Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matumla anavyowaburuza vijana nje ya ulingoni

Matumla Pict

Muktasari:

  • Mara ya mwisho Matumla au Snakeboy kama alivyopenda kujiita alizichapa Agosti 2013, na kutoka sare na Maneno Oswald mjini Mororogo.

Licha ya kutopanda ulingoni kwa miaka 11 mfululizo, Rashid Matumla ameendelea kutajwa kama bondia bora wa muda wote chini, akiwaburuza nyota wanaofanya vizuri hivi sasa.

Mara ya mwisho Matumla au Snakeboy kama alivyopenda kujiita alizichapa Agosti 2013, na kutoka sare na Maneno Oswald mjini Mororogo.

Matumla anaufunga mwaka 2024 akiwa ndiye kinara wa muda wote Tanzania kwa mujibu wa Mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec).

umeendelea kumtaja bondia huyo wa uzani wa super welter kama bondia bora wa muda wote.

Matumla ambaye pambano lake la ngumi za kulipwa la kwanza alishinda kwa pointi mwaka 1993 dhidi ya Ali Ramadhan wakati huo akiwa kijana wa miaka 24.

Hadi anastaafu alipigana mapambano 72 na kushinda 49 (34 wa KO) amepigwa mara 19 (6 kwa KO) na kutoka sare mapambano manne.


Kilichombeba Matumla

Bingwa huyo wa zamani wa dunia, aliyekuwa akitumia zaidi mkono wa kulia (orthodox) ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na pointi alizowahi kuvuna enzi zake ambazo hakuna aliyezifikia hadi sasa.

bondia wa zamani, Ally Bakari (Champion) anasema kinchombeba Matumla ni rekodi yake na pointi alizovuna ambazo hazijafikiwa na bondia yoyote hadi sasa.

“Tangu amestaafu ni muda mrefu, hii inaonyesha wezo wake na rekodi zake na aina ya mapambano aliyocheza, haikuwa rahisi kwake kufikia rekodi hiyo, kuna cha kujifunza,” anasema.


Mwenyewe afunguka

Akizungumzia rekodi hiyo, Matumla amesema ni heshima aliyoiweka na mapambano aliyocheza wakati huo.

‘Hili ni funzo kwa vijana, vitu ambavyo nilifanya na kushinda, nakumbuka miaka ile nilishinda mapambano ya ubingwa wa dunia na mabara wa IBC na WBU (World boxing Union) anasema Matumla alipozungumza na gazeti hili jana.


20 bora ya muda wote hii hapa

Mbali na kinara Matumla, katika orodha ya Boxrec kwenye 20 bora, mabondia wanane pekee wanaozichapa hadi sasa ndiyo wameingia huku 12 walioingia kwenye 20 bora ni wa zamani.

Kinara wao ni Anthony Mathias aliyekamata nafasi ya tano, Ibrahim Class aliyekamata nafasi ya sita, Hassn Mwakinyo (namba tisa), Fadhil Majiha (nafasi ya 10), Nasibu Ramdhani (14), Juma Fundi  (15), Dulla Mbabe (19) na Ramadhani Shauri aliyehitimisha 20 bora.

Katika orodha hiyo, Rogers Mtagwa ni namba mbili na mdogo wa Matumla, Mbwana Matumla amehitimisha tatu bora ya muda wote ya Tanzania.

Wengine na nafasi zao kwenye mabano ni Joseph Marwa (4), Francis Miyeyusho (7), Francis Cheka (8), Hamisi Kimanga (11), Mambea Bakari  (12) na Bozon Haule (13).

Wengine ni Maneno Oswald (16), Thomas Mashali (sasa ni marehemu amekamata nafasi ya 17 ya ubora wa muda wote na Mohammed Matumla aliyekamata nafasi ya 18, bondia huyo alistaafishwa ngumi mwaka 2017 baada ya kupata ufa kwenye fuzu la kichwa.