Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenedy Ayoo na safari ya mikasa hadi Russia kuzichapa

Ayoo Pict

Muktasari:

  • Ayoo alimchapa Ismat Guliyev wa Azerbaijan katika pambano lililofanyika Desemba 13, mwaka huu jijini Moscow, Russia ambapo siku mbili tu baada ya pambano zikaenea taarifa za kukwama kwa Mtanzania huyo.

WIKI iliyopita katika tasnia ya mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kulitokea mshtuko baada ya kuenea taarifa za bondia Kenedy Ayoo kukwama nchini Russia baada ya kupata ushindi wa pointi aliopata.

Ayoo alimchapa Ismat Guliyev wa Azerbaijan katika pambano lililofanyika Desemba 13, mwaka huu jijini Moscow, Russia ambapo siku mbili tu baada ya pambano zikaenea taarifa za kukwama kwa Mtanzania huyo.

Bondia huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani wa Mara, ameweka rekodi yake ya ushindi katika pambano lake kwanza kucheza nje ya mipaka ya Tanzania.

Ayoo ana rekodi ya kucheza mapambano manane, ameshinda sita kati ya hayo mawili kwa Knockout huku akipigwa mawili yote ni kwa Knockout huku akiwa bondia wa tano katika mabondia 44 uzani wa middle. Duniani anashika nafasi ya 310 kati ya mabondia 1879 kwa uzito huo.

YO 04

Kutokana na sakata la bondia huyo kuvuma na kupelekea kuwepo kwa taarifa nyingi, Mwanaspoti limeingia mzigoni na kumtafuta bondia huyo ili kujua ukweli wa kilichotokea katika safari yake ya Urusi.

Ayoo ni baba wa familia ya watoto wawili, wakike na wakiume huku akiwa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni mmoja ya ulinzi katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.

Bondia huyo, ameanza kueleza namna alivyopewa pambano hilo na wakala aliyemtambulisha kwa jina la Azalinho, Novemba 27, mwaka huu ambayo anakiri aliikubali kutokana kufanya mazoezi muda mwingi bila ya kuwa na uhakika wa kuweza kupata pambano kwa mwaka huu.

"Ukweli ofa ya pambano la Urusi (Russia) nimeipata Novemba 27, alinitafuta wakala mmoja ambao kawaida wanaitwa 'matchmaker', jina lake Azalinho kwamba kuna ofa ya pambano la raundi sita Russia niliambiwa ni pambano la kupigana siyo kuachia.

YO 01

"Binafsi nilikubali kwa sababu kawaida nimekuwa mtu wa kufanya mazoezi kila siku na nikaona siyo sawa kutoikubali ikiwa sina uhakika wa kupanda ulingoni tena kwa mwaka huu lakini nilijiona nipo fiti naweza kwenda kupigana.

"Wakala akanitumia mkataba ninao kwenye simu kabla ya kuonana naye kwa ajili ya kusaini pamoja na kuweka sawa mambo mengine ya vibari.

"Ikafika muda wa kwenda ubalozini kuomba viza ya kuingia Urusi, nilienda na wakala mwenyewe pamoja na mtu mwengine ambaye ndiyo wakala alitaka nifuatane naye kwenye safari ya Urusi.

"Sasa matatizo nadhani yalianzia hapo kwa sababu yule jamaa hakuchukua paspoti yake badala yake alikuwa nayo kwenye simu, maofisa wa ubalozi wakamwambia haiwekani hadi ailete.

"Yule rafiki yake wakala, paspoti yake ilikuwa ameiacha Tanga tukakubaliana aitume kwenye basi siku ambayo nafuata ya kwangu na yeye agongewe kisha tutoke nazo pamoja basi ikawa hivyo.

"Lakini siku ambayo naenda yule jamaa hakuweza kutokea yeye wala paspoti yake kwa sababu wakati inasafirishwa kuja Dar kutoka Tanga, basi lilipata shida ikabidi mizigo yote irudishwe Tanga na yeye bahasha aliyokuwa amewekewa haikuwa imeandikwa namba ya simu.

"Sasa kutokana na hivyo ikishindikana yeye kuweza kuipata kwa wakati, viza nikawa nimepata peke yangu, sina mtu wa kuweza kufuatana naye kwenda Urusi, wakala akaniambia niende jamaa watanipokea vizuri bila shida.

