Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaihakikishia EPL nafasi tano UCL

Muktasari:

  • The Gunners walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 nchini Ureno, juzi Jumanne usiku ambapo Kai Havertz aliingia akitokea benchi na kufunga bao la ushindi katika dakika za nyongeza. Bao hilo lilikuja baada ya lile la Martin Zubimendi kufutwa na VAR, huku Viktor Gyökeres akionekana kuwa ameotea katika maandalizi ya bao hilo.

LISBON, URENO: TIMU ya Arsenal imeihakikishia Ligi Kuu England kuwa na nafasi tano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuifunga Sporting Lisbon katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya mashindano hayo wa robo fainali.

The Gunners walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 nchini Ureno, juzi Jumanne usiku ambapo Kai Havertz aliingia akitokea benchi na kufunga bao la ushindi katika dakika za nyongeza. Bao hilo lilikuja baada ya lile la Martin Zubimendi kufutwa na VAR, huku Viktor Gyökeres akionekana kuwa ameotea katika maandalizi ya bao hilo.

Hata hivyo, Arsenal wanapaswa kumshukuru Raya ambaye alifanya mfululizo wa kuokoa hatari na kuwanyima wenyeji mabao. Awali, Maximiliano Araujo alipiga shuti kali lililookolewa na Raya kwa kugonga mwamba wa juu, kabla ya kumzuia Geny Catamo aliyepiga kichwa akiwa karibu kabisa na lango.

Baada ya mechi, Havertz alimsifu kipa huyo akisema: “Ni wa ajabu. Nafikiri bado anadharauliwa katika dunia ya soka, lakini kwangu kwa misimu miwili iliyopita ndiye kipa bora duniani. Ametuokoa mara nyingi sana.”

Raya pia alizungumzia kiwango chake akisema: “Nipo kwa ajili ya kusaidia timu kadri niwezavyo katika kila tukio, siyo tu kuokoa, bali pia kuongoza na kucheza mpira. Nafurahia sana na ushindi.”

Araujo akizungumzia tukio la kuokolewa kwa shuti lake na Raya, alisema: “Ulikuwa ni wakati muhimu. Tulifanya mashambulizi ya haraka nilipiga mpira vizuri lakini na nilifanikiwa kugusa mpira kidogo ukaenda kugonga mwamba. Hizi ni nyakati zinazoweza kubadilisha mchezo.”

Bao hilo linaipa timu ya Mikel Arteta faida kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa kwenye Uwanja wa Emirates Aprili 15, ambapo mshindi atakutana na Barcelona au Atletico Madrid kwenye nusu fainali.

Wakati huohuo, wapinzani wa Arsenal katika Ligi Kuu England pia wana sababu ya kushangilia baada ya kuthibitishwa kwa nafasi ya tano ya ziada katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa ushindi huo, Arsenal wameihakikishia England kumaliza angalau nafasi mbili za juu kwenye jedwali la mgawo, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA). Ni hispania pekee ndiyo inayoweza kuwazidi alama na hii itakuwa mara ya pili mfululizo kupata nafasi ya ziada. Msimu uliopita, Newcastle United walinufaika baada ya kumaliza nafasi ya tano.

Kwa sasa, Liverpool wanashika nafasi ya tano wakiwa na mechi saba mkononi, lakini wana pointi moja tu mbele ya Chelsea. Brentford na Everton wako pointi tatu nyuma ya nafasi tano bora, hali inayofanya ushindani kuwa mkali.

Habari hizi pia zinaongeza matumaini kwa Manchester United na Aston Villa, ambazo kwa sasa ziko ndani ya nne bora, zikiwa mbele ya Chelsea kwa tofauti ya pointi saba na sita mtawalia.