Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GUY ROUX: Kocha aliyefundisha timu moja miaka 44, baba wa AJ Auxerre

KOCHA Pict
KOCHA Pict

Muktasari:

  •  Mmoja wa makocha wa aina hiyo ni Guy Roux, raia wa Ufaransa ambaye jina lake haliwezi kutajwa bila kuambatana na timu ya AJ Auxerre inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1).

KATIKA historia ya soka duniani majina ya makocha wakubwa huandikwa kutokana na  mataji waliyoshinda, timu walizopita na nyota waliowahi kuwanoa. Lakini ni wachache walioweza kutajwa kutokana na kujenga timu kutoka chini kabisa hadi kileleni na kuzitumikia kwa muda mrefu.

 Mmoja wa makocha wa aina hiyo ni Guy Roux, raia wa Ufaransa ambaye jina lake haliwezi kutajwa bila kuambatana na timu ya AJ Auxerre inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1).

Roux ni zaidi ya kocha. Ni kiongozi, mlezi, mbunifu, na mtu aliyeamini katika ndoto, wengine wakasema ndiye baba wa Auxerre kutokana na alivyojitolea kwa ajili ya timu hiyo.

Aliitumikia Auxerre kwa zaidi ya miaka 44, akiiongoza kutoka Daraja la Nne hadi kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutwaa mataji kadhaa ndani ya Ufaransa.

Roux alifanya hayo yote wakati timu ikiwa na bajeti ndogo na akiwekeza zaidi kwa wachezaji vijana.

Katika makala hii, tutaitazama safari ya kipekee ya Roux na AJ Auxerre yake, mikakati aliyotumia wakati timu haina fedha, mafanikio aliyopata, changamoto alizokumbana nazo na urithi mkubwa aliouacha si tu kwa Auxerre, bali kwa soka la dunia kwa ujumla.

KOCH 02

MWANZO WA SAFARI YA GUY ROUX

Guy Roux alizaliwa Oktoba 18, 1938 huko Colmar, Ufaransa. Alikulia katika familia ya kawaida, lakini akiwa kijana mdogo alionyesha mapenzi ya dhati kwa mchezo wa soka. Baada ya muda mfupi kama mchezaji akiwa Auxerre na klabu nyingine ndogo, aliomba kazi ya ukocha AJ Auxerre mwaka 1961 akiwa na umri wa miaka 23. Hapo ndipo historia ilipoanza kuandikwa.


KUJENGA TIMU TOKA CHINI

Wakati Roux anaanza kazi ya ukocha, AJ Auxerre ilikuwa timu inayoshiriki Ligi Daraja la Nne, isiyo na jina wala nguvu ya kifedha. Lakini kupitia maono, nidhamu na uvumilivu, alibadilisha kila kitu. Aliwekeza zaidi katika kukuza vipaji vya vijana badala ya kununua wachezaji wa bei ghali. Mfumo huo wa maendeleo ya vijana baadaye ulizaa wachezaji nyota kama Eric Cantona, Djibril Cisse, Basile Boli, Philippe Mexes na Laurent Blanc ambao wote waliuzwa kwa ofa nono kwenda timu zingine.

Roux aliamini katika msingi wa “kujenga badala ya kununua.” Alikuwa si kocha tu, bali mlezi, mwalimu na hata baba wa pili kwa vijana wa akademi ya Auxerre.

Chini ya uongozi wa Roux, Auxerre ilipanda kutoka Ligi Daraja la Nne hadi Ligue 1. Hii haikuwa kazi rahisi kwani ilichukua zaidi ya miaka 15, lakini  hakuwahi kuchoka hadi alipofanikisha hilo.

KOCH 01

ALIVYOJITOA

Hakuishia tu kuwa kocha wa Auxerre, bali kutokana na hali mbaya ya timu hiyo wakati huo, Roux alijitolea kufanya kazi za ziada ikiwa ni pamoja na kuwa mtunza uwanja wa kuchezea, mtunza vifaa, akawa katibu wa timu na alikuwa akihudhuria mikutano ya shirikisho. Vilevile alikuwa kiongozi wa msafara ambapo alihakikisha timu inasafiri na wachezaji kupata chakula bila ya shida yoyote.

Katika kuhakikisha timu inafanikiwa, Roux aliwasajili wachezaji kutoka mitaa ya karibu wengi wao wakiwa wakulima na wafanyakazi wa kawaida. Kwa kutumia wachezaji hao, Auxerre ilikuwa ilifanya vizuri kwani wachezaji hao walikuwa wakicheza kwa kujitoa zaidi kupambania timu  ya nyumbani licha ya kupewa pesa kiduchu.

Roux pia alikuwa mtu wa nidhamu kali, lakini mwenye moyo wa huruma. Aliwajali wachezaji kama familia yake. Alikuwa na ushawishi mkubwa si tu kwa wachezaji, bali hata kwa mashabiki, viongozi wa timu na jamii nzima ya Auxerre.

Kocha huyo alijulikana kwa maneno ya hekima, tabia ya unyenyekevu na usimamizi wa karibu katika kila eneo hata wakati mwingine alikuwa anakagua chakula wanachokula wachezaji wanapokuwa nyumbani.

KOCH 03

MATAJI

Kocha huyo alibeba ubingwa wa Ligue 1 (1995/96)

Mataji manne ya Coupe de France (1994, 1996, 2003 na 2005).

Ushiriki wa mara kwa mara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Uefa Cup (Europa League).

Ushindi UEFA Intertoto Cup (1997) .

Nusu fainali ya UEFA Cup 1992/93 waliyofungwa na Borussia Dortmund kupitia mikwaju ya penalti.

KOCH 04

KUSTAAFU NA URITHI

Baada ya miaka 44 ya ukocha wa Auxerre (1961–2005), Roux alistaafu. Aliondoka akiwa ameweka historia ya kuwa kocha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika timu moja Ulaya. Pia aliweka rekodi ya kuiongoza timu katika zaidi ya mechi 2,000.

Hata baada ya kustaafu aliendelea kuwa karibu na timu kama mshauri. Mafanikio yake yalimfanya kutunukiwa Tuzo ya Rais wa UEFA m 2000 kwa mchango wake mkubwa katika soka.

Ingawa timu ilipata changamoto kadhaa baada ya kuondoka kwake, lakini urithi wake bado unaishi. Mfumo wa maendeleo ya vijana unafanya kazi.

Kwa mashabiki wa soka wa Ufaransa, Auxerre ni zaidi ya timu bali alama ya kazi ya mtu mmoja aliyejitoa kwa moyo ambaye ni Roux.

KOCH 05

MAKOCHA WENGINE

Mbali ya Roux, kocha mwingine ambaye alidumu kwa muda mrefu katika timu moja ni Sir Alex Ferguson  aliyehudumu Manchester United kwa miaka 26 kuanzia 1986 hadi 2013, akifuatiwa na Arsene Wenger ambaye alidumu kwa miaka 21 na miezi saba kuanzia 1996 hadi 2018.