Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kazi aliyonayo Aisha Mnunka Simba Queens

Aisha Pict

Muktasari:

  • Licha ya nyota huyo kurudi unyamani, lakini jambo ambalo mashabiki wanajiuliza ni juu ya  kazi kubwa aliyo nayo kurudisha kiwango chake cha msimu uliopita ambapo alikuwa bora akiwatungua makipa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) atakavyo, wakiwemo wa Yanga Princess na JKT Queens.

KAMA tulivyoripoti  tangu kuanza kwa sakata la mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka hadi lilipoisha baada ya pande zote mbili kukaa chini na kumalizana, lakini kuna jambo ambalo kila mtu anajiuliza.

Licha ya nyota huyo kurudi unyamani, lakini jambo ambalo mashabiki wanajiuliza ni juu ya  kazi kubwa aliyo nayo kurudisha kiwango chake cha msimu uliopita ambapo alikuwa bora akiwatungua makipa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) atakavyo, wakiwemo wa Yanga Princess na JKT Queens.

Msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao 20 na kuibuka mfungaji bora wakati ambao kocha mkuu wa timu hiyo alikuwa Juma Mgunda aaliyetimkia Namungo. Kufuatia matokeo mabaya kwenye michuano ya Cecafa ambayo Simba ilishiriki, timu hiyo ikamtimua Mgunda na kumkabidhi Mghana Yussif Basigi ambaye ni mgeni kwa mchezaji huyo.


MU 01 (1)

ILIVYOKUWA

Picha lilianza Agosti mwaka jana baada ya Mnunka kumaliza majukumu ya timu ya taifa ‘Twiga Stars’ alipaswa kurejea kambini na wenzake, lakini hakuonekana.

Wakati huo Simba ilikuwa inajiandaa na michuano ya Cecafa kwa wanawake ambayo ilikuwa inachezwa Addis Ababa, Ethiopia.

Ndani ya wiki moja ambayo Simba ilikuwa kwenye maandalizi nyota huyo hakutokea na hata simu yake ikipigwa haikupatikana.

Mwanaspoti lilifahamu moja ya sababu za Mnunka kutoroka kambini ni moja ya timu iliyopanda Ligi Kuu ya Wanawake ilimsajili kimyakimya.

Mbali na kumsajili alifanya mazoezi na timu hiyo ilimpa ahadi ya kumnunulia nyumba ya kuishi, gari pamoja na simu nzuri na vyote mchezaji aliridhia.

MUV 04

Hata hivyo, ahadi hiyo haikutimia kwani mmoja wa kiongozi wa timu hiyo aliliambia Mwananspoti kuwa wanapitia kipindi kigumu cha ukata wa kifedha, hivyo wameshindwa kumpa mahitaji Mnunka kama walivyokubaliana.

Baada ya kutangaza kwa umma kwamba nyota huyo hajaonekana, Simba ilimtafuta kupitia mawasiliano yake ya simu, lakini nayo hayakufua dafu.

Timu hiyo haikuishia hapo iliendeleza juhudi za kumtafuta meneja wa mchezaji huyo ambaye naye pia ilidaiwa hakuwa anapatikana ndipo ikakimbilia TFF kushtaki na Kamati ya Hadhi za Wachezaji ikaamuru  pande mbili baina ya mchezaji na timu zimalizane na hatimaye sasa yupo katika timu hiyo akicheza.


MUV 02

KAZI ALIYONAYO

Licha ya mchezo wake wa kwanza kufunga mabao mawili dhidi ya Mlandizi Queens - timu iliyopo mkiani mwa msimamo, lakini bado ana kazi kubwa ya kuonyesha kiwango chake.

Nyota huyo alikaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano bila kucheza mchezo wowote wa mashindano.

Ikumbukwe nyota huyo alikuwa mfungaji bora msimu uliopita akiibuka na tuzo ya kiatu cha dhahabu kwa kufunga mabao 20 huku tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) ikienda kwake pia.

Kutokana na sintofahamu aliyokuwa nayo tangu msimu huu nyota huyo alikuwa hajaonekana uwanjani duru la kwanza lote na kutoonekana muda mrefu na timu kunaweza kumfanya asiwe katika kiwango kama cha msimu uliopita.

MUV 05

Ingawa ametupia mabao mawili dhidi ya Mlandizi Queens, lakini ukweli ni kwamba timu hiyo iko mkiani mwa ligi na hivyo haipo fiti kivile katika ushindani wa kweli. Mnunka anarejea wakati ambao Simba inamtegemea mshambuliaji Mkenya Jentrix Shikangwa ambaye ni kinara wa mabao akiwa nayo 13 katika mechi 10. Shikangwa ambaye amekuwa na mwendelezo mzuri wa kiwango bora msimu huu akiwa na wastani wa kufunga bao moja kwa kila mchezo.

Ikumbukwe pia Shikangwa ni msimu wake wa tatu kucheza Ligi ya Kuu ya wanawaka Bara akitokea Vihiga Queens ya Kenya na msimu wake wa kwanza (2022/23) aliibuka kinara akitupia mabao 17. Hivyo hadi sasa mshindani mkubwa na kazi aliyonayo Mnunka kuipambania namba kwenye kikosi hicho ni Shikangwa ambaye ana uzoefu ndani ya Simba.

Mbali na Shikangwa, pia Mnunka ana kazi kumuaminisha kocha wa timu ya taifa ‘Twiga Stars’, Bakari Shime juu ya kiwango chake baada ya kipindi kirefu kupita bila kucheza. Ushindani kwenye kikosi cha timu ya taifa ni mkubwa kutokana na nafasi anayocheza kuwapo nyota kama Aisha Masaka anayecheza Brighton ya England, Stumai Abdallah (JKT Queens), Opah Clement (Henan Jianye), Clara Luvanga (Al Nassr), Enekia Lunyamila (Mazaltan) na wengine ambao wamekuwa wakiingia na kutoka.

Ili kumvutia Shime kwenye kikosi nyota huyo anapaswa kuonyesha juhudi ndani ya Simba.


MUV 03

MSIKIE MWENYEWE

Akizungumza na Azam TV baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mlandizi Queens, Mnunka alisema amerudi uwanjani kuisadia timu yake kufikia malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara.

“Najua watu walinimisi, nimerudi. Natamani kuisaidia timu yangu kuchukua ubingwa. Kwa sasa ligi ni ngumu hadi mwisho wa msimu ndio tutafahamu vizuri,” alisema mchezaji huyo.