Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jokic kupenya bato la NBA MVP msimu huu?

JOKIC Pict

Muktasari:

  • Kuna takwimu chache ambazo Jokic ameshindwa kuzifikia ikiwamo ya mchezaji ambaye amezoea kukusanya 'triple-double' siyo kwa mechi moja tu, bali kwa msimu mzima. Hata hivyo, nyota huyo wa Denver Nuggets huenda hatimaye akakutana na kikwazo.

OKLAHOMA, MAREKANI: NIKOLA Jokic anaendelea kupona taratibu, hali inayompa Luka Doncic nafasi ya kupanda hadi nafasi ya pili kwenye kinyang'anyiro cha kuwa mchezaji bora wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) yaani MVP hivi karibuni.

Kuna takwimu chache ambazo Jokic ameshindwa kuzifikia ikiwamo ya mchezaji ambaye amezoea kukusanya 'triple-double' siyo kwa mechi moja tu, bali kwa msimu mzima. Hata hivyo, nyota huyo wa Denver Nuggets huenda hatimaye akakutana na kikwazo.

Namba hiyo ni 65; idadi ya chini ya michezo inayotakiwa ili mchezaji astahili tuzo za NBA. Kwa kuwa Jokic yuko nje tangu Desemba 29 kutokana na jeraha la goti na hakuna ratiba rasmi ya kurejea kwake.

Iwapo atacheza leo Jumapili dhidi ya Oklahoma City au keshokutwa, Jumanne, dhidi ya Detroit na kuepuka kutolewa atajitengenezea mazingira bora zaidi ya u-MVP. Lakini, hatapaswa kukosa mchezo wowote uliosalia msimu huu. Nuggets wana mechi tano za back-to-back zilizobaki kwenye ratiba.

JOK 01

Kama yasingekuwa majeraha na Jokic angeendelea kucheza kwa sababu hapendi kupumzishwa au kukaa nje ya michezo, alikuwa na nafasi bora zaidi. Lakini Nuggets wana sauti yao kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa timu yenye matumaini ya kutwaa ubingwa ambayo imecheza vizuri hata bila yeye.

Hilo siyo jambo jema kwa Jokic ambaye alikuwa mbele kwa mbali katika mbio za kuondoka na tuzo ya MVP kabla ya kuumia. Tangu hapo, nafasi yake imekuwa tete. Shai Gilgeous-Alexander amechukua nafasi ya kwanza, huku Luka Doncic akiwa namba mbili wiki hii katika kinyang'anyiro hicho.

Hali hiyo inafanana kwa kiasi fulani na aliyopitia 'Hall of Fame' Bill Walton msimu wa 1977–78. Mabingwa watetezi Portland Trail Blazers walishinda michezo 50 kati ya 60 ya kwanza, na matumaini ya kutetea taji yalionekana makubwa. Walton alikuwa akifunga wastani wa pointi 18.9, ribaundi 13.2, asisti tano na kuzuia mara 2.5 kwa mchezo akiwa Jokic wa wakati wake kama senta bora.

Lakini, katika hali ya kushangaza alivunjika mguu na kucheza michezo 58 - idadi ndogo zaidi kuwahi kucheza mshindi wa MVP kabla au baada ya hapo. Tofauti ni kwamba Walton alimaliza msimu wa kawaida (regular season). Alirejea kwenye mchujo (playoffs), lakini akaumia tena katika mchezo wa pili wa mfululizo wa kwanza wa Blazers.

JOK 02

Jokic, kwa upande mwingine atarejea wakati fulani msimu huu.

Tofauti nyingine? Wakati huo hakukuwa na idadi ya chini ya michezo inayotakiwa ili mchezaji astahili kuwa MVP, kupenya katika kikosi cha All-NBA star au tuzo nyingine. Kwa sasa, Jokic anashiriki 'mashindano matatu' tofauti dhidi ya timu pinzani, kanuni ya michezo 65 na kama atakuwa na bahati na kutimiza vigezo basi dhidi ya mastaa wote wanaopambana kubeba tuzo hiyo.

Vyovyote iwavyo atabaki na kumbukumbu ya 'triple-double' ya pointi 56 aliyoipata siku ya Krismasi mwaka jana na  huenda hakuna staa atakayeifikia msimu huu na pengine kwa muda mrefu ujao.


VIGEZO VINGINE?

Kuwa MVP wa NBA kunahitaji mchanganyiko wa vitu kadhaa. Siyo suala la kipaji tu, bali kile unachotoa kwa timu.

Kwa kifupi, haya ndiyo mambo makuu

Takwimu; MVP kawaida anapaswa kuwa na takwimu kali yaani pointi nyingi za kufunga, riboundi na asisti. Pia anatakiwa kuwa na ufanisi uwanjani akiibeba timu mabegani kwake. Siku hizi takwimu za nyongeza zinaangaliwa zaidi.

Mafanikio ya timu; karibu kila MVP anatoka kwenye timu inayofanya vizuri msimu husika. Mara nyingi timu ya juu kwenye ukanda. Ukiwa mchezaji bora lakini timu iko chini, nafasi inapungua.

JOK 03

Umuhimu kwa timu; unaitwa “Most Valuable” kwa sababu bila wewe timu ingeumia. Ukiwa kiongozi au mtu anayeibeba timu kila mchezo hilo linaongeza uzito.

Kucheza mfululizo; siyo mechi 10 nzuri tu. MVP anakuwa mkali kuanzia mchezo wa kwanza hadi wa mwisho na anaepuka majeraha makubwa na kukosekana mchezoni mara kwa mara.

