupiga mipira chini ya 70, idadi ambayo haizidi par 72 ya viwanja vya gofu vinavyokubalika kimataifa.

“Changamoto iliyonifanya nisisonge mbele zaidi ni mchezaji unapofikia kiwango cha juu, lazima kuwe na hatua nyingine ya kupiga mbele, kama vile kuwa pro. Nimeona wachezaji kama watano waliandika barua za kuomba kuwa pro, lakini hadi sasa hawajajibiwa,” anasema na kuongeza:

“Pia, wachezaji wa kulipwa wanakosa mashindano ya muendelezo kutokana na kukosekana kwa uhakika wa udhamini wa mashindano ya mara kwa mara. Hiyo ikawa sababu ya mimi kutafuta ajira. Kwa sasa nafanya kazi katika kiwanda cha tumbaku kilichopo Chunya kama Agricultural Labour Practices Technician. Majukumu yangu makubwa ni kuhakikisha hakuna utumikishwaji wa watoto, kulinda haki za wafanyakazi, kusimamia kilimo cha kisasa na mambo mengineyo.”


SAFARI KATIKA GOFU

Anasema anakumbuka mambo mengi mazuri aliyopitia katika gofu, lakini anaamini akipata likizo ataendelea kucheza. Pia anaamini kama Mbeya kungekuwa na viwanja vya gofu, angejiunga na klabu za huko.

“Zamani kulikuwa na viwanja ambavyo sasa matumizi yake yamebadilika. Naamimi vikijengwa tena vitasaidia wakazi wa huku kuwa na afya njema na kuwajengea mtandao wa mahusiano na watu ambao wanaweza kubadilisha maisha yao kutoka hatua moja kwenda nyingine. Ikumbukwe kuwa gofu ni ajira kama ilivyo mpira wa miguu, ambapo karibu kila mkoa una viwanja vya mchezo huo,” anasema.

Mcharo anasema miongoni mwa mafanikio makubwa aliyowahi kuyapata ni kutwaa mataji ya PDF mwaka 2019, Lugalo Open, Arusha Open na Morogoro Open. Pia aliwahi kushika nafasi ya pili katika viwango vya Tanzania One mwaka 2015.

Mbali na gofu, Mcharo ni shabiki wa Yanga. Mchezaji anayemkubali zaidi ni kipa Djigui Diarra, nafasi aliyokuwa akiicheza alipokuwa shule ya msingi.

Lakini katika Kombe la Dunia la 2026 linaloendelea, nashabikia Ufaransa.