Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DROO CHAN 2024: Ugumu, wepesi uko hapa

CHAN Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo litafanyika kuanzia saa 2:00 likiongozwa na kusimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika (Caf) likihusisha timu 18 zilizofanikiwa kufuzu fainali hizo zikiwemo Uganda, Kenya na Tanzania ambazo ni wenyeji.

Droo ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) 2024 itafanyika keshokutwa Jumatano jijini Nairobi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta.

Tukio hilo litafanyika kuanzia saa 2:00 likiongozwa na kusimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika (Caf) likihusisha timu 18 zilizofanikiwa kufuzu fainali hizo zikiwemo Uganda, Kenya na Tanzania ambazo ni wenyeji.

Fainali hizo kwa mujibu wa kalenda ya mashindano ya Caf, zitafanyika katika miji ya Nairobi, Kampala, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia Februari Mosi had Februari 28 mwaka huu.

Katika droo hiyo ya keshokutwa, timu ambazo zitapangiwa makundi ya fainali za Chan 2024 ni Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Senegal, Morocco, Guinea, Madagascar, Rwanda, Sudan,  Mauritania, Niger, Angola, Congo, Burkina Faso, Nigeria, Burkina Faso, Afrika ya Kati na DR Congo.

CHA 01

Vyungu vitatu

Kutakuwa na vyungu vitatu katika uchezeshaji wa droo hivyo ambavyo vitatoa timu za kuingia katika makundi ya fainali za Chan 2024.

Upangaji wa vyungu hivyo umetokana na pointi ambazo kila timu imevuna kulingana na ushiriki wake kwenye fainali zilizopita za mashindano hayo.

Tanzania, Kenya na Uganda zenyewe hazihusiki katika vyungu hivyo kwa vile ni timu wenyeji.

Chungu cha kwanza kina timu mbili tu ambazo ni Morocco na Senegal wakati chungu cha pili kikiwa na timu tano ambazo ni Guinea, Madagascar, Rwanda, Sudan na Zambia.

Chungu cha tatu kitakuwa na timu za DR Congo, Nigeria, Niger, Angola, Mauritania, Congo, Burkina Faso na Afrika ya Kati.


Wanyonge wachache

Ni timu tatu tu kati ya 18 shiriki ambazo hazijawahi kuonja ladha ya mashindano hayo na hivyo fainali za mwaka huu zitakuwa za kwanza kwao kushiriki.

Timu hizo ni Kenya, Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini nyingine 15 zimewahi kushiriki na kuishia katika nafasi tofauti katika fainali hizo.

Uganda na DR Congo ndio timu zinazoongoza kwa kushiriki fainali hizo mara nyingi ambapo kila moja hii ni mara yake ya saba kucheza fainali za Chan zikifuatiwa na Morocco, Zambia, Rwanda, Niger na Angola ambazo fainali za mwaka huu zitakuwa za tano kwa kila moja kushiriki.

Timu ambazo zitashiriki fainali hizo kwa mara ya nne ni Guinea, Sudan, Burkina Faso, Nigeria na Mauritania, Tanzania itakuwa inashiriki kwa mara ya tatu na Madagascar yenyewe  inacheza mashindano hayo kwa mara ya pili.


CHA 02

Morocco yabeba jahazi Afrika Kaskazini

Kanda ya soka ya Kaskazini mwa Afrika (Unaf) imekuwa mbabe wa fainali za Chan kwani ndio inaongoza kwa kutwaa taji hilo mara nyingi ikifanya hivyo mara nne kati ya saba zilizopita ikifuatiwa na kanda ya Afrika ya Kati iliyotwaa mara mbili na Afrika Magharibi iliyotwaa mara moja.

Libya, Morocco na Tunisia ni timu tatu zilizoiheshimisha kanda ya Unaf kwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ambapo Morocco imechukua mara mbili huku Libya na Tunisia kila moja ikitwaa mara moja.

Hata hivyo katika fainali za mwaka huu, kanda ya soka ya Kaskazini mwa Afrika itawakilishwa na Morocco tu kutokana na Algeria, Misri na Libya kuamua kujitoa huku Tunisia ikiwa haijafuzu.


Afrika Magharibi yatawala

Idadi ya timu sita zitashiriki fainali hizo za Chan mwaka huu zikiwakilisha kanda ya soka ya Magharibi mwa Afrika (Wafu) ambazo ni Mauritania, Senegal, Burkina Faso, Nigeria, Niger na Guinea.

Hilo linaifanya Wafu kuwa kanda iliyo na idadi kubwa ya timu katika fainali hizo ikifuatiwa na kanda ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambayo inawakilishwa na timu tano ambazo ni Sudan, Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda.

Kanda ya Kusini mwa Afrika (Cosafa) na kanda ya kati (Uniffac) kila moja inawkailishwa na timu tatu huku Unaf ikiwa na timu moja.

Timu tatu zinazowakilisha Cosafa ni Zambia, Angola na Madagascar na zinazowakilisha Uniffac ni DR Congo, Congo na Afrika ya Kati.


CHA 04

Taifa Stars na deni

Kwa kundi lolote ambalo timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itapangwa, itakuwa na kibarua cha kulipa deni la unyonge ambao imekuwa nao kwa miaka 15 tangu mashindano hayo yalipoanzishwa.


Unyonge huo ni wa kuishia hatua ya makundi katika fainali mbili ilizowahi kushiriki hapo nyuma ambazo ni fainali za 2009 na fainali za 2020 hivyo inapaswa kuvuka zaidi ya hapo katika fainali za awamu hii.


Tanzania haina presha

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ alisema kuwa wapo tayari kukabiliana na timu yoyote watakayopangwa nayo katika fainali hizo.

“Timu yoyote ambayo imefuzu kushiriki Chan ni nzuri na haijafanya hivyo kwa kubahatisha hivyo sisi tunajiandaa kwa droo tukiamini kila timu ni bora na tutapaswa kupambana kuhakikisha tunaleta heshima nyumbani,” alisema Morocco.

Mshauri wa benchi la ufundi la Taifa Stars, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema kuwa hakuna cha kuhofia katika hayo mashindano.

“Tanzania haina uoga wa kucheza na timu yoyote katika Chan kwa vile tuna wachezaji ambao wanatoka katika ligi yetu iliyo bora kwa sasa na tumeshawahi kushiriki huko nyuma. Ukiongezea faida ya kuwa nyumbani, nadhani tutafanya vizuri muhimu ni Watanzania kuiunga tu timu mkono,” alisema Julio.