Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geay anakula mara tano kwa siku

UZI tuliishia sehemu ambayo Geay anazungumzia kuhusu maisha yake ya Chuo cha Utumishi wa Umma Singida na jinsi alivyokutana na wanariadha wakubwa wakifanya mazoezi na kumpa ushirikiano wa kutosha.

Lakini kumbuka kuwa tuliangalia mazingira ambayo mwanariadha huyo amezaliwa ikiwa ni eneo ambalo linajihusisha na ufugaji, tukaona hata mashindano yake ya kwanza yalikuwa pale Manyara, kabla hajasafiri kwenda Angola ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwake nje ya nchi lakini mwenyewe anasema kuwa hakufanikiwa kufanya vizuri lakini ikiwa ni ziara ambayo ilimsaidia sana kwa kuwa alijifunza mambo mengi kuhusu mchezo huo.

Anasema moja ya jambo ambalo amekuwa akijifunza mara nyingi ni kuwaza mambo makubwa kuliko uwezo wake na hii ndiyo imemsaidia na kumfikisha hapa alipo leo.

Leo tunaendelea na sehemu ya pili ambayo inazungumzia jinsi ambavyo aliondoka Manyara na kuanza rasmi maisha ya Arusha na kwanini alifanya hivyo.

“Baada ya kumaliza chuo niliwasiliana na kocha wangu Thomas na akaniambia kuwa natakiwa kuja Arusha kama nataka kuwa mwanariadha mzuri, kwa kuwa nilikuwa nafahamiana naye kwa muda mrefu kuanzia nikiwa nashiriki mashindano ya Umisseta wala haikuwa shida kubwa sana.

“Unajua wakati tunafanya mashindano ya Umisseta hapa kwenye Uwanja wa Ilboru ndiyo ilikuwa sehemu ambayo tunafanyia mashindano hiyo aliponiambia nifike hapa halikuwa tatizo kwangu.”


AMKUTA FABIAN JOSEPH

Geay anasema mmoja kati ya mtu ambaye alikuwa akimvutia sana kwenye riadha kwa kipindi chake chote ni Fabian Joseph, anasema alishtuka baada pia ya kumkuta akiwa kwenye uwanja huohuo ambao naye alikuwa akifanya mazoezi.

“Kuanzia wakati naanza riadha nilikuwa navutiwa sana na wanariadha wakubwa, mmoja alikuwa Fabian Joseph yule paleeee, (ananionyesha alipo), nilipofika hapa Ilboro kwa mara ya kwanza nilimkuta naye aliwa anafanya mazoezi hapa, ukweli nilifurahia sana na hadi leo yupo.

Ingawa wapo wengi ambao nawakubali na nilikuwa nawafuatilia lakini huyu ni mmoja wao kati ya wale bora kwangu, hata leo bado amekuwa akinishauri, name nazungumza naye mambo mengi sana, riadha ni mchezo ambao pia unatakiwa kusikiliza sana kwa wale waliokutangulia."


KWANINI ILBORU SIYO UWANJA MWINGINE ARUSHA?

Kama nilivyosema mwanzoni, ukifika kwenye uwanja huu ni rahisi kukuta wanariadha 100 na zaidi wakiwa wanafanya mazoezi asubuhi hivyo inaonekana kuwa ni sehemu muhimu sana kwa wanariadha wa mkoa wa Arusha.

“Jaribu kuwauliza wanariadha wote wakubwa watakuambia kuwa walifanya mazoezi hapa, nafikiri tangu enzi za kina Filbert Bayi kama kambi ya mazoezi haikuwa hapa basi utakuta kuna wakati alikuja kukaa hapa kwa ajili ya maandalizi, huku ni pazuri kwa kuwa kuna hali nzuri ya hewa.

“Maandalizi ya riadha yanafaa sehemu yenye baridi kali kama hapa, lakini pia utulivu huku hakuna kelele na hakuna watu wanapita uwanjani, hii inamsaidia mtu kuwa kwenye maandalizi mazuri kwa kuwa hakuna mtu anayepita uwanjani kama vilivyo viwanja vingine hapa Arusha,” alisema mwanariadha huyo ambaye anaishi karibu na uwanja huo.


RATIBA YAKE KWA WIKI KIBOKO

Geay mwenye umri wa miaka 26, anasema hakuna kitu ambacho anafanya mwenyewe, bali kila kitu anaelekezwa na kocha wake kukifanya na kila siku kuna utaratibu tofauti.

“Mimi nakimbia marathoni hivyo mara nyingi kila siku ina utaratibu wake, ukiona hapa uwanjani umewakuta wanariadha wengi lakini kila mmoja ana malengo yake.

“Kuna wale ambao wanakimbia mbio fupi wapo hapa, kuna wengine wanakimbia marathoni wapo lakini tazama hata hao wengine wanaopanda na kushuka milimani ni programu tofauti, lakini hapa hapa kuna wengine ndiyo wanaanza riadha sasa.

Anasema ratiba yake kwa wiki imebana sana kwa kuwa kila siku anatakiwa kuwa na programu maalumu awe na mashindano au asiwe nayo.

“Kila Jumatatu asubuhi sana natakiwa kuwa barabarani, naanza kupasha mwili joto nakimbia pembeni ya barabara kilomita 20 narudi nyumbani nakunywa chai napumzika.

“Jumanne ndiyo kama leo, nakuja uwanjani, naweza kutumia muda mrefu kidogo kuandaa mwili wakati mwingine hata saa mbili baada ya hapo nafuata programu ya kocha wangu anataka nifanye nini kwa siku hiyo.

Geay ambaye kila akishamaliza mazoezi lazima avae nguo yenye nembo ya kampuni ya Adidas (tutaelezana mbele kwanini) anasema Jumatano yeye huwa anarudi barabarani.

“Jumatano sifanyi kama ilivyo Jumanne au Jumatatu, huwa nakimbia kilomita 12 au 15, na nikishamaliza narudi napumzika, lakini siyo jambo la ajabu kama nitafanya tena mazoezi jioni kidogo, Alhamisi narudi uwanjani Ijumaa na Jumamosi barabarani halafu siku yangu ya mapumziko ni Jumapili tu.


ANAKULA MARA TANO KWA SIKU

Mimi mara nyingi sili chakula kwa kuwa natakiwa kula kwa utaratibu asubuhi, mchana, usiku, hapana mimi huwa nakula nikiwa na njaa, hata mara tano kwa siku nakula.

“Naweza kuamka asubuhi nikisikia njaa nakula, mchana nakula na wakati mwingine saa nane nikisikia njaa nakula, ikifika jioni nakula. Huu ndiyo utaratibu wangu mara nyingi sina muda maalumu wa chakula, na ninachokula ni kile ambacho nimeelekezwa kula.