Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geay kukiwasha New York Marathon leo

Riadha Pict
Riadha Pict

Muktasari:

  • Geay ndiye anashikilia rekodi ya Tanzania katika mbio ndefu (marathon) ambapo katika mbio za New York atakutana na ushindani kutoka kwa nyota wengi akiwemo mshindi wa mbio hizo wa mwaka 2023, Tamirat Tola kutoka Ethiopia ambaye pia ni mshindi wa marathoni za Olimpiki za Paris 2024.

MBIO za New York City Marathon zinatazamiwa kufanyika leo nchini Marekani zikianza saa 2:00 asubuhi (sawa na saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania) zikishirikisha wanariadha mbalimbali wa kimataifa huku Mtanzania, Gabriel Geay akiwa ni miongoni mwa wababe ambao watashiriki.

Geay ndiye anashikilia rekodi ya Tanzania katika mbio ndefu (marathon) ambapo katika mbio za New York atakutana na ushindani kutoka kwa nyota wengi akiwemo mshindi wa mbio hizo wa mwaka 2023, Tamirat Tola kutoka Ethiopia ambaye pia ni mshindi wa marathoni za Olimpiki za Paris 2024.

Mtanzania huyo alianza kukimbia mbio za viwanjani kisha akapanda hadi mbio za marathoni mwaka 2021 na kuvunja rekodi ya taifa kwa kutumia muda wa saa 2:04:55 katika mchezo wake wa kwanza wa marathon huko Milan ambako uchezaji huo ulimwezesha kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

R4
R4

Geay aliendelea kung’ara zaidi ambapo mwaka 2022 alimaliza wa saba katika mbio za Marathoni za Dunia ambazo zilifanyika Eugene, Oregon nchini Marekani akitumia muda wa saa 2:07:31 na mwaka huo pia alivunja rekodi yake ya taifa ya marathoni na kuweka mpya kupitia mbio za Valencia za nchini Hispania kwa muda wa 2:03:00 baada ya kushika nafasi ya pili.

Alishika pia nafasi ya pili katika mbio za Boston Marathon za 2023 nchini Marekani kwa muda wa saa 2:06:04, akishika nafasi nne mbele ya bingwa wa Olimpiki mara mbili mfululizo mwaka 2016 na 2021, Eliud Kipchoge wa Kenya aliyemaliza wa sita kwa 2:09:23.

Marathoni za Olimpiki za Paris 2024 huko Ufaransa, Geay alishiriki lakini akashindwa kufanya vizuri kutokana na changamoto ya hali ya hewa na pia majeraha ambayo alikuwa nayo.

R3
R3

Kabla ya kuondoka kwenda kushiriki mbio za leo huko New York, Mwanaspoti lilimtembelea Geay mazoezini kwake kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Ilboru iliyopo jijini Arusha kujionea maandalizi yake na haya ndiyo aliyosema:


MAANDALIZI YAKE

Alisema maandalizi kwa ajili ya mbio za leo za New York Marathon yalikuwa mazuri tangu aliporejea kutoka katika Olimpiki ya Paris na anatarajia kupata matokeo mazuri.

“Japo ni mara yangu ya kwanza kushiriki New York lakini kulingana na nilivyofuatilia na watu ambao wamekuwa wakikimbia mbio hizo ni wale ambao huwa nashindana nao, nawashinda wakati mwingine na wao wananishinda wakati mwingine, kwahiyo naamini na mimi nitakuwa kwenye nafasi hizo za ushindi.”

R2
R2

WALA HAOGOPI

Alisema hahofii chochote, licha ya kwamba mbio hizo zinashirikisha mabingwa wa marathoni akiwamo mshindi wa mbio hizo mwaka 2023, Tamirat Tola ambaye pia ni mshindi wa marathoni ya Olimpiki ya Paris 2024 pamoja na mshindi mara mbili wa mbio za Boston Marathon, Evans Chebet kutoka Kenya.

Nyota wengine watakaoshiriki leo ni Geoffrey Kamworo, Abel Kipchumba, Albert Korir, Wesley Kiptoo wote kutoka Kenya, Bashir Abdi (Ubelgiji), Abdi Nageeye (Uholanzi), Elkanah Kibet, CJ Albertson (Marekani), Callum Hawkins (Great Britain), Addisu Gobena kutoka Ethiopia na wengine wengi.

“Naamini nitafanya kitu kikubwa ambacho haijawahi kushuhudiwa New York, kama nitakuwa fiti kwa asilimia zote lazima nitashinda,” alisema.

Alizungumzia ushindani uliopo baina yake na mwanariadha kutoka Kenya, Evans Chebet ambaye pia anashiriki mbio hizo, akisema anatarajia kufanya vyema mbele yake licha ya kwamba mara zote ambazo ameshindana naye kwenye mbio za Boston Marathon hakuwahi kumshinda.


SIJAFANYA KITU MWAKA HUU

Anasema mwaka jana 2023 kwake ulikuwa ni mwaka wa mafanikio kwake ambapo aliweka matarajio makubwa zaidi pia mwaka huu lakini mambo yameenda tofauti na alivyotarajia baada ya kushindwa kutamba katika mbio mbili za Boston Marathon na Olimpiki.

