Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MABULA: Kuna Samatta, halafu Fei Toto

MABULA Pict

Muktasari:

  • Tanzania ni miongoni mwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa wachezaji wenye kipaji na mmoja wao ni Alphonce Mabula.

KATIKA ulimwengu wa soka la kisasa, vipaji vipya vinaibuka kila mara na wengine wanazidi kupambana kuhakikisha ndoto zao zinatimia.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa wachezaji wenye kipaji na mmoja wao ni Alphonce Mabula.

Nyota huyo kwa sasa anakipiga Shamakhi inayoshiriki Ligi Kuu ya Azerbaijan na zimepita siku chache tu tangu aongeze mkataba wa mwaka mmoja baada ya ule wa miezi sita kumalizika mwezi Juni.

Mabula alijiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Serbia alikokuwa na FK Spartak Subotica ya Ligi Kuu ya huko maarufu kama Serbian SuperLiga.

Amecheza mechi 17 na kufunga mabao matatu akisaidia chama hilo kumaliza nafasi ya saba kati ya 10 zinazoshiriki ligi hiyo.

“Tunashukuru tulifanikisha lengo la timu na kwangu pia kucheza na kuonyesha kiwango bora, ukimaliza msimu salama bila majeraha ni jambo la kumshukuru sana Mungu,” anasema Mabula.

Kiungo huyo fundi mwenye uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufanisi anaeleza hajakutana na changamoto kubwa nchini humo zaidi ya hali ya hewa.

“Baridi tu ndiyo changamoto kidogo ingawa sio kubwa kwa sababu nilishaishi sana nchi hizo wakati nacheza Serbia lakini tunapambana na kuhakikisha tunafanikisha lengo letu,” anasema.

Kiungo huyu  mwenye uwezo wa kucheza kwa ufanisi nafasi ya kati ameendelea kujizolea umaarufu akiwa na kikosi cha Shamakhi na kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Uwezo wake wa kuusoma mchezo, kupora mipira na kuanzisha mashambulizi ni miongoni mwa vitu vinavyombeba nyota huyo ambaye tangu amesajiliwa kwenye miezi michache ameingia kwenye mfumo na kuwa mchezaji muhimu.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na nyota huyo wa zamani wa Alliance ya Mwanza akieleza mambo mbalimbali ikiwemo maisha yake Azerbaijan.

MABU 01

MAISHA YA AZERBAIJAN

“Maisha ya Azberjain ni mazuri hali ya hewa ni baridi ingawa ni changamoto lakini wakati nacheza Serbia nilikutana nayo kwa hiyo nimeshaizoea kila kitu kipo sawa kabisa kwangu.”

“Tofauti na hilo pia nchi hiyo napata ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzangu kwa hiyo ukitoa Tanzania, nchi hiyo pia naona kama nyumbani.”


MSIMU WA KWANZA

Anasema huu ni msimu bora kwake kwani alicheza na kuingia kwenye kikosi hicho kilichosheheni nyota wakubwa.

“Ulikuwa msimu mzuri kwangu sababu nimefanya vizuri, nimefunga mabao muhimu kwa timu na kutoa  asisti, nimeisaidia timu yangu kufikia malengo tuliyojiweka msimu uliopita,” anasema na kuongeza

“Kiwango bora ndio kilikuwa kinaamua kubaki kwani kwenye mkataba nilisaini ulikuwa wa miezi sita wenye kipengele cha kuongeza mmoja kama nitafanya vizuri nashukuru Mungu nilifanikiwa na wakaniongezea mkataba,”

MABU 02

KUREJESHWA STARS

Mara ya mwisho kiungo huyo kuitumikia timu ya taifa ni mwaka 2021 kwenye mashindano ya vijana ya AFCON U-17.

Hivi karibuni amejumuishwa Taifa Stars ikiwa ni mara yake ya kwanza kwa timu kubwa.

“Najisikia vizuri kurudi Taifa Stars, kila mchezaji anatamani kuitumikia timu yake ya taifa, kwa hiyo ni jambo jema kwangu na naamini itaniongezea kitu kwenye CV yangu,” anasema.

Alipoulizwa amejipangaje kukabiliana na ushindani eneo la kiungo ambalo lina nyota kama Himid Mao, Novatus Miroshi, Adolf Mtasingwa, Yusuph Kagoma na Mudathir Yahya ambao wamekuwa wakicheza anasema;

“Suala la nani apate nafasi  hilo ni la mwalimu, mimi jukumu langu kubwa ni kufanya mazoezi kwa bidii ninapopata nafasi niipeperushe vizuri bendera ya nchi yangu.”


OFA NONO

Anaeleza sababu ya kuondoka Serbia ambayo ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kisoka na kujiunga na Sgamakhi ni pamoja na ofa nono aliyoweka.

