Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama kaifumua hat trick ya Okwi akijenga yake mpya

CHAMA Pict


CLATOUS Chama, mzaliwa wa Nchanga na mkaazi wa Nndola, Zambia, ameandika historia ya aina yake.


Chama, mwananusu fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016 akiwa na Zesco United ya Zambia, amekuwa mchezaji wa pili wa kigeni baada ya Emmanuel Okwi wa Uganda, kuitumikia Simba katika vipindi vitatu tofauti.

TUNI 03

CLATOUS CHAMA

Chama aliyejiunga na Simba mara ya kwanza mwaka 2019 akitokea Lusaka Dinamos ya Zambia. Akahudumu kwa misimu miwili hadi 2021 alipotimkia Morocco katika klabu ya RS Berkane. Mwaka 2022 akarudi Simba baada ya kuachana na Berkane kutokana na  matatizo ya kifamilia.

Kipindi hicho, Chama alifiwa na mkewe na ndugu wa mwanamke walitaka kuwachukua watoto, kitu ambacho yeye hakukitaka. Lakini, kwa kuwa alikuwa mbali (Morocco), asingeweza kuwachukua na kukaa nao yeye...ndipo akapambana kurudi Simba, ambako ni karibu na kwao.

Akakaa tena Simba hadi 2024 alipotimkia kwa mahasimu wa waajiri wake, Yanga. Akasema anajiunga na Yanga ili ashinde taji la Afrika, huku Simba wakisema wamemuacha kwa sababu hana kipya cha kuwapa.

CHAM 04

Maisha ya Chama ndani ya Yanga hayakuwa mazuri, kwani hakupata muda mwingi wa kucheza. Baada ya msimu mmoja, akaondoka na kujiunga na Singida Black Stars. Na sasa 2026 anarejea tena Simba kwa mara ya tatu. Hii ndiyo inaitwa hat- trick, kama ingekuwa magoli ya kufunga.

CHAM 02

EMMAUEL OKWI

Alijiunga na Simba 2009 akitokea SC Villa ‘Jogoo’ ya Uganda. Kwa kuwa alikuwa chini ya miaka 18, alitakiwa kusubiri kwa nusu msimu hadi Januari 2010 ndipo akaanza kucheza.

Alidumu Simba  hadi 2012 alipoondoka na kutimkia Austria kwenye klabu ya RB Salzburg kufanya majaribio.

Wakati huo klabu hiyo ilikuwa chini ya unahodha wa Mganda mwenzake, Ibrahim Sekagya. Yeye ndiye aliyempendekeza na kumpatia nafasi hiyo ya majaribio. Lakini Okwi ni kama alikuwa bado na utoto mwingi, alishindwa kuendelea na majaribio akisema anaumwa...akaondoka.

Nafasi yake ya majaribio ikachukuliwa na Sadio Mane wa Senegal, akafaulu na kilichofuata baada ya hapo ni historia.

Okwi akarejea Simba ambao moja kwa moja walimuuza Etoile du Sahel ya Tunisia.

CHAM 01

Huko nako hakudumu sana, akarudi kwao Uganda na kujiunga na klabu yake aliyokulia, SC Villa. Dirisha dogo la 2014 akajiunga na Yanga na kuhudumu kwa nusu msimu. Mwaka 2015 akasaini Simba kwa mara ya pili na kudumu hapo kwa msimu mmoja...akaondoka.

Safari hii alienda Denmark kuniunga na Sönderjyske Fodbold. Mwaka 2017 akarudi Simba kwa mara ya tatu na kudumu hadi 2019 alipotimkia Al Ittihad ya Misri, baada ya kung’aa katika AFCON 2019 zilizofanyikia nchini humo.

Kwa kusaini Simba mara tatu, Okwi akawa mchezaji wa kwanza raia wa kigeni kupiga hat-trick ya mkataba klabuni hapo.

Wakati Okwi akitimkia Misri, huku nyuma Simba wakamsaini Chama...walipishana kidogo tu. Na sasa Chama anaifikia rekodi ya Okwi ya kupiga hat-trick ya mkataba. Okwi aliporudi kwa mara ya tatu alikuwa hatari zaidi kuliko zile mara mbili za kwanza, kwa maana ya mabao.

Kwani hiki ndicho kipindi ambacho aliibuka mfungaji bora na kuisaidia Simba kurudisha ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya miaka minne, na kufuzu hatua ya makundi hadi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chama naye anaianza safari yake ya mkataba wa tatu ndani ya Simba, tuone atafanya nini kikubwa zaidi ya alichokifanya. Je, naye ataisaidia Simba kurudisha ubingwa wa Ligi Kuu? Atakuwa mfungaji bora, au atafanya nini cha kulingana na Okwi...au kuzidi kile alichokifanya yeye mwenyewe hapo kabla? Tusubiri!