"Lakini wakati huo Mzee Emmanuel Mlundwa alikuwa na yeye safari ya kwenda Urusi, alikuwa anampeleka Goodluck Mrema nikamuomba tufuatane, kweli tulifuatana na hata safari ya kwenda Uwanja wa ndege ilianzia nyumbani kwake Keko.

YO 02

"Tuliondoka wote hadi Moscow, Urusi lakini mambo yalibadilika baada ya kushuka na kufika kwenye ukaguzi, mzee Mlundwa na bondia aliyekwenda naye wakafanikiwa kuvuka kwenye ukaguzi hivyo walivyotoka nje wakaondoka na wenyeji wao.

"Mimi kwanza nilizuiwa, nilikaa kwa masaa siyo chini ya mawili, nafikiri kwa sababu ilikuwa safari yangu ya kwanza lakini baadaye nikafanikiwa kutoka yaani kuruhusiwa kuingia katika nchi ya Urusi.

"Lakini hadi natoka ndani ya uwanja, sioni mwenyeji wangu aliyekuja kunipokea ikabidi nimpigie wakala wangu ambaye alikuwa ameenda Dubai na mabondia wengine.

"Wakala wangu akaongea na promota wa Urusi ambaye yeye pia nikapewa namba zake, niliwasiliana naye, akaniambia baada ya masaa mawili atafika kunichukua ingawa baadaye aniambia amenitumia usafiri texi ambayo itanipeleka hotelini.

"Wakati nasubiria usafiri nikaunganishwa na mtu mwengine, nilivyomuuliza wakala akaniambia wote wa moja basi nikabaki kusubiri usafiri wa kwenda hotelini.

"Baada ya niliambiwa kwamba gari imefika kunichukua na shida nyengine ambayo ilikuwa kubwa Urusi wanatumia lugha yao, hawaongei kingereza, nikauliza kwa madereva wengine kwa kuwaonyesha namba ya gari hadi nikaipata.

"Gari ikanichukua hadi hotelini, nafika hotelini jamaa akawa amenishusha kisha akaondoka zake, ikabidi niulize kwa watu ambao walikuwa na 'Min Super Market'  bahati mbaya nao wanaongea kirusi kabla ya kupata mtu mwengine aliyekuwa anajua kingereza.

"Kiukweli alinisaidia nikafika hadi mapokezi baada ya kuonyesha passport yangu, wakanipokea na kunipa chumba, nikaomba huda ya mtandao wakanipa kwa sababu ipo kila chumba.

"Nikawatafuta wenyeji wangu, waniletee chakula maana njaa ilikuwa inauma sana na bariki ilikuwa kali, niliomba wali na chai ila wali ukanishinda hakuwa kama nilivyotegemea kimapishi.

YO 03

"Ikabidi niombe chai na mkate na mkate wenye ni skonzi ndogo sana na kibakuli kidogo cha supu, mazoezi nikawa nafanyia chumbani kwangu maana hawakuwa na muda na mimi tena kwa ajili ya kujua mahitaji yangu.

"Mzee Mlundwa na bondia aliyempeleka walipigana siku ambayo mimi naenda kupima uzito na aliyekuja kunichukua ni yule mtu wa pili niliyekuwa nawasiliana naye mbaya zaidi ndiyo alikuwa mpinzani wangu.

"Tukaenda tukapima baada ya kupima akanirudisha hotelini ingawa changamoto nyengine ikawa ipo upande wa chakula kwa sababu ujazo ulikuwa mdogo sana.

"Siku ya pambano, yule bondia hakuja kunifuata ila aliniambia niende mapokezi waniagizie taxi inilipeleke mahali alipo ila katokea changamoto ya kutoelewana wenyewe ikapelekea nipoteze muda mwingi mapokezi maana nikitaka mawasiliano hadi nirudi ghorofa ya 14 kilipokuwa chumba changu.

"Nilijitahidi kuuliza hadi pale hotelini akatokea mtu akanielekeza hoteli niliyopaswa kwenda ambayo niliambiwa haziwezi kuzidi dakika tano, ikabidi niingie mtaani mwenyewe kwenda.

"Nikajikuta nazurura na hotelini sikifiki halafu baridi kali inapiga, ikabidi nirudi kwenye ile hoteli ndiyo akatokea mtu ambaye akanichukulia taxi ya mtandaoni baada ya kumuomba, yeye akaniambia mwenyeji wangu nikifika ifabidi amtumie pesa yake.

