Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juni 25 tucheze dabi, halafu wote tuseme ‘Never again’

JICHO Pict

Muktasari:

  • Wana msemo wao maarufu wa ‘Never Again’. Kwamba haitatokea tena. Nataka tuutumie msemo huu kukomesha ubabe wa Simba na Yanga katika soka letu. Mtu mmoja pekee ambaye alihitajika kuturudishia pambano la Dabi amefanya hivyo. Rais wa nchi.

WANYARWANDA waliuana vilivyo katika mauaji ya kimbari (genocide) Aprili 1994. Watutsi na Wahutu waliuana kiasi cha kufikia idadi ya watu milioni moja waliopoteza maisha. Baada ya vita kumalizika walijiapiza kutorudia tena kilichotokea.

Wana msemo wao maarufu wa ‘Never Again’. Kwamba haitatokea tena. Nataka tuutumie msemo huu kukomesha ubabe wa Simba na Yanga katika soka letu. Mtu mmoja pekee ambaye alihitajika kuturudishia pambano la Dabi amefanya hivyo. Rais wa nchi.

Vinginevyo tulikuwa gizani kuhusu pambano hili. Jana ilikuwa wazi kwamba Yanga wasingeingia uwanjani kucheza pambano hili kama walivyosema. Na sikuona kama Mwamuzi angeingia uwanjani na kupuliza filimbi yake akimaliza pambano baada ya kuisubiri Yanga kwa dakika 30.

Kwamba Ahmed Arajiga angeweza kuingia uwanjani na kumaliza pambano sikuona dalili hiyo. Ni kama ambavyo sikuona kama mwamuzi angeingia uwanjani na kuipa Yanga pointi tatu Machi 8. Huu ndio ukubwa wa Simba na Yanga.

Yanga angegomea pambano la jana, Bodi ya Ligi ingepanga mechi upya, Simba angegomea tena na wasingefanywa kitu. Mchezo huu ungeweza kuendelea kwa muda mrefu na kusingekuwa na mtu mwenye ubavu wa kutoa pointi tatu za mezani hasa nyakati hizi ambazo wamepishana kwa pointi chache.

JICH 01
JICH 01

Wenyewe wanafahamu ukubwa wao, ndio maana wakisema hawachezi huwa wanamaanisha. Rafiki zetu Coastal Union au Kagera Sugar huwa hawana ubavu huu. Wanajua tu kwamba wakifanya ujinga huu, basi wataporwa kweli pointi tatu na sheria zote zitafuata. Wakubwa Simba na Yanga wanajua kuwa jambo hili halipo kwao.

Lakini sasa ifike mwisho. Wote tusema ‘never again’ kama Wanyarwanda walivyosema. Imetosha. Tusirudie tena ujinga huu uliotokea. Tusihitaji kupigiwa simu za kwenda Dodoma ili kuambiwa mechi ichezwe.

Kuanzia sasa kusiwe na sababu za kijinga kuahirisha pambano la Simba na Yanga katika dakika za majeruhi. Tunahitaji wanaume katika Bodi ya Ligi ambao watakuwa huru na watakuwa na jeuri ya kutopokea maagizo kutoka juu. Mpira usiingizwe katika siasa tena.

JICH 02

Timu ambayo itakacha kuingia uwanjani sheria zichukue mkondo wake. Mpinzani apewe pointi tatu. Vinginevyo kilichotokea msimu huu kitatokea tena na tena. Imewahi kutokea mara saba nyuma na kama hatutasimama imara basi itatokea tena na tena.

Wanajua hakuna wa kuwafanya kitu. Ikitokea mtani mmoja akipewa pointi tatu za mezani na bado Bodi ya Ligi ikashikilia msimamo wake nadhani adabu itarudi. Mbona Misri wamefanya? Tatizo letu tumewadekeza wakubwa kwa kiasi kikubwa.

