Masau ni fundi kotekote

Friday February 19 2021
MASAU PIC

KAMA vile ambavyo amekuwa akimudu kutupa maneno ya kuinadi Ruvu Shooting ndivyo anavyo anatakuwa hodari wa kuondoa ujinga kwa wanafunzi wake shuleni.

Masau ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam, amemwagiwa sifa zake huko wadau wanasema ni vyema kumpongeza na sio kusubiri wakati akiwa hayupo ndio tutambue mchango wake. Msemaji huyo ambaye hajawahi kushindwa kuikingia kifua Ruvu hata inapopoteza inaelezwa kuwa ni mwalimu mzuri mno wa masomo ya Hisabati na Sayansi ambayo alianza kuyafundisha tangu mwaka 1994. Alianza kazi hiyo akiwa na umri mdogo.

Advertisement