"Kweli nikaenda japo nilikuwa nimechelewa na nikwambia juu ya pesa ya taxi, baada ya hapo ndiyo tukaja kuchukuliwa na promota nikiwa na mpinzani wangu hadi kwenye ukumbi lakini tulivyofika wakanionyesha chumba cha kujiandaa.

"Lakini sikuwa hata na mtu wa kusaidia na hakukuwa na mtu mwengine kutoka Afrika, kuna kocha wa Kirusi nikaomba anisaidie ndiyo alinifunga bandeji na kunisaidia wakati napigana kwa kunipa maelekezo.

"Tulipigana kwa raundi, nikatangazwa mshindi wa majaji watatu, yule mpinzani wangu akashuka fasta kuondoka maana hakutegemea kabisa kama nitampiga ikabidi nimfuate kwa sababu sikuwa najua nani ananilipa.

"Nikamuuliza wakala wangu, nalipwa na nani akaniambia hao watakulipa mwisho wa siku nikaondoka na mpinzani wangu baada ya kusema yeye ndiyo atanilipa, tukaenda hadi kwenye hoteli yake, akanilipa pesa yangu.

"Tukalala wote pale, asubuhi siku ya Jumamosi akanipeleka Uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani.


Nini kililipelekea wewe kukwama?

"Unajua kilichotea baada ya kufika Uwanja wa Ndege, nilisubiri dirisha na ndege ya kampuni yangu lifunguliwe kwa ajili ya kuprint tiketi na muda ulivyofika nikafanikiwa lakini changamoto iliotokea foleni ya ukaguzi ilikuwa kubwa na ikawa haendi inavyopaswa.

"Kuna mmoja wa maofisa akaniuliza naondoka na ndege gani nikamtajia akanihamishia kwenye mstari mwengine ili niwahi kwa bahati mbaya namaliza tarabu yule askari akanifuata na kuniambia ndege imeshaondoka.

"Kiukweli sikuwa peke yangu tulikuwa kama watu sita wa mataifa tofauti, tukaelekezwa twende  kwenye ofisi ya kampuni ya ndege tuliyokata tiketi ili watubadilishie tiketi lakini, niliambiwa natakiwa nikate mpya.

"Ulitokea mzozo kidogo, wakati huo viza yangu inaishq Jumatatu, nikawasiliana na wakala wangu na TPBRC ili waweze kunisaidia, wakala nilimwambia amcheki promota.

"Lakini promota alisema yeye alisharudi kwenye nchi yake hawezi kusaidia chochote ila ashauri niende uwanja mwingine umbali wa masaa mawili nitapata tiketi ya bei rahisi maana pale Moscow ilikuwa dola 1000 halafu kuliwa na tiketi ya dola 800 kutoka Urusi hadi Dubai halafu Tanzania.

"Kumbuka kwamba pesa siyo yote yangu ambayo ndiyo nilienda kupigania lazima nije nigawane na wakala wangu, ikabidi nimpigie simu kumueleza, yeye akaniambia nisubiri waongee na balozi wa Tanzania, Urusi wajue anasemaje.

"Sasa watu wa ubalozi walivyonicheki nikawa nimeshatoka Moscow kwenda uwanja mwengine ambao niliambiwa tiketi bei rahisi ambapo ilinibidi nimlipe taxi mwenyewe ingawa haikuwa rahisi kwa sababu alitaka nimlipe kwa Rubin na siyo dola.

"Watu wa ubalozi wakaniuliza kama nina pesa ya tiketi nikawaambia wakaniambia watanikatia mtandao ambapo tulipata tiketi ya dola 700 ambayo awali ilikuwa dola 770 ya ndege ya kupita Dubai.

"Sasa wakati nashughulikia hilo ndiyo naona taarifa zikasambaa kwamba nimekwama lakini wakati huo nilishapata tiketi kwa msaada wa ubalozi kupitia pesa yangu mwenyewe kwa sababu ubalozi hauna fungu la kugharamia safari za watu.

"Taarifa nilikuja kuzifahamu baada ya kufika Dubai kwa sababu sikuwa na uwezo wa masiliano kwenye ndege na hilo ndiyo lililotokea.

"Nawashukuru TPBRC na serikali kwa kuweza kunisaidia kurudi licha ya kupitia changamoto lakini pia nimeshauriwa kwamba nikiwa na pambano la nje natakiwa kutafuta ubalozi ili watambie na kama ikitokea changamoto iwe rahisi kusaidiwa," anasema Ayoo.