Ubora flani hivi; hili lina nguvu. Mfano hapa ni kuibeba timu baada ya majeruhi, kubadili ubora wa timu kuwa mzuri zaidi na kurudia ubora kila mara baada ya kubezwa (hili mara nyingi hutumiwa na waandishi wa habari wanaopiga kura)

Uongozi & heshima ya ligi; unavyoongoza wenzako, unavyoheshimika na wapinzani na hata lugha ya mwili wako mchezoni vyote vinaangaliwa.

Wapinzani ni kina nani? Kila msimu unashindana na nyota wengine. Wakati mwingine unafanya msimu kuwa bora na kurudia tena na tena dhidi ya timu na mastaa wa timu pinzani.

JOK 04

TANO BORA

1. Shai Gilgeous-Alexander (Oklahoma City Thunder); Anaongoza kinyang'anyiro cha MVP akiwa na pointi 32, ribaundi 4.4 na asisti 6.2 kwa mechi. Gilgeous-Alexander ni wa pili kwa ufungaji NBA nzima na ndiye mwenye rekodi bora zaidi katika ligi. Akishinda MVP ya pili mfululizo atajiweka miongoni mwa magwiji wa muda wote.

2. Luka Doncic (Los Angeles Lakers); Wiki iliyopita alikuwa nafasi ya tatu na sasa amepanda moja. Takwimu za msimu zinaonyesha ana wastani wa  pointi 33.6, ribaundi 8.7 na asisti 7.7 kwa mechi. Vita yake na Gilgeous-Alexander ni nzito na haitabiriki kwani huenda ikaenda hadi mwisho wa msimu wakivutana.

Mwamba huyo anaongoza ligi kwa ufungaji akiwa wa tatu kwa asisti na ni miongoni mwa walinzi wanaowini ribaundi nyingi zaidi. Amefunga angalau pointi 25 akiwa na ribaundi tano na asisti tano katika michezo sita mfululizo, na alianza wiki iliyopita akifunga pointi 46 dhidi ya Chicago Bulls.

3. Nikola Jokic (Denver Nuggets); Alikuwa wa pili wiki iliyopita, lakini ameporomoka. Licha ya majeruhi takwimu za msimu zinambeba kwani ana wastani wa pointi 29.6, ribaundi 12.2 na asisti 11. Ana wastani wa 'triple-double' na kitakwimu yuko ndani ya watatu bora kwa ufungaji, reboundi (namba moja) na asisti (namba tatu). Kwa maneno mengine, Jokic ni wa kawaida. Mechi zake bora ukimlinganisha na mtu mmoja mmoja anawazidi wengine wote kwenye kinyang'anyiro. Jokic ameanza mazoezi ya uwanjani katika wiki mbili zilizopita. Kwa sasa suala ni kubaki katika kinyang'anyiro cha tuzo. Akikosa vigezo ataondolewa na ingawa sheria ni sheria, itakuwa pigo kwa mmoja wa magwiji wa mchezo wa kikapu.

4. Victor Wembanyama (San Antonio Spurs); Mkali huyo yupo nafasi ya nne aliyokuwapo kwa wiki iliyopita akiwa na wastani wa pointi 24.3, ribaundi 11.2 na kuzuia 2.7 kwa msimu. Wiki iliyopita alianza vibaya dhidi ya Rockets (pointi 28, ribaundi 16 na kuzuia mara tano). Cha kuzingatia alicheza dakika 28 tu katika ushindi huo. Hilo linaendana zaidi na msimu wake mzima, na hata wachezaji bora hupitia kipindi cha kushuka kiwango. Badala ya kuangalia tukio moja, ni bora kumhukumu msimu wake kwa ujumla. Kwa mtazamo huo, huu ndio msimu bora zaidi kuwahi kucheza. Hakuna anayezidi wastani wake wa kuzuia, na mchezo wake wa kushambulia umeimarika. Ni vigumu kupata mchezaji mwingine kwenye kinyang'anyiro mwenye uwiano huo mzuri pande zote mbili za uwanja.

5. Jaylen Brown (Boston Celtics); Nafasi yake wiki iliyopita alikuwa nafasi ya sita akiwa na wastani wa takwimu za msimu pointi 29.4, ribaundi 6.8 na asisti 4.9. Brown anaendelea kung’ara akiwa Celtics ambako bado wanamkosa Jayson Tatum. Na kama hali ingekuwa kinyume, je, Tatum angekuwa ndani ya tano bora wa MVP bila Brown? Bila shaka ni jambo jema kwa Brown. Hata hivyo Brown ana rekodi za juu zaidi binafsi karibu kila kipengele msimu huu (wa tatu kwa ufungaji), hasa akionyesha ubora zaidi kwenye ushambuliaji (majaribio 986 ya mashambulizi). Uwezo wake wa kuibeba timu inayokosa wachezaji wakubwa wanne msimu uliopita (Tatum, Al Horford, Kristaps Porzingis na Jrue Holiday) ni wa kipekee.

JOK 05

MASTAA 10 WANAOFUATA

6. Cade Cunningham (Detroit Pistons)

7. Donovan Mitchell (Cleveland Cavaliers)

8. Tyrese Maxey (Philadelphia 76ers)

9. Anthony Edwards (Minnesota Timberwolves)

10. Jamal Murray (Denver Nuggets)

11. Scottie Barnes (Toronto Raptors)

12. Jalen Brunson (New York Knicks)

13. Kevin Durant (Houston Rockets)

14. Jalen Johnson (Atlanta Hawks)

15. Alperen Sengun (Houston Rockets)