Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa walioingia, kutoka Ligi Kuu England dirisha dogo la usajili 2025

Usajili Pict

Muktasari:

  • Baada ya klabu kibao ikiwamo Barcelona na AC Milan kuonyesha dhamira ya kumnasa staa huyo wa England, Aston Villa ndiyo iliyofanikiwa kunasa saini yake kumwondoa kwenye tatizo la kuwekwa benchi na kocha Ruben Amorim huko Man United.

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la wachezaji la uhamisho wa majira ya baridi 2025 limefungwa rasmi na hakika klabu za Ligi Kuu England zilikuwa bize kwelikweli kuboresha vikosi ili kuwa na nguvu mpya ya kumalizia msimu huu kibabe.

Kasheshe kubwa lilikuwa kwa Marcus Rashford juu ya hatima yake kwenye kikosi cha Manchester United, ambapo kilichokuwa kikiulizwa hali ingekuwaje endapo kama angeendelea kubaki Old Trafford.

Baada ya klabu kibao ikiwamo Barcelona na AC Milan kuonyesha dhamira ya kumnasa staa huyo wa England, Aston Villa ndiyo iliyofanikiwa kunasa saini yake kumwondoa kwenye tatizo la kuwekwa benchi na kocha Ruben Amorim huko Man United.

Kwa maana hiyo, Rashford ataendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England baada ya kutua Aston Villa ambayo inaruhusu kumbeba jumla mwishoni mwa msimu kama itakuwa tayari kulipa kiasi cha pesa - Pauni 40 milioni.

Manchester City ilianza mwezi wa usajili kwa kumnasa staa wa Kiargentina, Claudio Echeverri ambaye alisajiliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu England, Januari mwaka jana, lakini alibaki River Plate kwa mwaka mzima kabla ya kutua Etihad dirisha hili.

Na hakika miamba hiyo ya Etihad ilikuwa bize kwelikweli kwenye usajili, ikiwanasa pia Abdukodir Khusanov, Omar Marmoush na Vitor Reis kwa ada ya jumla ya Pauni 150 milioni, huku Kyle Walker akitolewa kwa mkopo kwenda AC Milan. Nico Gonzalez ulikuwa usajili wa dakika za mwisho za Man City, ambapo dili lake lilikamilika kwenye dakika za mwisho kabisa za kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa juzi Jumatatu.

Tottenham yenyewe pia ilikuwa kazini kunasa nyota wapya kwenye kikosi hicho, ambapo ilimsajili Antonin Kinsky na kumjumuisha kwenye timu yao. Na kwenye dakika za mwisho kabisa kabla ya dirisha kufungwa, Spurs ilifanikiwa kumnasa staa wa Bayern Munich, Mathys Tel, baada ya mchezaji kubadili mawazo na kutaka kwenda kuitumikia timu hiyo baada ya awali kugoma. Man United na Arsenal nazo zilihitaji huduma yake.

Liverpool inashusha pumzi kwa sababu imenusurika kumpoteza beki wao matata kabisa, Trent Alexander-Arnold baada ya Real Madrid kuonyesha dhamira ya kumsajili, lakini kilichopo dili hilo limeshindwa kukamilika kwenye dirisha dogo, ikisubiriwa mwisho wa msimu ambapo mkataba wake utafika tamati. Hakuna mchezaji mpya aliyeingia kwenye dirisha hili la Anfield, lakini ilifungua milango kwa makinda wao kwenda kucheza timu nyingine kwa mkopo.

Arsenal na Chelsea nazo zilikuwa kimya sana kwenye ishu ya kunasa wachezaji wapya zaidi ya kuwafungulia milango ya kutokea kwenda kwingineko.

Huu hapa usajili wote uliofanywa na klabu za Ligi Kuu England kwenye dirisha dogo la majira ya baridi, ambalo lilifungwa usiku wa juzi Jumatatu...


Arsenal

Walioingia: Hakuna

Waliotoka: Josh Robinson (Wigan, imefichwa), Marquinhos (Cruzeiro, mkopo)


Aston Villa

Walioingia: Donyell Malen (Borussia Dortmund, Pauni 20milioni), Andres Garcia (Levante, Pauni 6milioni), Marcus Rashford (Aston Villa, mkopo), Marco Asensio (PSG, mkopo), Axel Disasi (Chelsea, mkopo)