“Mwaka huu nilianza vibaya ikiwamo kushindwa kumaliza mbio ambazo nimeshiriki, lakini nataka nikafanye vizuri na kuwafurahisha Watanzania wote ambao wamekuwa wakiweka matumaini kwangu.”

“Ninapata wakati mgumu ninapoona nashindwa kupata matokeo au kushindwa kufikia malengo ikiwamo kushindwa kumaliza mbio au kushindwa kumaliza katika nafasi za juu.”

Aliweka wazi kuwa kulingana na jinsi ambavyo amejifua kwa miezi mitatu tangu alipotoka Olimpiki Paris mwezi Julai, anajiwekea asilimia kubwa kwenda kufuta makosa yote na kufunga mwaka kwa namna ya kipekee.

R1
R1

HALI YA HEWA

Alisema si kwamba alienda Paris kwenye michezo ya Olimpiki akiwa mgonjwa kama wengi wanavyodai kwamba ndio ilichangia yeye kushindwa kumaliza mbio, ila kwake changamoto kubwa ilikuwa ni hali ya hewa.

“Changamoto kubwa ambayo nilikutana nayo Olimpiki ni hali ya hewa. Hali ya hewa huwa ina upendeleo kwa mmoja na changamoto kwa mwingine.

“Kwangu hali ya hewa ya majira ya joto ni changamoto ila kama ingekuwa ni msimu wa baridi kiasi kwangu ingekuwa ni wakati mzuri sana”.

Anafunguka licha ya kwamba hali ya hewa kwake ilikuwa ni kikwazo, lakini pia changamoto nyingine ilikuwa ni milima ambayo ilimfanya kushindwa kumaliza mbio kwani hakufanyia mazoezi mazingira kama hayo wakati wa maandalizi.

Ukizingatia alitoka kuwa majeruhi hivyo hakuwa na uwezo wa kupanda milima na kushuka kwa sababu ya majeraha ambayo alikuwa nayo kwani mazoezi yake mengi alifanya katika sehemu ya tambarare.


HASIKILIZI MANENO YA WATU

Geay anadai maneno ambayo yanasemwa na watu kwamba amekuwa ‘akijivunja’ ili kukwepa Michezo ya Olimpiki ambayo mara nyingi tuzo huwa ni heshima na badala yake kukimbilia kushiriki mbio za pesa, kwake ameshazoea na wala haogopi kwani hayawezi kumwondoa katika reli na kikubwa kwake ni kuendelea kupambana zaidi na kutimiza malengo ambayo amejiwekea.

“Uwepo wangu Paris ulifanya bendera ya Tanzania ipepee na kufika kwangu pale na kushiriki ni jitihada zangu binafsi, kwahiyo kwa mtu kuongea hainipi shaka kwa sababu ningekuwa sijafanya vizuri huko nyuma nisingeenda Olimpiki”.

“Kila mmoja anatamani kwenda Olimpiki ila wanashindwa kwa sababu wanashindwa kufikia vigezo na kufika vigezo vya Olimpiki sio jambo dogo ni kitu kikubwa sana”.

Anasema watu wanatakiwa kuelewa kwamba kufikia kwenye viwango vikubwa vya dunia ni jitihada za mtu binafsi kujitoa na kufanya mazoezi kwa bidii.

“Sio sisi peke yetu tuliofanya vibaya, wapo wengi na wengine wengi walijitoa. Na ukiangalia tulishiriki wanariadha wanne ambao kupata medali ni bahati, lakini kama tungekuwa zaidi ya hapo angalau ingeweza kutokea jambo.

“Tanzania kupata medali kwa wanariadha wanne pekee waliotumwa Olimpiki ni bahati ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya, Uganda, Ethiopia ambazo zilipelekea washiriki wengi.”


OMBI KWA SERIKALI NA RT

Alitumia fursa hii kuiomba Serikali kupitia Baraza la Michezo (BMT) na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kuweka nguvu kubwa sana kuzalisha wanariadha wengi ambao wataweza kufikia vigezo vya Olimpiki na mashindano mengine ya dunia.

“Mashindano ya kimataifa yanazidi kuwa magumu kama sasa hivi. Mwakani kuna Mashindano ya Dunia ambayo yatafanyika Tokyo, Japan. Vigezo vya kufuzu vimesogezwa mbele ambavyo ni kukimbia kwa muda wa saa 2:06:30 kwa wanaume na saa 2:23:30 kwa wanawake.

“Ukifikia muda huo ndio unaweza kwenda kwenye mashindano hayo na kwa Tanzania waliowahi kukimbia kwenye rekodi za taifa chini ya 2:06:30 ni mimi na Alphonce Simbu tu tangu Tanzania izaliwe”.


CHANGAMOTO RIADHA HII HAPA

Geay ambaye ana taasisi yake ya kuibua na kulea vipaji vya wachezaji wa riadha, anasema wachezaji chipukizi ni wengi sana lakini moja ya changamoto ni kukosa sapoti na vijana kuridhika mapema.