Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hapa ndo anapoishi bosi kubwa Arsenal

BOSI Pict

Muktasari:

  • Mwaka 2023, Josh alivutia vichwa vya habari si tu kwa mafanikio ya timu zake, bali pia kwa kununua jumba la kifahari lenye thamani ya Dola 15.75 milioni katika eneo la kipekee la Cherry Hills Village, Colorado, Marekani.

LONDON, ENGLAND: JE umewahi kujiuliza mtu anayesimamia himaya ya michezo yenye thamani ya mabilioni ya dola huenda wapi kupumzika? Unapokuwa Josh Kroenke, hununui tu nyumba, bali unanunua mahali pa kujisitiri.

Mwaka 2023, Josh alivutia vichwa vya habari si tu kwa mafanikio ya timu zake, bali pia kwa kununua jumba la kifahari lenye thamani ya Dola 15.75 milioni katika eneo la kipekee la Cherry Hills Village, Colorado, Marekani.

Nyumba ya hiyo ya kifahari ya Josh, mmoja wa watoto wa bilionea Stan Kroenke na mkewe Ann Walton Kroenke imejengwa kwenye eneo tambarare lenye mandhari ya kuvutia. Kroenke anamiliki timu maarufu za Arsenal inayokimbiza katika Ligi Kuu England na Denver Nuggets ya Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Vilevile anamiliki timu kadhaa za michezo ya kulipwa zikiwemo Los Angeles Rams ya Soka la Kimarekani, Colorado Avalanche ya Ligi ya Mchezo wa Magongo Marekani, Colorado Rapids ya Ligi Kuu Marekani.

Kwa Josh, mtoto wa bilionea na mmoja wa wasimamizi wakuu wa Arsenal siyo tu nyumba ya kawaida anayoishi, bali ni jengo ambalo lina kila kitu ndani likiwa na faragha na ladha ya hali ya juu kwa mtu anayekuwa ndani yake katika eneo lenye ukubwa wa zaidi ya futi za mraba 12,000. Kwa ujumla ni nyumba ya mfano bora wa anasa ya kisasa.

BOS 01

CHERRY HILLS VILLAGE

Eneo la Cherry Hills Village ni makazi ya watu maarufu wenye ukwasi mkubwa na wasomi waliowekeza mjini Denver.

Hata hivyo kwa nini Josh alichagua Cherry Hills Village? Inaelezwa kwamba eneo hilo linafananishwa na Beverly Hills ya milimani. Ni mahali ambapo matajiri wa zamani na watu wenye nguvu mpya ya kifedha hukutana na kupiga stori zinazohusiana na biashara kubwa kubwa.

Faragha katika eneo hilo ndiyo thamani kubwa zaidi, kwani mabilionea wanapokwenda sehemu hiyo ni nadra sana kuonekana au kufikiwa na vyombo vya habari hususan waandishi wa habari wanaofuatilia maisha ya watu maarufu duniani (mapaparazi).

Cherry Hills Village ni miongoni mwa maeneo tajiri zaidi Marekani. Nyumba nyingi zipo kwenye maeneo makubwa zikiwa zimejificha nyuma ya barabara ndefu na miti mingi. Kwa mtu mashuhuri kama Josh, faragha hiyo ni muhimu kwake.

Majirani zake pia ni watu maarufu wakiwemo wanasoka wa zamani na wakurugenzi wakuu wa kampuni kubwa duniani na uamuzi wake wa kwenda kununua nyumba eneo hilo ni kama kujiunga na klabu ya kipekee ya watu wenye ushawishi mkubwa kifedha na kijamii. Licha ya kumiliki mjengo wa maana, lakini hakuna taarifa zozote kuhusu maisha binafs ya Josh hususan iwapo ana mchumba au watoto.

BOS 03

MWONEKANO WA NYUMBA

Nyumba ya Josh imejengwa kwenye eneo la zaidi ya ekari tano. Muundo wake umechanganywa kwa mtindo wa ranchi ya kisasa na anasa ya milimani ya Kimarekani. Yanapozungumziwa madhari ya anasa ya milimani ni yale mandhari ya kutengeneza.

Nyumba hiyo ina ukuta wa mawe, mbao kubwa na madirisha makubwa ya vioo yanayoruhusu mwanga mwingi wa asili. Inaonekana kuwa ni nyumba ya kifahari lakini kwa ndani kuna masingira ya joto fulani la kutengeneza.

