Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kulikuwa na Cameroon ya Eto'o, halafu kuna hii kichekesho

PAZIA Pict


NANI alisema Simba hawezi kuzaa paka? Nilikuwa natazama Cameroon wakifungwa na DR Congo juzi pale Morocco. Ni huzuni. Wale Simba Wasioshindika ‘The Idomitable Lions’ sio wale tena. Kuna wakati taifa linashuka na kufilisika.


Nyakati zimekwenda wapi? Leo Cameroon wa kufungwa na Congo katika pambano muhimu la ‘nusu fainali’ ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia? Imenikumbusha mambo mengi. Imenikumbusha namna ambavyo kuna tatizo kubwa mahala katika soka lao.


Cameroon lilikuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kutinga robo za fainali za michuano ya Kombe la Dunia pale Italia mwaka 1990. Wazungu walipigwa na butwaa wakati Francois Omam-Biyik aliporuka juu na kufunga bao zuri la kichwa la ushindi dhidi ya mabingwa watetezi Argentina waliokuwa na Diego Maradona ndani yake.

Kikosi kile kilikuwa na mafundi. Kina Emmanuel Kunde, Biyik mwenyewe, Kana Bikiy, Cyrille Makanaky, Steven Tataw, Louis Paul Mfede na mafundi wengine lukuki. Waingereza ndio waliokomesha safari yao ya kuisaka nusu fainali ya michuano hiyo.

PAZ 01

Leo Cameroon wanashindwa kumfunga DR Congo kwa ajili ya kusaka tiketi ya Kombe la Dunia na hawatakuwepo Marekani, Canada wala Mexico. Kama wangefungwa na Morocco au Algeria pengine tungeweza kuwasamehe, lakini kufungwa na kina Fiston Mayele katika mechi ambayo timu zote zilionyesha kiwango sawa inaonyesha wazi kuna shida mahala pale Cameroon.

Baadaye wakati dunia ya mpira ikibadilika Cameroon wakatutengenezea kikosi kingine cha masela kikiongozwa na Samuel Eto'o. Kulikuwa na mafundi haswa. Kina Marc-vivie Foe, Laurent Etame Mayer, Rigobert Song, Idriss Kameni, Geremi Njitap, Pierre Njanka na wengineo.

Wazungu walitishika na ubora wao uwanjani, pia maumbo yao. Leo Cameroon imetolewa na DR Congo na haitakwenda Kombe la Dunia. Sababu ni rahisi tu, wana wachezaji wa kawaida tu ambao hawana hata hadhi ya kucheza timu kubwa Ulaya.

PAZ 02

Wakati ule Wacameroon wenyewe walikuwa wanacheza katika timu kubwa za Ulaya. Samuel Eto'o alikuwa anacheza Barcelona. Mayer alikuwa Arsenal, Njitap alikuwa Real Madrid. Song alikuwa Liverpool. Foe alikuwa miongoni mwa viungo bora wa Ligi Kuu England akicheza katika klabu za West Ham na Manchester City katika nyakati tofauti.

Leo kuna mchezaji gani wa Cameroon anaweza kucheza Real Madrid, Barcelona, Arsenal au Liverpool? Wana Bryan Mbeumo tu ambaye ameamua kucheza Cameroon kwa sababu asingeweza kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa nchi ambayo amezaliwa.

Vinginevyo kabla ya Mbeumo staa wao alikuwa kipa, Andre Onana ambaye awali alikuwa Manchester United pia, lakini baadaye ameangukia katika timu ya Trabzonspor ya Uturuki baada ya kufanya makosa mengi katika lango la Manchester United.

PAZ 04

Sijui ni kitu gani kimetokea nchini kwao, lakini ukweli ni taifa lao limeanguka. Zamani ambao wangeweza kuwasumbua Cameroon walikuwa Nigeria tu. Hata mataifa ya Afrika Kaskazini yalikuwa hayauwezi muziki wa Simba hawa. Leo wanafungwa na DR Congo.

Kule kwao kuna shutuma kubwa kwa Rais wa soka wa nchi hiyo, Samuel Eto'o. Kwamba analiendesha Shirikisho la Soka la nchi hiyo ovyo ovyo. Hata hivyo, kitu hiki ni tofauti na namna ambavyo nafahamu mastaa wa zamani wa Cameroon walikotokea.

Cameroon kama ilivyo kwa mastaa wengi wa Afrika Magharibi wachezaji wao huwa wanajikuza wenyewe na kisha kutokomea Ulaya. Hawana mifumo mizuri rasmi kama ilivyo kwa wachezaji wa Ulaya bali wachezaji wao utokomea Ulaya kivyao na kisha kupata mafanikio makubwa halafu wanarudi nyumbani kusaidia taifa.

PAZ 05

Cameroon haitegemei wachezaji wa ligi ya ndani. Wachezaji wanazamia Ulaya na kisha kurudi nyumbani kuliwakilisha taifa. Mfano kipa wao Onana ni mchezaji aliyepelekwa Ulaya na Etoo katika kambi ya timu ya vijana ya Barcelona.

Hatujui ni kwa nini ubora wa wachezaji wanaozamia sasa hivi Ulaya umepungua. Inawezekana wameingia katika kilio cha kila kona ya dunia, vipaji vimepungua. Lakini kwa nini isiwe kwa wengine pia pale Afrika Magharibi? Cameroon wamekwenda chini zaidi.

Kitu kingine cha kukumbuka ni ukweli, wakati mwingine tusiwalaumu sana wachezaji wenye asili ya Afrika wanaogoma kuja kucheza nyumbani. Mfano mzuri ni Cameroon yenyewe na Kylian Mbappe ambaye baba yake ametoka Cameroon.

Kama Mbappe angekuwa amechagua kucheza Cameroon ina maana sasa hivi angekuwa amekosa safari ya kucheza Kombe la Dunia mwakani kule Marekani, Canada na Mexico. Ni wazi Cameroon ingekuwa imempotezea muda.

PAZ 03

Wachezaji mahiri huwa wanatumia michuano hii pia kwa ajili ya kusaka tuzo binafsi kama ile ya Mwanasoka Bora wa Dunia. Vipi kama Mbappe angechagua kucheza katika kikosi cha Cameroon? Labda ndio maana huwa tunasubiri wale wasio na ubora wa kucheza katika mataifa makubwa waachwe kwanza katika vikosi vya mataifa hayo kisha wanakimbilia huku.

Kama Bukayo Saka angeamua kuchezea Nigeria badala ya England ni wazi nafasi yake ya kutamba katika soka la kimataifa ingekuwa ndogo. Nigeria ya leo inamtegemea Victor Osimhen tu pale mbele. Zamani enzi za kina Jay Jay Okocha ilikuwa na wachezaji tegemeo.

Tukirudi kwa Cameroon ukweli ni sasa sio Simba wasioshindikana tena. Wana wachezaji wengi wa kawaida ambao wangeweza pia kupata wakati mgumu kama wangecheza na Taifa Stars au Harambee Stars. Nyakati zimepita ambapo tuliwaogopa kama ukoma kina Samuel Eto'o lakini kwa sasa unaweza kucheza na Cameroon katika uwanja wowote wa soka duniani.