Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaruph: Kutoka Yanga, Simba hadi Morocco

Muktasari:

  • Hata hivyo, kwa Jaruph Juma kwake hakuna kukata tamaa. Licha ya kutamba na klabu za vijana za Yanga na Simba, hakupata nafasi ya kucheza soka la kawaida na kuamua kuibukia la ufukweni na sasa anatamba nalo akiwa nchini Morocco anakokipiga na klabu ya Ain Diab.

CHANGAMOTO ni moja ya hali inayomsukuma binadamu au kiumbe chochote kuchukua maamuzi magumu. Wapo wanaokata tamaa kutokana na changamoto iwe za kimaisha ua mambo wanayotaka kufanya.

Hata hivyo, kwa Jaruph Juma kwake hakuna kukata tamaa. Licha ya kutamba na klabu za vijana za Yanga na Simba, hakupata nafasi ya kucheza soka la kawaida na kuamua kuibukia la ufukweni na sasa anatamba nalo akiwa nchini Morocco anakokipiga na klabu ya Ain Diab.

Mwanaspoti lilimtafuta na kufanya naye mahojiano na anasema uwepo wake huko ni fursa kubwa kwani imemwezesha kuchezea timu ya taifa ya soka la ufukweni kwani awali haikuwa rahisi.

ALIVYOTUA MOROCCO

Anasema sababu ya kufanikisha dili hilo ni pamoja na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afcon,

“Morocco walikuwa wakifuatilia sana tunapokutana timu za taifa na hizi mechi za mwezi uliopita nikapata dili hilo,” alisema Jaruph na kuongeza;

“Kila tunapocheza na Morocco nimekuwa nikiwafunga sana zaidi ya bao moja, kwa hiyo ilikuwa suala la muda na nafasi tu naamini muda umefika na mimi kuchezea nje.”


ANAPAMBANA MWANZO MWISHO

Anasema tayari amepata nafasi ya kucheza mechi tisa za ligi akiweka kambani mabao saba jambo linalomfanya aendelee kupambana kufunga kila anapopata nafasi.

“Nashukuru Mungu nimecheza dakika zote ni jambo la kuendelea kupambana nalo kwa sababu unacheza nchi za Kiarabu ambazo zina wachezaji hivyo kupata nafasi inatubidi tufanye cha ziada,” alisema Jaruph. 


KAKIPIGA YANGA, SIMBA

Ukiachana na soka la ufukweni Jaruph aliwahi kusakata kabumbu akiwa na Yanga U-20 (2015), African Lyons kuanzia msimu wa 2019/21 na Simba (2016).

“Mimi nimecheza huko ingawa sikufanikiwa kwa kiasi kikubwa, nikaona niache na kutafuta maisha huku.”

“Hata sasa hivi bado naweza kucheza nafasi ya ushambuliaji na nikafunga kama huku ufukweni kwa sababu utofauti na soka wanacheza uwanjani, sisi tunacheza kwenye mchanga.”

ALIONA FURSA UFUKWENI

Nyota huyo anasema kilichomsukuma kucheza soka la ufukweni ni pamoja na fursa ya kuichezea timu ya taifa na hapo awali haikuwa rahisi.

“Binafsi niliona soka la ufukweni kwangu ni fursa baada ya kuwa nafanya vizuri kwenye michezo ya kimataifa nawakilisha nakuipambania bendera ya nchi yangu,”

“Kitu ambacho kwa wakati huo hakikuwa rahisi kupata fursa hiyo kupitia soka la kawaida, kwa hiyo ikabidi kuongeza jitihada kidogo tu huku na kuona namna gani naweza kuendeleza na kuwa chanzo cha maendeleo ya ukuaji wa ufukweni.”


UFUKWENI KUNA CHANGAMOTO ZAKE

Anasema changamoto ni nyingi kwenye mchezo huo na ni rahisi kufanikiwa kama nchi itaamua kuufuatilia kama ilivyo michezo mingine.

“Soka la ufukweni halina ligi imara kwa nchi yetu, hakuna mdhamini, hilo linafanya kutokuwa na ligi bora kwetu tofauti na mataifa mengine kama Morocco,” anasema na kuongeza;

“Lakini pongezi kubwa kwa TFF kwa sababu ndiyo uti wa mgongo wa mchezo huo na kimsingi majukumu ya Shirikisho ni makubwa mno, mzigo walionao kwa timu za taifa ni mkubwa sana, kwa hiyo kuna wakati wanalazimika kujibana ili kuiwezesha timu ya taifa.”

“Kwenye soka la ufukweni kwa ngazi ya timu ya taifa hakuna hamasa kutoka kwa wadau wenye nguvu ya pesa au nguvu ya uhamasishaji.”

“Morocco wako vizuri lakini sio kama Tanzania tuko vibaya, soka la ufukweni halijapata watu sahihi.”

“Fikiria timu inatakiwa iwe na wachezaji 15 tu, ni rahisi kuihudumia kama umekusudia mafanikio, wachezaji na viongozi hawazidi 22 wadau wakiamua kulea idadi hiyo kwa malengo endelevu tunaweza kufanikisha hilo.”


TOFAUTI YA UFUKWENI NA SOKA

Anasema hakuna tofauti kubwa ya soka la kawaida na ufukweni kwani inafuata sheria 17 za mpira.

“Tofauti inakuja kwenye kanuni na Jiografia ya uwanja, aina ya mipira inayotumika, idadi ya wachezaji uwanjani, utaratibu wa kubadilisha wachezaji, kwenye benchi ni ingia toka kama ilivyo futsal.”

“Muda wa mchezo ni dakika 36 zenye vipindi vitatu vya dakika 12 kila kipindi na mapumziko ya dakika tatu na huku hakuna sare, yatapigwa matuta hadi mshindi apatikane.”


KIMATAIFA BADO BADO

“Kwa ranki za Afrika, Tanzania tuko nafasi ya nane baada ya mashindano ya Afcon mwezi uliopita. Tutahitaji kucheza mechi mbili tu mwakani kutafuta nafasi ya kufuzu kushiriki mashindano hayo.

“Timu ikifanikiwa kufuzu Afcon kwa kushinda hizo mechi mbili, inahitaji kushinda mechi nne tu kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia ambayo mwaka jana yalifanyika Russia na mwakani yatafanyika visiwa vya shelisheli.”

Kitendo cha timu kufuzu Kombe la Dunia, hapo tunazungumzia ukombozi wa maisha ya vijana kwa sababu masilahi yake ni makubwa mno, sasa nani anajua kwenye mchezo huo tukiwekeza ili kutafuta matokeo mechi saba maisha ya watu yatabadilika.”

SIMBA, YANGA, AZAM ZIWE NA TIMU ZA UFUKWENI

Anatoa ushauri kwa Simba, Yanga na Azam ambazo zina ushawishi mkubwa kuanzisha klabu za soka la ufukweni ili kukuza mchezo huo.

“Kiufupi ni Simba, Yanga, Azam kuunda timu za ufukweni, mtu akisikia wanacheza Coco, hamasa yake itakuwa ni kubwa na itatengeneza ufahamu kwa watu, huu ni mchezo gani mbona inakuwa hivi wataanza kuufatilia na mwishowe unakua.”