“Ofa yao ilikuwa juu zaidi na nzuri zaidi kwangu, ilinivutia pia ligi ya Azberjain ni kubwa ina wachezaji wengi wenye uzoefu waliotoka ligi kubwa tano za Ulaya, Bundesliga, Serie A, Laliga na nyinginezo,”

“Azerbaijan ni miongoni mwa ligi zenye ushindani sana ukifuatilia mpira au ukiwa unaangalia mechi utajua ni nini ninachozungumza, fuatilia profile za wachezaji wanaocheza ligi hiyo kwa hiyo pia hawako mbali.”

MABU 03

ALIFIKAJE ULAYA?

Mabula alicheza msimu mmoja tu Ligi Kuu Bara akiwa na Alliance wakati ule haijashuka daraja na hapa anaeleza.

“Nilifanya vizuri AFCON U-17  tuliocheza Tanzania menejimenti yangu ya Sama Player Management ilinitafutia trial Serbia ndipo nikaenda kufanya trial nakupita ndipo mwanzo wa maisha yangu ya soka yalipoendelea mpaka leo.”

“Lakini timu ya taifa waliniona baada ya kufanya vizuri nikiwa kwenye akademi ya Alliance ya Mwanza, nimekulia pale, nilibahatika kupata nafasi timu ya taifa chini ya miaka 15 nikaendelea kukua hadi chini ya miaka 17.”€

“Nashukuru Mungu nilikuwa sehemu ya wachezaji ambao walichaguliwa kwa ajili ya Afcon 2019 chini ya miaka 17 mashindano yaliyofanyikia nyumbani Tanzania baada ya apo nilipandishwa timu ya wakubwa Alliance msimu ule ilikuwa ligi kuu nikacheza ligi kuu.”

Baada ya hapo aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 20 iliyoenda kucheza Afcon Maurtania ndipo alipokutana na ajenti ambaye alimsaidia kupata nafasi Serbia.

“Niliskautiwa na meneja wangu wa saivi anaenisimamia Berna Erasmus ambaye yupo Ubeligiji. Akanitafutia timu Serbia nikaenda kufanya majaribio ambayo yalikuwa ya wiki moja, walinipitisha na nilikuwa tayari na miaka 18 nikasaini mkataba wangu wa kwanza kama mchezaji wa kulipwa katika timu yangu ya Spartak Subotica,” anasema.

MABU 05

AMTAJA SAMATTA

Anasema mafanikio yake yamechangiwa na nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta ambaye amekuwa mtu muhimu kwake kufanya vizuri.

“Unajua Samatta amefanya mengi, kaweka historia ya nchi yetu kuna mchezaji ukimtajia natoka Tanzania anaweza asipajue lakini ukimtajia Samatta anamfahamu kwa sababu ya rekodi alizoziweka Ulaya,” anasema na kuongeza:

“Kwangu amekuwa akinipa ushauri na ‘kunipush’ nipambane, ananiambia bado umri wako mdogo hiki ndio kipindi cha kutengeneza maisha yako ya soka kwa hiyo ni mtu ninaemuangalia sana natamani nifikie yale aliyoyafanya au zaidi ya hapo,” anasema ambaye kwa sasa yuko likizo nchini.


KUHUSU SIMBA, YANGA

Alipoulizwa kama ikitokea Simba na Yanga kumfuata na kuhitaji huduma yake alisema kwa sasa anatafuta maisha na pesa nje ya nchi.

“Kwa sasa malengo yangu ni kucheza soka la kulipwa nje hususani Ulaya na natamani nisaidie wenzangu hapo baadae kwa sababu Tanzania kuna vipaji wengi.”

MABU 04

FEITOTO HATARI

Anamtaja Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto’ ndiye mchezaji aliyemkosha msimu huu kutokana na muendelezo bora aliouonyesha.

“Nafuatilia Ligi Kuu kwa sababu kuna washkaji zangu wanacheza, kuna viungo wengi wamepambana wazawa lakini Feitoto amepambana sana msimu huu na amekuwa na muendelezo.”


ALIKOPITA

2021/22 Alliance FC

2022/23 FK Spartak Subotica (Serbia)

2023/24 RFK Novi Sad (Kwa mkopo)

2024/25 Shamakhi

Baadhi ya picha alizoposti Rima zinamuonyesha akiwa dimba la Allianz Arena ilipopigwa fainali hiyo, huku nyingine zikionyesha wachezaji wakisherehekea kisha akaandika ‘wikiendi ya mabingwa’. Bila shaka atafanya hivyo tena pindi Dembele akishinda Ballon d’Or 2025 au wakati ujao.