Tunaahirisha mechi bila ya kujua madhara yake. Kuna watu wanaingia gharama nyingi kutoka mikoani kuja kutazama mechi. Watu wanatoka Simiyu, Newala, Ngara na kwingineko kuja kuangalia dabi. Wanatumia mamilioni ya pesa kwa nauli na kuja kukaa katika nyumba za kulala wageni. Lakini ghafla simu moja kutoka juu inaamua kuahirisha mechi.

JICH 03

Kampuni ya Azam TV iliyotia mamilioni ya pesa kama udhamini katika ligi yetu inaingia hasara kubwa kwa kutoonyesha pambano hilo kwa sababu ya simu ya mtu mmoja tu kutoka juu. Upuuzi wa karne nyingi zilizopita.

Kuna wadhamini wa Ligi ambao kupitia mechi kama hii wanapata fursa kubwa ya kujitangaza, lakini mtu mmoja anapiga simu kutoka juu na kuahirisha pambano kwa sababu zake binafsi. Kampuni zikijitoa katika udhamini klabu zinapata shida kujiendesha.

Watu wa Bodi wawe imara, lakini kwa wakubwa ambao wanaingilia mechi hizi kwa maslahi yao nadhani wanapaswa kupata funzo kubwa kwa kilichotokea. Binafsi naamini Almasi Kasongo na Steven Mguto wametolewa kafara tu katika sakata hili.

JICH 04

Kuna mtu ametulia sehemu kama kivuli akishuhudia kung’olewa kwa Mnguto na Kasongo, lakini anajua kwamba yeye ndiye chanzo cha pambano hili kutochezwa. Mtu huyu naye tumwambie ‘never again’ na asiharibu mpira wa nchi hii.

Fifa hawakuwa wajinga kutaka mpira wa miguu ujitegemee. Walijua kwamba kuna aina ya watu wataleta utata mkubwa kama huu. Tusipokemea itajirudia tena na tena. Tutaendelea kuwatoa kafara watu wengi wasiohusika.

Na sasa tuna mechi mkononi. Ninachokiona kwa sasa Simba waamke. Yanga wamejinyanyua kisaikolojia kwa sababu walikuwa wa mwisho kushinda takwa lao baada ya Simba kushinda takwa la Machi 8. Yanga wamekuwa wakijitamba mitandaoni kwamba wapo tayari kucheza na watashinda mechi.

Yanga walikuwa wa kwanza kuposti katika ukurasa wao wa mitandao ya kijamii kukaribisha mechi lakini hadi sasa Simba hawajaandika chochote kuhusu mechi hiyo. Ni kweli waliamini katika pointi za mezani?


Wanachotakiwa kwa sasa ni kukubali kwamba mechi ipo na wapo tayari kushinda na kutwaa taji. Hii itarudisha morali ya wachezaji na timu yenyewe kwa ujumla. Ukimya wao unaipa faida Yanga kujiona ipo hatua nyingi mbele ya mtani ndani na nje ya uwanja.

Wakati mwingine mechi hizi zinashinda kisaikolojia zaidi. Simba waamke sasa na kuanza kutembeza mikwara ya hapa na pale. Ukimya wao unaonyesha kama vile walikuwa wanasubiri pointi za mezani zaidi kuliko kuicheza mechi yenyewe.

Mechi nne zilizopita Simba imefungwa na Yanga, lakini kadri siku zinavyoendelea pengo lao na Yanga linapungua. Ni tofauti na ilivyokuwa wakati ule inafungwa mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Mkapa. Sasa hivi kuna kina Ellie Mpanzu ambao wameifikisha timu katika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika. Kwanini waogope?

Mpira umeshinda. Tunasubiri mechi nzuri na ya kusisimua ambayo ni wazi itafunga msimu kabla hatujaelekea katika masuala ya usajili ingawa siku tatu baadaye Yanga watacheza na ndugu zao Singida Black Stars katika fainali za Shirikisho pale Unguja.