Sehemu ya nje ya nyumba inatawaliwa na eneo la burudani, ikiwa na bwawa kubwa la kuogelea na pia kuna jiko la nje, oveni ya pizza na maeneo ya kukaa. Lakini, mandhari yake yamepambwa kwa mimea ya asili na njia binafsi za kutembea kwa miguu.

Unapoingia ndani ya nyumba ni kama uingiapo katika hoteli ya nyota tano, kwani kuna mapambo ya anasa yanayogharimu mamilioni ya fedha, vifaa vya hali ya juu na mwanga mwingi. Sebuleni kuna madirisha makubwa yanayoonyesha milima.

Unapoingia jikoni unakutana na vifaa vya kisasa vya kupikia, kaunta za marumaru na chelezo mbili za maandalizi ya chakula. Pia kuna chumba kinachotumika kuhifadhia vyombo, vyakula au vinywaji; kuandaa chakula kabla ya kupelekwa mezani na kuweka vitu visionekane ili jiko libaki safi.

Eneo la chakula katika nyumba hiyo linaweza kuchukua wageni hadi 20, pamoja na chumba cha kuhifadhi divai chenye uwezo wa kuweka chupa 1,500.

Kuna uwanja wa wa michezo nje wenye teknolojia za kisasa za aina mbalimbali ukiwa na uwezo wa kushuka chini ya ardhi na juu yake kupaki magari kadhaa. Mfumo wa nyumba hiyo yaani “smart home” unaruhusu kudhibiti taa, joto, usalama na muziki kupitia kifaa kimoja. Kuna gereji kubwa ya magari inayoendeshwa kwa mfumo wa nishati rafiki kwa mazingira (solar HVAC ya kisasa).

BOS 05

VYUMBA VYA KULALA, FARAGHA

Nyumba hiyo ina vyumba sita vya kulala, kila kimoja kikiwa na bafu lake. Chumba kikubwa kina ukubwa wa futi za mraba 2,000, kikiwa na eneo la kulala lenye dari ya juu, bafu la kifahari kubwa la kisasa, vyumba vitano vya nguo, eneo la mazoezi na matibabu. Hii ina maana kwamba kuna ofisi kabisa ya daktari wake kando ya chumba hicho.

Vingine vilivyomo ni gym kali ya kisasa, chumba cha yoga, sauna na chumba cha kupumzika baada ya mazoezi, huku kukiwa na burudani mbalimbali zinazoruhusu mtu kufurahia maisha kama michezo ya kisasa ya roboti, ukumbi mdogo wa muziki unaodhibiti vyema sauti kutoka, eneo la tajiri kukutana na wageni binafsi, ukumbi wa sinema wa kisasa, chumba cha michezo na baa.

BOS 02

MENGINEYO

Licha ya kwamba Josh kwa sasa ndiye mwenye mamlaka makubwa ndani ya Arsenal kutokana na hatua ya baba yake kuanza kujitenga na shughuli za kila siku za kiutendaji, lakini pia ana jukumu lingine zito la kusimamia klabu za michezo mingine zinazomilikiwa na mzazi wake huyo.

Kutokana na majukumu hayo familia hiyo imekuwa ikimlipa mishahara inayofikia Dola 10 milioni kila mwaka, huku pia akiwa na bonasi za mamilioni iwapo anafanikisha timu mojawapo kubeba ubingwa wa mchezo husika, huku pia akivuta mkwanja mwingine kutokana na uwekezaji wake binafsi katika masoko ya mitaji yaliyopo England na Marekani.

Kutokana na hayo yote Josh anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 500 milioni, akiwa na msururu mrefu wa mali binafsi anazomiliki ikiwamo majumba katika miji ya London (England), Paris (Ufaransa) na Los Angeles na New York (Marekani) na Ottawa (Canada), huku akimiliki pia ndege ndogo mbili alizonunuliwa na baba yake kwa ajili ya kumrahisishia safari za kikazi.

Licha ya utajiri alionao, lakini mwenye umri wa miaka 45 hapendi mambo makubwa kama kumiliki magari ya kifahari na pia starehe na mitoko ya kifahari kama walivyo watoto wa mabilionea wengi duniani. Baba’ke, Stan anamiliki utajiri wa Dola 26.8 milioni. Mbali ya Josh, pia bilionea huyo ana binti mmoja, Whitney Ann Kroenke.