Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

IMRAN KHAN: Nahodha, shujaa wa Kriketi anayeliliwa Pakistan akiwa jela

Muktasari:

  • Walimkumbuka kwa maumivu waliyopata baada ya kufungwa na India, mahasimu wao wakubwa katika mchezo huu na siasa, Februari 17, katika mashindano ya Kombe la Dunia ya kiwango cha chini yaliyofanyika Sri Lanka.

KWA mara nyingine, wananchi wa Pakistan, hasa mashabiki wa kriketi wanamkumbuka Imran Khan aliyekuwa nahodha wa kikosi chao kilichoshinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza na pekee mnamo 1992.

Walimkumbuka kwa maumivu waliyopata baada ya kufungwa na India, mahasimu wao wakubwa katika mchezo huu na siasa, Februari 17, katika mashindano ya Kombe la Dunia ya kiwango cha chini yaliyofanyika Sri Lanka.

Hapo kabla, Pakistani ilisusia kucheza na India ili kuiunga mkono Bangladesh, iliyofungiwa mlango kushiriki shindano la India, ambayo imempa hifadhi aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikha Hasina.

Kiongozi huyo mwanamke, aliyedaiwa kutawala kwa mkono wa chuma alilazimika kuikimbia nchi baada ya maandamano ya kumtaka aachie uongozi. Hivi sasa, akiwa India, anauponda utawala wa sasa wa Bangladesh.

Kilichowaumiza Wapakistani ni kushindwa vibaya na India, ambayo mara ya mwisho kukutana nayo katika mashindano ya kimataifa ilikuwa miongo miwili iliyopita.

Kikosi cha India kiliposhuka uwanjani dhidi ya Pakistan kilizungukwa na wachezaji maarufu wa zamani walioongozwa na Kapil Dev aliyekuwa nahodha wa India iliposhinda Kombe la Dunia 1983 kwa kuifumua West Indies katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Lord’s, Uingereza.

Lakini, Pakistan hawakuwa pembeni. Imran Khan, nahodha wao waliposhinda Kombe la Dunia 1992 kwa kuifunga England katika fainali iliyofanyika Australia, alithibitisha umahiri wa kiuongozi. Wakati pambano lilipofanyika, Khan alikuwa anaendelea kwa mwaka wa tatu gerezani kwa shutuma za ufisadi na rushwa, ambazo zinadaiwa kuwa za kisiasa. Alidaiwa kuzifanya alipokuwa Waziri Mkuu wa Pakistan kuanzia 2008 hadi 2013.

Zaidi ya wachezaji 50 mashuhuri kutoka India, Pakistan, England, Barabados, Afrika Kusini, Bangladesh, Australia na New Zealand wanaitaka serikali ya Pakistan kumuachia Khan ambaye afya yake izorota, huku madaktari na watoto wake waliopo England wakiwa hawaruhusiwi kumuona.

Katika mchezo wa Februari 17, mashabiki wa kriketi waliokuwepo Sri Lanka waliowaona Wapakistani wakimlilia Khan, wakiamini kwamba angekuwepo pembezoni mwa wachezaji wa Pakistan, vijana wao wangepata motisha ya kutafuta ushindi.

Baada ya kustaafu kucheza kriketi, Khan alidhihirisha uongozi wake kwa kuanzisha Chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) mnamo 1996, na kushinda uchaguzi miaka minane baadaye akawa Waziri Mkuu. Ushindi wake uliendelea kuwahamasisha wanamichezo mashuhuri wa nchi mbalimbali duniani kuingia katika siasa na kupata mafanikio.


MAISHA NA MAFANIKIO YA KHAN

Alizaliwa Punjab 1952 na kupata elimu katika vyuo mbalimbali vya Uingereza, ikiwa pamoja na Chuo Kikuu cha Oxford. Alianza kucheza kriketi akiwa na miaka 13 katika shuleni mjini Worcestershire na alichaguliwa kujiunga na timu ya Pakistan 1971 akiwa na miaka 18.

Baada ya kufaulu katika Chuo Kikuu cha Oxford alikwenda Pakistan na kuichezea timu ya taifa hadi 1992 alipostaafu baada ya kuiongoza kubeba Kombe la Dunia. Hadi leo, anahesabika kuwa mmoja wa wachezaji wa kriketi waliofanikiwa zaidi duniani, na habari zake zimewekwa katika ukumbi wa Baraza la Kimataifa la Kriketi (ICC).

Mnamo 1991, alichangisha fedha kusaidia wagonjwa wa kansa kama kumbukumbu kwa mama yake aliyepoteza maisha Khan aliye na mafunzo ya udaktari alichangisha Dola 25 milioni kwa hospitali mbili za Pakistan, moja mjini Lahore na nyingine Peshawar.

Alijitokeza Aprili 1966 kuunda chama cha siasa kinachojulikana kama Pakistan Tehreek-e-Insaf (Vuguvugu la Haki la Pakistan). Alishinda ubunge 2002 akashika wadhifa huo hadi 2007, na kuchaguliwa tena hadi 2013.

Chama chake kilikuwa cha pili kwa ukubwa Pakistan. Khan pia ameandika vitabu vingi juu ya matibabu na michezo. Ushindi wake wa kisiasa unaendelea kuonyesha historia ya wanamichezo na wachezaji maarufu wa sinema kuingia siasa na kufanikiwa.

Baadhi ya wanamichezo waliopata mafanikio makubwa katika siasa wakiwamo, George Weah, aliyekuwa rais wa Liberia na kuwahi kuwa mchezaji maarufu wa kandanda aliichezea Monaco, PSG, AC Milan, Chelsea na Manchester United. Alianzisha Chama cha Congress for Democratic Change 2004, akagombea urais  2011 na kushindwa, lakini akashinda uchaguzi wa rais mnamo 2017. Pele (Arantes do Nascimento); aliingia siasa kama Waziri wa Michezo wa Brazil 1995.

Arnold Schwarzenegger; mcheza sinema wa Marekani, aliyekuwa seneta wa California, Marekani 2003 hadi 2011;

Mohammad Azharuddin, nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya India aliyechaguliwa mbunge 2009 na Zico (Arthur Antunes Coimbra), mchezaji maarufu wa kandanda wa Brazil aliyehudumu kama Waziri wa Michezo wa Brazil 1990.

Wengine ni Hakan Sukur, mfungaji bora wa mabao wa Uturuki aliyeingia katika siasa na kuchaguliwa mbunge 2011. Hivi sasa yupo Marekani kama mkimbizi wa kisiasa akiendesha biashara ndogondogo za vyakula.

Kwa sasa kinachosubiriwa ni kuona hatima ya Imran Khan na kwa kiasi gani uwepo wake gerezani utaathiri maendeleo ya kriketi na serikali ya Pakistan. Wakati ndio utaotupa majibu. Tusubiri.