Waliotoka: Lewis Dobbin (Norwich, mkopo), Jaden Philogene (Ipswich, Pauni 20milioni), Diego Carlos (Fenerbahce, Pauni 8.5milioni), Tommi O’Reilly (MK Dons, mkopo), Emi Buendia (Bayer Leverkusen, mkopo), Louie Barry (Hull, mkopo), Joe Gauci (Barnsley, mkopo), Jhon Duran (Al Nassr, Pauni 67milioni), Kosta Nedeljkovic (RB Leipzig, mkopo), Samuel Iling-Junior (Middlesbrough, mkopo), Sil Swinkels (Bristol Rovers, mkopo), Kadan Young (Royal Antwerp, mkopo)

US 01

Bournemouth

Walioingia: Matai Akinmboni (DC United, imefichwa), Kai Crampton (Chelsea, imefichwa), Julio Soler (Lanus, imefichwa), Zain Silcott-Duberry (Chelsea, imefichwa), Eli Junior Kroupi (Lorient, Pauni 10 milioni)

Waliotoka: Lewis Brown (Salisbury, mkopo), Finn Tonks (Farnborough, mkopo), Philip Billing (Napoli, mkopo), Max Aarons (Valencia, mkopo), Mark Travers (Middlesbrough, mkopo), Eli Junior Kroupi (Lorient, mkopo)


Brentford

Walioingia: Michael Kayode (Fiorentina, mkopo)

Waliotoka: Ashley Hay (Cheltenham, mkopo), Val Adedokun (Cheltenham, mkopo), Jayden Meghoma (Preston, mkopo), Tristan Crama (Millwall, imefichwa), Tony Yogane (Exeter, mkopo), Mads Roerslev (Wolfsburg, mkopo), Matt Cox (Crawley, mkopo), Ryan Trevitt (Exeter, mkopo)

US 02

Brighton

Walioingia: Diego Gomez (Inter Miami, Pauni 11 milioni), Eiran Cashin (Derby, Pauni 9 milioni), Stefanos Tzimas (Nurnberg, Pauni 20.8 milioni).

Waliotoka: Louis Flower (Gateshead, mkopo), Imari Samuels (Dundee United, imefichwa), Ben Jackson (Queens Park, mkopo), Jakub Moder (Feyenoord, Pauni 1.2 milioni), Julio Enciso (Ipswich, mkopo), Kamari Doyle (Crawley, mkopo), Evan Ferguson (West Ham, mkopo), Marcus Ifill (Bromley, imefichwa)


Chelsea

Walioingia: Hakuna

Waliotoka: Alex Matos (Oxford United, mkopo), Kai Crampton (Bournemouth, imefichwa), Zain Silcott-Duberry (Bournemouth, imefichwa), Max Merrick (Hampton & Richmond, mkopo), Jimmy-Jay Morgan (Gillingham, mkopo), Renato Veiga (Juventus, mkopo), Cesare Casadei (Torino, Pauni 12.5 milioni), Caleb Wiley (Watford, mkopo), Carney Chukwuemeka (Borussia Dortmund, mkopo), Ben Chilwell (Crystal Palace, mkopo), Harvey Vale (QPR, imefichwa), Zak Sturge (Millwall, mkopo), Axel Disasi (Aston Villa, mkopo)

US 03

Crystal Palace

Walioingia: Romain Esse (Millwall, Pauni 12 milioni), Ben Chilwell (Chelsea, mkopo)

Waliotoka: Chris Francis (Dagenham & Redbridge, mkopo), Jemiah Umolu (Port Vale, mkopo), Asher Agbinone (Gillingham, mkopo), Trevoh Chalobah (Chelsea, amerudishwa kutoka kwenye mkopo), Rob Holding (Crystal Palace, mkopo), Jeffrey Schlupp (Celtic, mkopo)


Everton

Walioingia: Carlos Alcaraz (Flamengo, mkopo)

Waliotoka: Charlie Whitaker (Notts County, bure), Stanley Mills (Oxford United, imefichwa), Harrison Armstrong (Derby, mkopo)

US 04

Fulham

Walioingia: Willian

Waliotoka: Conor McAvoy (Wealdstone, mkopo), Olly Sanderson (Harrogate, mkopo)


Ipswich Town

Walioingia: Ben Godfrey (Atalanta, mkopo), Jaden Philogene (Aston Villa, Pauni 20 milioni), Julio Enciso (Brighton, mkopo), Alex Palmer (WBA, Pauni 4 milioni)

Waliotoka: Harry Barbrook (Chelmsford, mkopo), Henry Gray (Braintree, mkopo), Ayyuba Jambang (Chatham, mkopo), Jokubas Mazionis (Woking, mkopo), George Edmundson (Middlesbrough, Pauni 600,000), Ali Al-Hamadi (Stoke, mkopo), Harry Clarke (Sheffield United, mkopo), Osman Foyo (Wimbledon, imefichwa)

US 05

Leicester City

Walioingia: Woyo Coulibaly (Parma, Pauni 1.9 milioni)

