Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kimwaga: Lile bao la Yanga nyie acheni tu!

UNALIKUMBUKA lile pambano la Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Azam FC iliyopigwa Septemba 22, 2013 na Vijana wa Jangwani kubutuliwa mabao 3-2?

Yanga ilipasuka kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa (sasa Benjamin Mkapa) na bao la ushindi likiwekwa kimiani na mchezaji chipukizi kwa wakati huo, Joseph Kimwaga kwa shuti kali la mwana ukome.

Bao hilo lilimpa heshima kubwa, Kimwaga aliyekuwa amepandishwa kutoka timu ya vijana na Kocha Stewart Hall na mashabiki walimtabiria kufika mbali, lakini mambo yakaenda kinyume.

Mwanaspoti liliamua kumsaka mchezaji huyo ambaye amesahaulika machoni na masikioni mwa mashabiki kutokana na kuwa kimya sana na yeye kufunguka kila kitu juu ya bao hilo lilivyomheshimisha na mikasa yake iliyomfanya apotee kwa muda mrefu uwanjani.

Kimwaga aliyefanana kiuchezaji na muonekano wake na Sadio Mane na Simon Msuva (kiuchezaji), amelezea safari ya maisha yake ya soka, iliyojaa kicheko na huzuni zilizomuweka nje kwa muda, akisubiri mambo yakae sawa ili aendelee na kazi zake. Ebu endelea naye...!


KWA NINI YUPO NJE

Anajibu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili Polisi Tanzania msimu wa 2020/21 hakuweza kuitumikia timu hiyo, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake kuzieleza.

“Ikanitoa kwa mkopo kwenda Kitayosce ya Championship ambako nilicheza miezi sita, kisha nikaa nyumbani, ishu hii ni nzito na sina sababu ya kuiweka wazi,” anasema.



ANAFANYA NINI KWA SASA

Kimwaga kwa sasa yupo chini ya menejimenti inayojulikana kama Tanzania Empowerment, ambayo ina vijana wengi wanaoelimishwa namna ya kuishi katika jamii na kutimiza ndoto zao.

“Muda ambao nipo nje ya uwanja, nipo na vijana wenzangu tunashikamana na jamii kujenga taifa kwa nyanja mbalimbali, ingawa si kitu rahisi mchezaji kukaa bila kucheza, inahitaji nidhamu ya hali ya juu,” anasema.

Anaulizwa tukutarajie lini utarejea dimbani tena? Anajibu kilichomuweka nje kinaelekea kupata mwafaka hivyo siyo muda mrefu atarudi kazini.

“Kuna watu wamenipigania nisiondoke kwenye ramani ya soka ambao ni Pascal Fumbuka na Hemed Mtumbuka, hakika nitarejea kwa nguvu,”anasema.

Mbali na hilo, anasema kazi inayompatia kipato nje na soka amejikita kwenye kilimo cha biashara anachokifanya mkoani Tanga, analima mahindi,mpunga, karanga na mihogo.


BAADA YA KUIFUNGA YANGA

Anasema alipandishwa kutoka Azam B siku moja kabla ya kucheza dhidi ya Yanga msimu wa 2013/14, msimu ambao ulikuwa wa mafanikio kwake.

“Stewart Hall hakupenda nicheze ‘gemu’ hiyo, nakumbuka kocha msaidizi, Kalimangonga Ongala alitumiwa ujumbe na mabosi wa Azam ili niingie kabla ya mchezo kumalizika,” anasema Kimwaga na kuongeza;

“Niliingia dakika ya 75 nikafunga bao la ushindi lililofanya Azam FC tushinde mabao 3-2 dhidi ya Yanga na ndio mwaka tuliochukua ubingwa.

Anasema kocha Hall hakuwaamini vijana, hivyo hakumhitaji katika programu zake, ndipo Zacharia Hans Poppe (marehemu) akamchukua kwa mkopo kwenda Simba, akacheza miezi sita kisha akarejea Azam FC.

“Tulipandishwa vijana watatu, mimi Farid Mussa na Ray Ngungila sababu tulicheza kwa kiwango kikubwa mechi ya kirafiki dhidi ya Villa Squad ambapo tulishinda 3-1 mimi nilifunga mabao mawili,” anasema Kimwaga na kuongeza;

“Baada ya kumaliza mkopo wa miezi sita Simba, nikarejeshwa baada ya kocha Hall kuondoka, ila kwa bahati mbaya zikiwa zimebakia mechi chache kufunga msimu niliumia dhidi ya Kagera Sugar hadi nilikwenda kutibiwa Afrika Kusini.

Anasema kutokana na majeraha hayo yalimuweka nje kwa msimu mzima, lakini baadae akarejea kazini tena.

Anasema makocha ambao walimtia moyo na kuamini katika kipaji chake ni Ibrahim Shikanda na Ongala, waliomtaka apambane bila kuangalia vikwazo katika kazi yake.


MAISHA NDANI YA AZAM

Anasema tangu alipochukuliwa kikosi B cha Azam FC akitokea timu ya Copa Cocacola ya Kindoni 2010/11, iliyomkuza kwenye misingi ya soka, ndio inayomsaidia hadi sasa.

“Azam FC imehusika kwa asilimia kubwa kukionyesha kipaji changu kwa Watanzania, pia ilinitibu kwa hali na mali nje na hapo huenda nisingekuwepo kwenye soka hadi sasa,’ anasema.


MANE, MSUVA

Kimwaga amekuwa akifananishwa na winga wa Liverpool Sadio Mane na Simon Msuva kwa namna anavyocheza na analiezea suala hilo kuwa;

“Msuva nafanana naye vitu vingi ikiwemo aina ya uchezaji na kasi na namuona kama kioo cha jamii, huyo Sadio Mane nawaachia mashabiki wanachonifananisha naye,”anasema.


MAHUSIANO YANAZINGUA

Anasema baada ya kuonyesha kiwango cha juu kwenye michuano ya Copa Cocacola akiwa na timu ya Kinondoni 2010/11 kuna mrembo alipenda kazi yake hadi akamuomba aingie naye kwenye mahusiano.

“Huyo binti alikuwa mdogo wake na rafiki yangu alikuwa anacheza Simba B, alimwambia kaka yake kwamba ananipenda, nikaenda kukutana naye, nakajikuta nampenda zaidi, lakini kilichokuja kutokea baadae ni maumivu kwangu,” anasema na kuongeza;

“Kama unavyojua maisha yetu ya mpira hayana makazi maalumu yanamhitaji mwanamke mvumilivu sana, najua alichoka ngoja ngoja zangu, akaniambia naolewa na akanitumia picha za ndoa, saizi namwita dada.


FARID, TSHABALALA WANAMTAKA AOE

Anasema marafiki zake ambao wamekuwa pamoja Farid Mussa (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wamemtaka kwa sasa aoe.

“Marafiki hao kwa sasa wananikomalia niowe, maana wenzangu wameishafanya hivyo, namuomba Mungu nipate mke sahihi, kulingana na kazi zangu hizi,” anasema.