Waliotoka: Tom Cannon (Sheffield United, Pauni 10 milioni), Hamza Choudhury (Sheffield United, mkopo), Tom Wilson-Brown (Kilmarnock, mkopo), Arjan Raikhy (Tamworth, mkopo), Oliver Ewing (Buxton, mkopo)


Liverpool

Walioingia: Hakuna

Waliotoka: Rhys Williams (Morecambe, mkopo), Marcelo Pitaluga (Fluminense, imefichwa), Calvin Ramsay (Kilmarnock, mkopo), Tom Hill (Harrogate, imefichwa), Stefan Bajcetic (Las Palmas, mkopo)

US 10

Manchester City

Walioingia: Claudio Echeverri (River Plate, imefichwa), Abdukodir Khusanov (Lens, Pauni 33.8 milioni), Omar Marmoush (Eintracht Frankfurt, Pauni 59 milioni), Vitor Reis (Palmeiras, Pauni 29.5 milioni), Juma Bah (Valladolid, imefichwa), Nico Gonzalez (FC Porto, Pauni 50 milioni)

Waliotoka: Issa Kabore (Werder Bremen, mkopo), Josh Wilson-Esbrand (Stoke, mkopo), Juma Bah (Lens, mkopo), Kyle Walker (AC Milan, mkopo), Jacob Wright (Norwich City, mkopo)


Manchester United

Walioingia: Patrick Dorgu (Lecce, Pauni 30 milioni), Ayden Heaven (Arsenal, imefichwa)

Waliotoka: Ethan Ennis (Doncaster, mkopo), Ethan Williams (Cheltenham, mkopo), Antony (Real Betis, mkopo), Ethan Wheatley (Walsall, mkopo), Joe Hugill (Carlisle, mkopo), Jack Kingdon (Rochdale, mkopo), Marcus Rashford (Aston Villa, mkopo)


Newcastle United

Walioingia: Hakuna

Waliotoka: Isaac Hayden (Portsmouth, mkopo), Alex Murphy (Bolton, mkopo), Travis Hernes (Aalborg, mkopo), Charlie McArthur (Carlisle, mkopo), Jamie Miley (Hartlepool, imefichwa), Miguel Almiron (Atlanta United, Pauni 8 milioni), Lloyd Kelly (Juventus, mkopo)

US 06

Nottingham Forest

Walioingia: Wayne Hennessey (hana timu, ametemwa), Tyler Bindon (Reading, imefichwa)

Waliotoka: Aaron Donnelly (Dundee, imefichwa), Andrew Omobamidele (Strasbourg, mkopo), Esapa Osong (Cambridge, mkopo), Tyler Bindon (Reading, mkopo), Emmanuel Dennis (Blackburn, mkopo), James Ward-Prowse (West Ham, amerudishwa kutoka kwa mkopo), Fin Back (Wycombe, mkopo


Southampton

Walioingia: Welington (Sao Paulo, bure), Joachim Kayi Sanda (Valenciennes, imefichwa), Albert Gronbaek (Rennes, mkopo), Victor Udoh (Antwerp, imefichwa)

Waliotoka: Ronnie Edwards (QPR, mkopo), Will Armitage (Aldershot, mkopo), Ben Brereton Diaz (Sheffield United, mkopo), Maxwel Cornet (West Ham, amerudishwa kutoka kwenye mkopo), Shea Charles (Sheffield Wednesday, mkopo), Dom Ballard (Cambridge, mkopo), Gavin Bazunu (Standard Liege, mkopo)

US 07

Tottenham

Walioingia: Yan Min-hyeok (Gangwon FC, imefichwa), Antonin Kinsky (Slavia Prague, Pauni 12.5 milioni), Kevin Danso (Lens, mkopo), Mathys Tel (Bayern Munich, mkopo)

Waliotoka: Matthew Craig (Mansfield, mkopo), Alfie Dorrington (Aberdeen, mkopo), Luca Gunter (Wealdstone, mkopo), Yan Min-hyeok (QPR, mkopo), Will Lankshear (WBA, mkopo)

US 09

West Ham United

Walioingia: Evan Ferguson (Brighton, mkopo)

Waliotoka: Maxwel Cornet (Genoa, mkopo)


US 08

Wolves

Walioingia: Emmanuel Agbadou (Reims, Pauni 16.6 milioni), Nasser Djiga (Red Star Belgrade, Pauni 10 milioni), Marshall Munetsi (Reims, Pauni 16 milioni)

Waliotoka: Luke Cundle (Millwall, Pauni 1 milioni), Dexter Lembikisa (Barnsley, mkopo), Finn Ashworth (Port Vale, mkopo).